MTENDAJI,MKANDARASI
WADAIWA KUGUSHI NA KUIBA SH.MIL.I0
Apili 25,2013.
Serengeti.
OFISA Mtendaji kijiji cha Monuna kata ya Nyambureti Wilaya ya Serengeti Mkoani
Mara Juma Ntora kwa kushirikiana na Kampuni ya J.N.L. Construction and General
Traders Ltd ya Musoma wanadaiwa kughushi
nyaraka na kuiba sh.mil.10 za ujenzi wanyumba ya waganga Zahanati ya kijiji hicho.
Mradi huo ulipata sh.34,895.295.00 kupitia Mpango wa MMAM na
ziliwekwa benki ya NMB Tawi la Mugumu julai 31,2012 kwenye akaunti ya mradi wa
zahanati namba 3026600268,waeka sahihi wakiwa ni wajumbe wawili na ofisa
mtendaji huyo.
Wizi huo imebainika ulifanyika septemba 21,2012 ambapo
badala ya kuchukua sh.7,890,000=zilizopitishwa na kamati ya ujenzi wa nyumba ya
mganga Monuna ,na kuridhiwa na aliyekuwa
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Kimulika Galikunga kwa sasa
yuko Mpanda,lakini wakaongeza namba moja
mbele na kusomeka 17,890,000.
Blogu ilibaini muhtasari wa kamati uliandaliwa na ofisa
mtendaji huyo agosti 20,2012 badala ya kamati ya ujenzi ,lakini uliwekwa sahihi
na Juma Kongo(Mwenyekiti)Mussa Nyandete(Katibu)Meshack O.Janes(Mjumbe)Christina
Maro(mjumbe) na John Apiyo Agar(mjumbe).
Muhtasari huo ulioambatanishwa na barua yenye
kumb.NoK/U/K/M./VOL10/012 unaonyesha kiwango kilichotakiwa kuchukuliwa ni
7,890,000= baada ya mhandisi wa
halmashauri hiyo Mokoro Magori ,Katibu wa afya Peter Shilingi kwa niaba ya Mganga mkuu wa wilaya na aliyekuwa
Mkurugenzi mtendaji Galikunga kupitisha hati ya ukaguzi hatua ya kwanza.
Hati hiyo Kandarasi namba LGA/063/2008-2009/8/MMAM/09
inaonyesha mkandarasi JNL.Construction and General Traders Ltd, ilisainiwa
tarehe kati ya 13-17/9/2012,inatofautiana na mhitasari na barua ya kuchukua
fedha ambao uliandaliwa tarehe 20,8,2012.
Malipo hayo yakiwa ni kwa ajili ya shughuli za awali za msingi,kumwaga
zege la jamvi ya nyumba hiyo ya watumishi wawili wa afya.
Uchunguzi wa blogu hii ulibaini kuwa wizi huo ulifanikiwa
kirahisi baada ya kuongeza tarakimu moja mbele baada ya kuwa mtendaji huyo
ameacha nafasi wazi,pia kwa kutumia jina
la Solomon Eliud Nkaina toka kwenye muhtasari badala ya jina la Kampuni hali
ambayo inaashiria kuwa wanakwepa mapato ya serikali kwa kutokutumia jina la
kampuni.
Mweka sahihi.
Mjumbe na mweka sahihi kamati ya ujenzi wa nyumba hiyo
Meshack Janes alisema wizi huo aliubani wakati alipokwenda Benki ya NMB tawi la
Mugumu kuangalia salio na kubaini kati ya fedha walizoidhinisha milioni 10
ziliibwa.
“Nilipitia hapo NMB benki baada ya kutoka benki ya CRDB
kupokea malipo yangu ya tumbaku…kwa kuwa mimi ni mweka sahihi nikaona ni vema
kuchukua salio kwa kuwa tulishakubaliana tukifika mjini tupate muda wa kuhakiki
na kutoa taarifa kwenye kamati”alisema.
Kuhusu wizi huo alisema ulianzia kwenye muhtasari aliouandaa
na baada ya kuambiwa urekebishwe alitumia sahihi za wajumbe za awali na kisha
kuandaa muhtasari mwingine bila kuwashirikisha na kwenda kuchota fedha hizo.
Mtendaji.
Alipotafutwa kwa njia ya Simu Ofisa mtendaji Juma Ntora
alikiri kuwepo kwa tatizo na kuwa tayari anahojiwa”ninahojiwa an PCCB kwa sasa kuhusiana na suala hilo”alisema .
Alikiri kushirikiana na mwakilishi wa kampuni kupora fedha
hizo,”hata hivyo jamaaa amekimbia na kuniachia mzigo,nimekubali kulipa hizo
mil.10 zote ili mambo yaishe,maana hata pesa hizo sikufanikiwa kupata mgao.
Kampuni.
Mkurugenzi wa kampuni ya ya JNL Construction and General
Traders Ltd Lameck Chacha alikiri
mfanyakazi wake kuhusika na wizi huo,”niliambiwa nikafuatilia ni kweli
alishirikiana na mtendaji akamwandikia kwa jina lake badala ya kampuni ,ni wizi
huo na alitoroka sijui alipo”alisema.
Hata hivyo alikiri kuwa hakuna sehemu aliyotoa taarifa
kuhusu mfanyakazi wake kuiba na kutoroka,kwa madai kuwa yeye anajua fedha
walizokubaliana na kijiji zipo na akimaliza kazi atalipwa kama
walivyokubaliana.
Serikali ya kijiji.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Damas Kongo Watanda
alisema ,suala hilo wanategemea vyombo husika kuchukua hatua kwa kuwa wizi huo
unaathari kubwa kwa jamii,”akina mama wanatembea zaidi ya kilometa 10 kupata
huduma”alisema.
Ofisi ya Ded/Dc.
Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji na Mkuu wa wilaya imetaarifiwa
na kuwa suala hilo limeishaelekezwa PCCB kwa ajili ya uchunguzi na kuchukua
hatua kwa wahusika.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment