Subscribe:

Ads 468x60px

WAANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI ZA BIASHARA WAENDELEA NA MASOMO AWAMU YA TATU

 Mkufunzi chuo kikuu mtakatifu Augustino Saut Mwanza -Mass Communication Kopoka Mlagiri akitoa mada kwa waandishi  wa habari za uchunguzi za biashara chini ya ufadhili wa Best Ac,Ansaf na Saut
 Mkufunzi wa Mass Communication chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino Saut Denis Mpagaze akitoa mada ya maadili(ethics)kwa waandishi wa habari za uchunguzi za biashara
 Kaimu makamu mkuu wa chuo cha mtakatifu Augustino Saut-Padri Thadeus Mukamwa akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani

Baadhi ya waandishi wakisikiliza mkufunzi

WAANDISHI wa habari nchini wamesisitizwa kusoma zaidi ili kuboresha taaluma zao kwa lengo la kuisaidia nchi kutokana na matatizo yanayoikabili.
Makamu mkuu wa chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino(SAUT)Dk,Padri Thadeus Mukamwa amewaambia waandishi wa habari 16 wanaosoma kozi za uandishi wa habari za uchunguzi  biashara katika chuo kikuu hicho.
Amesema waandishi ni chachu ya mabadiliko hivyo wanapaswa kujiongezea maarifa ,”tumieni maarifa hayo kwa maslahi ya umma wala si kwa maslahi yenu….angalieni maslahi ya umma kwanza”alisema.
Alitoa mfano wa nchi ya Marekani kuwa wagombea wake walitanguliza zaidi nchi kuliko nafasi zao.
“Uhuru wa waandishi katika nchi zingine unalindwa sana …ingawa kwetu hapa kuna matatizo mengi yanayowasibu…lakini jikiteni zaidi kuandika ukweli kwa kuibua changamoto zinazokabili jamii”alisema Rukamwa.
Mmoja wa wakufunzi wa kozi hiyo iliyoanza julai 2012 chini ya ufadhili wa Best –Ac,Ansaf na Saut aliwataka waandishi kuwa na malengo ili kuboresha taaluma yao.
“Someni,fanyeni utafiti ili msiwe waandishi wa kupelekwa na wimbi la wanasiasa …chambueni issue ili muweze kuleta mabadiliko kwa kuibua mambo ambayo yanatasaidia kukuza uchumi wa nchi na kufichua mambo yanayosumbua kama mikataba “alisema.
Mwisho.


0 comments:

Post a Comment