Subscribe:

Ads 468x60px

kanisa laweka ratiba kuombea taifa


KANISA LAWEKA RATIBA KUOMBEA AMANI YA NCHI.
Na Anthony Mayunga-Serengeti
Agosti 19,2012.

KUTOKANA na taifa kukabiliwa na matatizo mengi ambayo yanachangiwa na ukosefu wa maadili kwa baadhi ya watumishi na kupelekea malalamiko kila kona ,kanisa la Mennote la Kiinjili Tanzania wilayani Serengeti limepenga ratiba ya maombi kwa ajili ya taifa.

Hivi karibuni madhehebu ya dini yamejitokeza kuombea taifa kutokana na kuibuka migomo,maandamano kila kona,migogoro ya kisiasa,lengo likiwa ni kuhakikisha taifa linapata amani na utulivu.

Shemasi wa kanisa hilo Wilson Itumbi katika mahubiri yake alisema maombezi hayo yatakuwa yakifanyika kila siku ya jumatano jioni hapo kanisa ili kuhakikisha amani,upendo na mshikamano unaimarika kwa kuwa nchi inakwenda vibaya.

“Amani inaonekana kutoweka na hali ikiendelea hivi nchi itakuwa kwenye vita kali chanzo ni kutoelewana kwa vyama vya siasa na kupelekea migogoro kwa viongozi walioko madarakani kutopendana wao kwa wao na kuwajengea mazingira magumu wananchi kujiletea maendelo”alisema.

Alisema kuwa licha ya Tanzania kusifika kuwa nchi ya amani na kusifika katika maeneo mbalimbali ya nje ya nchi,lakini kwa hali ilivyo sasa sifa hiyo imeanza kutoweka.

Aliwataka viongozi wa dini na washirika wa madhehebu mbalimbali kusimama imara katika kusimama imara kuliombea taifa na viongozi wote kuanzia rais ,wabunge na  madiwani waweze kuliongoza taifa vema kwa kutanguliza maslahi ya taifa wala si vyama vyao.


Mwisho.

0 comments:

Post a Comment