visima vingi vilivyochimbwa kwa ajili ya maji mbadala kwa wakazi wa North Mara havina maji
VISIMA VINGI WALIVYOCHIMBIWA WAKAZI WA
NORTH MARA HAVIJAWAHIN KUFANYA KAZI KWA KUKOSA MAJI.
Na Anthony Mayunga-Nyamongo
Septemba 3,2012.
TATIZO
la ukosefu wa maji linaendelea kuwatesa wakazi wanaozunguka mgodi wa African
Barrick North Mara ulioko Nyamongo wilayani Tarime ,kutokana na visima vingi
vilivyochimbwa kama vyanzo mbadala kutokuwa na maji.
Mwaka
2009 kamati za bunge mara baada ya kujiridhisha kuwa maji yam to Tighite
hayafai kwa matumizi kutokana na kuathiriwa na maji ya sumu yaliyovuja kutoka
mgodi wa Gokona.
Uchunguzi
wa blogu hii ulibaini kampuni haijachimba visima maeneo mengi kama ilivyoagizwa
badala yake inasambaza maji kwa kutumia magari yake,huduma ambayo wananchi
wanadai inawafanya wasichimbe visima ili wawe wanachota kwa wakati wanaotaka si
kama wanavyopelekewa kwa muda maalum.
Pia
visima vingi vilivyochimbwa na halmashauri havina maji ,ingawa serikali imekuwa
ikijinasibu kuwa wameishachimba visima kwa wakazi wanaozunguka mgodi huo.
Uchunguzi
ulibaini kuwa katika kisima kilichoko kitongoji cha Nyabikondo kijiji cha
Kewanja kata ya Kewanja kilichochimbwa na halmashauri hakina maji ,hata bomba
hakuna na eneo lote limegeuka kichaka.
Katika
kitongoji cha Kemambo kisima
kilichochimbwa na kampuni ya African Barrick North Mara hakina maji hali ambayo
inapelekea wananchi wa vitongoji hivyo kulazimika kupanga misululu kusubiri
magari ya kampuni kuwasambazia maji ambayo hawajui yanakotolewa.
Pia
kisima kingine katika eneo la Kenyatanka kilichochimbwa na kampuni hiyo
hakifanyi kazi kwa kuwa hakina maji,hali ambayo inawapelekea wananchi kwenda
kuchota maji kwenye kisima kingine kilichoko sekondari ya Ingwe na shule ya
msingi Nyamongo kilichochimbwa na halmashauri ya wilaya.
Visima
viwili kwa kijiji kizima ndivyo vina maji ambavyo ni kilichoshuleni na
kitongoji cha Mjini kati ambacho kimechimbwa na shirika la Japani (Jaica)
wengine kwenye lambo la Kewanja ambalo maji yake hayafai kwa matumizi ya kunywa
wala kupikia .
Wanne
Mwita mlinzi wa lambo hilo alisema kuwa maji ya lambo hilo ambalo lilikuwepo
lakini kampuni imesaidia kulipanua hayafai kwa matumizi ya kunywa,wala kupikia
lakini kutokana na tatizo la maji wengine huyatumia kwa kupikia na kuoga.
Hata
hivyo alisema liko hatarini kuziba kwa kuwa linazidi kujaa tope kutokana na
kuwa limetengezwa vibaya,hali ambayo ililalamikiwa na baadhi ya wananchi kuwa
wanalazimika kutumia maji yasiyokuwa safi na salama kutokana na serikali
kuwapuuza kwa kutoa taarifa za uongo.
Fanuel
Sasi mkazi wa kijiji hicho alisema kuwa visima vilivyochimbwa hapakuwahi
kufanywa tafiti kabla ili kujua kama kuna maji nan i salama ama eneo
limeathiriwa na sumu kutoka mgodini,hata ufuatiliaji wa halmashauri haupo ndiyo
maana eneo la kisima limegeuka kuwa kichaka kabla ya kutumika.
Diwani Kibasuka.
Diwani
wa kata ya Kibasuka Yusuph Moya (CCM)alisema eneo lake ndilo liliathiriwa na
maji ya sumu kwa kuua na viumbe hai lakini hawajahi kuchimbiwa visima.
“Wegita
na Nyarwana hawana maji wanatumia vyanzo vya kienyeji,visima vimechimbwa
Nyakunguru kuna vya Jaica na halmashauri ,vitongoji vipo saba vitatu vya
Nyamange,Nyakunguru na Nyamuma vina maji lakini Nyakwirambe,Itandura,Nyamichare
na Turuturu havina maji,hakuna maelezo tunayopewa”alisema kwa uchungu.
