VIONGOZI WA CWT WASHIKILIWA NA POLISI
Na Anthony Mayunga-Mara
Agosti 1,2012.
MGOMO wa walimu kwa Mkoa wa Mara sasa umechukua sura mpya kwa wilaya ya Tarime viongozi wa chama cha walimu wamekamatwa na polisi kwa madai kuwa wanachochea mgomo.huku wanafunzi wengi wakiamua kutokwenda shuleni kwa kuwa hawafundishwi.
Hali hiyo inajitokeza ikiwa ni siku ya tatu toka Mgomo mkubwa wa kitaifa umetangazwa na uongozi wa CWT wakitaka waongezewe misharaha asilimia mia na malimbikizo ya madeni.
Akiongea na Mwananchi kwa njia ya simu Mwenyekiti wa CWT wilaya ya Tarime Matinde Magabe alisema kuwa yeye na katibu wake John Magoko walikamatwa na polisi wakati wakiwa wamefuatilia Mwalimu wa shule ya msingi Rebu Esther Magesa aliyekamatwa julai 30,2012 kuhusiana na mgomo.
"Tukiwa polisi tumefuatilia dhamana ya Mwalimu Esther ,ocd akampigia ofisa elimu simu kuwa tupo,nikiwa nakunywa chai walifika askari wawili mmoja kavaa kiraia mwingine sare za polisi wanadai wananitaka mimi nachochea mgomo,kulitokea vurugu kidogo maana wananchi walichachamaa"alisema
Na kuwa walimfikisha kituo cha polisi kwa mahojiano,"niliona wanampango wa kunionea nikatoka kama napiga simu nikapanda bodaboda na kutoka kasi ,wakaamua kwenda kumkamata katibu wangu John Magoko na kumkwida"alisema Magabe.
Alisema hata yeye anatafutwa ili akamatwe ,kwa madai kuwa wamekuwa chanzo kikuu cha mgomo kusambaa wilaya nzima,huku akidai uamzi huo wa Mwajiri kutumia polisi ni kwenda kinyume na sheria kwa kuwa taratibu za mgomo zimefuata sheria vinginevyo wangekamatwa viongozi wa kitaifa wa chama.
Rpc akana.
Kamanda wa mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya Justus Kamugisha alipoulizwa alikana kuwepo kwa tukio hilo na kudai kuwa wao wanamshikilia mwalimu Esther kwa tuhuma za kuchochea wanafunzi wa shule ya Msingi Rebu kuandamana na kuwa yuko nje kwa dhamana na uchunguzi unaendelea.
Katibu adai alikamatwa.
Wakati Kamanda anakanusha kutokuwepo tujkio hilo Katibu wa CWT wilaya Tarime Magoko alilithibitishia Mwananchi kwa njia ya simu kuwa alikamatwa akituhumiwa kumtorosha Mwenyekiti wa wilaya walipokuwa polisi.
"Ndio kwanza naachiwa nimehojiwa hapo kituoni wakidai mimi niwaambie Mwenyekiti alipo ,maana wanadai nimemsadia kutoroka,nimekataa nimejieleza na nilikuwa na katibuwa CWT mkoa mwisho wameniachia"alisema.
Katibu Cwt Mkoa akiri kukamatwa kwa katibu wake.
Katibu wa CWT mkoa wa Mara Fatuma Bakari alilithibitishia Mwananchi kukamatwa kwa katibu huyo kisha kuachiwa,"niko hapa Tarime ni kweli amekamatwa na kuhoojiwa lakini ameachiwa ndio tunaendelea kufuatilia kwa undani zaidi"alisema.
Wakati serikali ikitumia njia hiyo kama vitisho wanafunzi katika shule nyingi za msingi na sekondari wilayani Serengeti na Tarime wameamua kutokwenda shuleni kwa kile wanachodai wanakwenda kucheza kwa kuwa hawafundishwi.
Kwa wilaya ya Serengeti imerbainika kuwa wazazi wengi waliamua kuwatumia watoto wao kwa shughuli mbalimbali za kuuza vitu vido vidogo mnadani ambao hufanyika kila tareme moja ya mwezi.
Uamzi huo pia unadaiwa kuungwa mkono na baadhi ya wazazi kwa madai kuwa wasubiri uamzi wa madai yaliyoko Mahakamani kama mgomo utasitishwa ama la,huku wakiwatuhumu baadhi ya viongozi wa serikali kuwa hawana uchungu na madhara ya mgomo huo kwa kuwa watoto wao hawasomi katika shule za serikali.
mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment