AFISA KILIMO,WAZABUNI WA PEMBEJEO WAPANDISHWA KIZIMBANI
WAKIKABILIWA NA MAKOSA 50.
Aprili 11,2013
SERENGETI .
AFISA kilimo na Mifugo wilaya ya Serengeti ,wazabuni wa pembejeo , watendaji wa vijiji,na wakulima wamefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara,wakikabiliwa na makosa 50 ya wizi wa fedha za Pembejeo zenye tahamani ya tsh,4,935,000=
Mwendesha mashitaka Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Abdallah Idd amewataja Waliofikishwa mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama hiyo, Amon Kahimba, kuwa ni Andrew Manyerere (55) Afisa kilimo/Mifugo wilaya, Nyitamboka Kitang’ita (61)wa kijiji cha Majimoto, Karebu Ruji(41), Paulo Nyandito (50) wote wafanyabiashara wa pembejeo.
Wengine ni Joseph Petro (38) Afisa Mtendaji kijiji cha Rwamchanga, Damiani Nyamaheda (34) hakuwepo Mahakamani baada ya kutoroka, Emmanuel Mkamba (29) mkulima mkazi wa kijiji cha Itununu na Pili Nyakimori (35) mkulima.
Mwendesha mashitaka aliambia Mahakama iliyokuwa imefurika watu kuwa mwaka 2012 kwa nyakati tofauti katika vijiji vyao wanavyofanyia kazi mshitakiwa wa pili hadi wa nane wanatuhumiwa kula njama, kugushi sahihi za watu na kuchukua fedha za pembejo na kufanya tendo la
wizi.

Alisema mshitakiwa wa kwanza katika shauri hilo Andrew
Manyerere ambaye ni Afisa kilimo na mifugo wilaya ya Serengeti anashitakiwa kwa
kosa la uzembe baada ya kushindwa kuchukua hatua za kudhibiti wizi huo mapema.
Alisema washitakiwa saba, wakiwemo wafanyabiashara, wakulima na watumishi wa ummawaliopewa dhamana ya kusambaza na kusimamia pembejeo kwa wakulima walikula njama na kugushi nyaraka, sahihi ambapo walijipatia fedha kati ya shilingi 100,000/= hadi 150,000/=,hata hivyo alisema viwango vya fedha na makosa yao yanatofautiana.

Akifafanua mashitaka hayo mwendesha mashitaka huyo aliiambia
mahakama kuwa yanaangukia kwenye wizi kwa kuwa washitakiwa walikula njama za
kuiba nakisha kuiba.
Kuhusu mshitakiwa wa sita Damian Nyamaheda ambaye ni mfanyabiashara hakufikishwa Mahakamani kwa vile hajakamatwa ,alisema jeshi la polisi linaendelea
kumsaka.
Washitakiwa wote walikana kuhusika na mashitaka yanayowakabili ya kula njama na kugushi nyaraka za pembejeo kujipatia fedha kinyume cha sheria walikana,na wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika hadi aprili 23 mwaka huu itakapotajwa tena.

Mwisho.
0 comments:
Post a Comment