Mhandisi wa maji wilaya.
Vita
Mkubwa mhandisi wa maji wilaya ya Tarime katika hali ambayo inaonyesha hajui
walichimba visima vingapi na wapi na kama vina maji na havina alisema ,anaomba
apewe muda awasiliane na wenzake ili kujua ukweli wake ndipo ataeleza.
“Niko
kwenye kikao mkoani ,lakini naomba muda ili nifuatilie hilo tatizo maana
nashindwa kukujibu ,vipo tulivyochimba sisi na Jaica,kama huna nafasi ya
kukutana kesho tuongee nitakupigia baada ya kuwasiliana na wenzangu,”alijibu.
Mgodi.
Mmoja
wa maafisa habari mgodini hapo aliyejitambulisha kwa jina la Robert alipoulizwa
alidai kuwa yuko mbali na ofisi na kudai kuwa yupo Shayo na kuahidi kutoa namba
yake kwa maelezo zaidi.
Hata
hivyo badala ya kutoa namba yake alidai ametoa namba ya mwandishi kwa Shayo
ambaye atapiga,alipotakiwa kutoa namba ya shayo aliahidi kutuma,hata hivyo
alipotafutwa tena hakutaka kupokea simu ,hadi tunakwenda mitamboni Shayo
hakupiga kama walivyoahidi.
Mwisho,inaendelea.
Nilifanyiwa unyama na kaka yangu
| Nilifanyiwa unyama na kaka yangu | Send to a friend |
| Sunday, 02 September 2012 07:24 |
Anthony Mayunga UKATILI wa kijinsia unaendelea kushika kasi nchini ambapo hivi karibuni, mkazi mmoja wa Kijiji cha Kemugesi, wilayani Serengeti mkoani Mara amembaka dada yake na kasha kumfunga porini kwa zaidi ya saa saba, huku yeye akitokomea kusikojulikana. Kijana huyo, jina tunalo alitenda unyama huo saa 1:00 asubuhi ya Julai 22, mwaka huu, huku taarifa nyingine zikidai kuwa kijana huyo pia aliwahi kumtendea ukataili kama huo shangazi yake. Akisimulia mkasa huo, binti aliyeathirika na ukatili huo(Jina tumelihifadhi kwa sababu za kimaadili), alisema kuwa kaka yake huyo alimbaka huku akiwa amemsokomeza nguo ya ndani mdomoni kumzuia asipige kelele. “Kaka alinibaka akiwa ameniwekea nguo yangu ya ndani mdomoni, huku akinibana nisipige kelele. Kisha akanifunga kwenye mti na nilikaa kuanzia saa 5 asubuhi hadi saa 12 jioni,” anasimulia binti huyo mwenye umri wa miaka 15. Anaelezea kuwa kaka yake huyo ambaye wanachangia baba, alimwomba aende naye shambani akamsaidie kuvuna pamba na ndipo alitekeleza unyama huo. Binti huyo ambaye ni mmmoja wa watoto 29 wa baba yao aliye na wake wanne anasema kuwa licha ya kupata maumivu makali kutokana na kubakwa, kaka yake huyo pia alimpiga sana na kumsababishia maumivu makali sehemu mbalimbali za mwili. Hata hivyo, mbali na binti huyo kufanyiwa unyama, baba yake mzazi anahaha kuhakikisha kwamba binti huyo na mama yake wanamaliza suala hilo nyumbani akidai kuwa kijana wake anasumbuliwa na majini na kwamba akifungwa anaweza kufia jela. Ilivyotokea Binti huyo anasimulia kuwa siku ya Jumapili Julai 22, saa 1:00 asubuhi mwaka huu, walikwenda na kaka yake huyo kuvuna pamba wakiwa na kijana wao wa kazi, anayewasaidia kuchunga ng’ombe. "Tulivuna pamba bila matatizo, kwenye saa 4:45 asubuhi akasema tukachume mahindi shambani kwetu kwa ajili ya kwenda nayo nyumbani kwa ajili ya kuchoma. Tukatoka vizuri hadi tulipoacha madumu ya pamba. Nikakaa, lakini yeye akamwagiza kijana wa kazi arudi shambani kumbe, alitaka kutekeleza nia yake. Hapo alinivamia na kunikaba shingoni,"anasema kwa unyonge na kuongeza: "Alinibeba na kukimbia nami hadi kichakani na kuchana nguo yangu ya ndani, gagulo na kuniwekea nguo ya ndani mdomoni huku amenibana shingo, akaanza kunibaka. ...Nilipata maumivu makali sana, alichukua muda mrefu akinifanyia unyama huo.” “Damu zilivuja sana na baada ya kumaliza akanipiga na kwenda kunifungia kwenye mti, kisha akanipiga teke na kusema kuwa nitafia hapo na nyumbani hawataniona tena,” anaeleza binti huyo. Anasema kuwa kijana wao wa kazi aliposikia kelele alifika eneo la tukio, lakini kaka yake huyo alimfukuza na kutishia kumuua na kuwa akisikia popote kasema jambo hilo, atamuua. “Nilihangaika sana kujinasua, nikawa nasugua mikono kwenye mti ndio maana nimechubuka hivi. Hatimaye kitambaa cha machoni kikalegea nikapata nafasi ya kuangalia alipofungia, nilihangaika hadi nikaweza kufungua,” anasema. Anasema kuwa baada ya kujifungua kwenye mti alikwenda nyumbani na kumkuta mama yake akiwa na wasiwasi kwa kuwa alioongozana nao walirudi na hawakueleza walipomwacha. Anasema kuwa alimsimulia mama yake kilichotokea naye aliamua kumpeleka kwa Mwenyekiti wa Kitongoji. Anaongeza kuwa njiani walikutana na mama wa mtuhumiwa na baada ya kumweleza alichofanya motto wake, alisema kuwa kijana wake ana matatizo mengi, hivyo hawezi kushangaa kusikia hilo. "Kama aliweza kumbaka shangazi yake, kisha akamfunga na kamba na kumwacha porini, sishangai kama amemtendea mdogo wake, maana anatisha kwa matendo yake,”alisema mama wa kijana huyo. Julai 23,walifika Kituo Kidogo cha Polisi Kenyana na kupewa fomu ya matibabu (PF 3) ambapo polisi walidai wapewe Sh30,000 za mafuta ili wakamtafute mtuhumiwa. “Walisema wanataka hizo fedha wanunue petroli na waende watatu kwa pikipiki, mama alisema kuwa hana, basi ikawa ndiyo tumekosa ushirikiano zaidi ya kwenda zahanati ya Kenyana kupata matibabu, kisha tukarudi nyumbani,"anaeleza binti huyo. Kwa mujibu wa binti huyo, Julai 29 mjomba wake, Chacha Makindi mkazi wa Kemugesi alimchukua hadi Kituo cha Polisi Mugumu ambapo walifungua jalada na kupewa barua ya kwenda kwa Mtendaji wa Kijiji ili mtuhumiwa akamatwe. Hata hivyo mtuhumiwa huyo hajakamatwa kwa kile kinachodaiwa kuwa baba yake amemficha. Binti huyo anadai kuwa hajui kusoma wala kuandika licha ya kuwa alisoma hadi darasa la tano na kuacha kutokana na matatizo ya kifamilia ambapo wenzake sasa wako kidato cha kwanza. "Kwetu hakuna hata mtoto aliyefika sekondari, yaani watoto wote 29 na baba hajali kabisa hata kununua sare. Ndiyo maana niliacha masomo na sasa sipendi kurudi kijijini nitakaa hapa kwa ndugu yangu...maana hali huko si nzuri,"anadai binti huyo. Wanaharakati Julai 30 akiwa na mjomba wake walifika ofisi ya Wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu, ili kupata msaada wa kisheria hali iliyomfanya baba yake mzazi ajisalimishe baada ya kuandikiwa barua na kuanza kumhudumia kwa ajili ya matibabu . Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirika la Wasaidizi wa Sheria na Haki za Binadamu wilayani Serengeti, Monica Daniel anasema kuwa baada ya kuona mchezo uliopo wa baba yake, waliamua kuingilia kati na wanasimamia matibabu yake . "Baba yake anataka mambo yaishe, anamlaumu sana mke wake kwa madai kuwa alishamwacha, hivyo kwa tatizo hili hataki kutoa msamaha kwa mtoto wa mke mwenzake. Sisi tulibaini kuwa huyu mzazi alipoachana na mke wake mdogo hata watoto pia hawapi huduma,"anasema Monica. Kuhusu vipimo alivyofanyiwa binti huyo Monica alisema: "Katika vipimo amekutwa na maambukizi katika njia ya mkojo(UTI) na macho pia yalikuwa yameumizwa, ambapo baba yake ametoa Sh00,000 za matibabu.” Anaongeza kuwa wanajiandaa kwenda kumpima binti huyo kama amepata maambukizi ya Vurusi vya Ukimwi. Hata hivyo, alisema kuwa baba wa binti huyo anaomba shirika lao lisaidie kumshauri mama ya binti huyo ili wayamalize nyumbani na kuendelea na matibabu ya kienyeji akiamini kuwa kijana wake aliyetenda unyama huo anasumbuliwa na majini. “Sisi tumempa msimamo kuwa haki lazima itendeke, kama ni mgonjwa anatakiwa akapimwe akili ikithibitika watamwachia. Kwa nini anamficha kama ni mwehu? Hilo tumelikataa kwa kuwa hata aliyejeruhiwa anataka afikishwe mahakamani,"anabainisha Daniel. Monica aliomba hatua kali zichukuliwe kwa mtuhumiwa wa tukio hilo kwa kuwa kitendo alichofanya ni cha kikatili na hakifai kunyamaziwa. Alidai kuwa hata mzazi wake anatakiwa kuhojiwa na polisi sababu za kutetea unyama aliofanya kijana wake kwa kuwa ni kinyume kabisa cha sheria ya Mtoto ya mwaka 2009. Polisi Polisi wanadai kuwa wanaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo na kuwa maagizo yalishatolewa kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kemugesi kuhakikisha kuwa wanamnasa au kutoa taarifa ili akamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria . |
mmoja wa watafiti kutoka chuo kikuu cha Waseda cha Japan wanaoshirikiana na shiika la sederec wilayani serengeti akiwa amepanda kwenye moja ya maghala wanayotunzia chakula wakazi wa kijiji cha rwamchanga ambayo kwa sasa si salama kwa kuwa tembo huvamia makazi na kuangusha na kula chakula chote ambacho hukitegemea kwa kuuza pia,sasa wanakabiliwa na lindi la umaskini kwa kwa kuwa serikali haiwalipi fidia
watafiti kutoka japani wanaoshirikiana na shirika la SEDEREC wakiwa na wakazi wa kijiji cha Rwamchanga wilayani Serengeti wakiangalia maghala wanayotunzia mahindi nyumbani,hata hivyo makundi ya tembo baada ya kumaliza mazao mashambani yanavamia maghala nyumbani na kula akiba ya mahindi wanayotunza kwa biashara na chakula
kanisa laweka ratiba kuombea taifa
KANISA
LAWEKA RATIBA KUOMBEA AMANI YA NCHI.
Na
Anthony Mayunga-Serengeti
Agosti
19,2012.
KUTOKANA
na taifa kukabiliwa na matatizo mengi ambayo yanachangiwa na ukosefu wa maadili
kwa baadhi ya watumishi na kupelekea malalamiko kila kona ,kanisa la Mennote la
Kiinjili Tanzania wilayani Serengeti limepenga ratiba ya maombi kwa ajili ya
taifa.
Hivi
karibuni madhehebu ya dini yamejitokeza kuombea taifa kutokana na kuibuka
migomo,maandamano kila kona,migogoro ya kisiasa,lengo likiwa ni kuhakikisha
taifa linapata amani na utulivu.
Shemasi
wa kanisa hilo Wilson Itumbi katika mahubiri yake alisema maombezi hayo
yatakuwa yakifanyika kila siku ya jumatano jioni hapo kanisa ili kuhakikisha
amani,upendo na mshikamano unaimarika kwa kuwa nchi inakwenda vibaya.
“Amani
inaonekana kutoweka na hali ikiendelea hivi nchi itakuwa kwenye vita kali
chanzo ni kutoelewana kwa vyama vya siasa na kupelekea migogoro kwa viongozi
walioko madarakani kutopendana wao kwa wao na kuwajengea mazingira magumu
wananchi kujiletea maendelo”alisema.
Alisema
kuwa licha ya Tanzania kusifika kuwa nchi ya amani na kusifika katika maeneo
mbalimbali ya nje ya nchi,lakini kwa hali ilivyo sasa sifa hiyo imeanza
kutoweka.
Aliwataka
viongozi wa dini na washirika wa madhehebu mbalimbali kusimama imara katika kusimama
imara kuliombea taifa na viongozi wote kuanzia rais ,wabunge na madiwani waweze kuliongoza taifa vema kwa
kutanguliza maslahi ya taifa wala si vyama vyao.
Mwisho.
Subscribe to:
Posts (Atom)






