wakati tarehe ya kuanza ukeketaji wilayani serengeti ikitajwa kuwa ni desemba 15 mwaka huu siku moja tu baada ya shule za msingi kufungwa wanaharakati wanaendelea na kampeini zao za kupinga vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia,picha kwa hisani ya Mayunga.blogsspot.com
UKEKETAJI KUANZA DESEMBA 15 BAADHI YA MAENEO.
Na
Anthony Mayunga-Serengeti
Novemba
28,2012.
WAKATI
wanaharakati wanazindua siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia
,wazee wa baadhi wa mila baadhi ya maeneo wilaya ya Serengeti wamepanga kuanza ukeketaji
na tohara kwa vijana wa kiume kuanza desemba 15 mwaka huu.
Uamzi
wa wazee wa mila kwa baadhi ya maeneo ambao unafanywa kisiri siri imebainika
kuwa itakuwa ni siku moja baada ya kufungwa kwa shule za msingi desemba
14,2012.
Habari
za uhakika ambazo zimethibitishwa na baadhi ya wazee wa mila zinadai kuwa muda
huo umepangwa ukizingatia tarehe ambazo ngariba wa vijana wa kiume atakuwa
amemaliza kazi nchini Kenya.
“Ngariba
wa kiume anatokea nchini Kenya ambako kwa sasa wanaendelea na kazi ya
kutahili…kuanzia tarehe hizo atakuwa amemaliza na ndiyo maana wamepanga tarehe
hizo…”alisema mmoja wa wazee wa mila
jina limehifadhiwa.
Aliliambia
Mwananchi kuwa ngariba wa kike wapo vijijini lakini kwa mila na desturi watoto wa kike hawawatangulii vijana wa
kiume,hivyo kazi hiyo itafanyika kwa wakati mmoja hasa maeneo ya kata ya
Kebancha bancha.
Akizungumzia
tishio la serikali la kuwakamata watakaohusika na kukeketa watoto wa kike ,alisema kuwa kuacha itakuwa
kazi ngumu kwa kuwa mila na desturi itakuwa imepotea.
“Ili
kutopoteza mila wanakata kidogo sana ili damu ionekane imevuja,kuacha kabisa ni
vigumu haya mambo yatakwenda taratibu yaishe yenyewe kama ilivyokuwa kwa kutoga
masikio”alibainisha.
Hata
hivyo baadhi ya maeneo wazee wa mila
wakiulizwa msimamo wao kuhusu kuacha ukeketaji wamekuwa wakisukumia wanawake
kuwa ndio wanashawishi watoto wa kike ,huku akina mama wakisema wenye sauti ni
wazee wa mila kwa kuwa ndio wanaoheshimiwa na jamii.
“Kuna
kusukumiana kwa wazee wa mila na akina mama … wazee wa mila wanasema akina mama
wanachangia kuendelea kwa ukeketaji kwa kuwa huwadanganya watoto kuwa wanaenda
kusalimia bibi zao …huko hukeketwa kwa aibu yao kwa jamii ni kubwa kuliko
wanaume,”alisema.
Kwa
mjibu wa tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa wanawake wananyanyapaliana sana
kama kuliko wanaume hasa mabinti zao
wanapokuwa hawajakeketwa,hali ambayo pia huwaathiri watoto wa kike kutengwa na
wenzao na wengine hutoroka kwenda kukeketwa.
Baadhi
ya mashirika yanayotoa elimu ya kupinga
vitendo vya ukeketaji kwa wilaya za
Serengeti na Tarime hasa Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT)wamesema kuwa wana
uhakika wa kupokea watoto wengi watakao kimbia kukeketwa.
Mwisho.
BABA ABAKA MWANAE WA MIAKA 2.5 NA
KUMUUMIZA VIBAYA.
Na Anthony Mayunga-Serengeti
Novemba 28,2012.
WAKATI wanaharakati wakipaza
sauti za siku 16 za kupinga ukatili ,mkazi mmoja wa mtaa wa Sedeko kata ya
Stendi kuu wilayani Serengeti John Nashon(25)amembaka mwanae wa miaka 2.5 na
kumuumiza vibaya kisha akatoroka.
Tukio hilo ambalo limepokelewa
kwa hisia tofauti na wakazi wa mji wa Mugumu linadaiwa kutokea novemba
26,majira ya saa 12.00 jioni mwaka huu katika mtaa huo na kuripotiwa kituo cha
polisi Mugumu mjini.
Mama mzazi wa mtoto huyo akiongea
na Mwananchi akiwa hospitali teule ya Nyerere ddh alikolazwa kitanda namba 8
wodi ya watoto ,alisema wakati unyama huo unatendeka alikuwa sokoni.
“Nilimwacha mwanangu na baba yake
ambaye ni fundi wa magari gereji ya Mayala mjini hapa,kurudi kufika mlangoni
mme wangu akanieleza niingie ndani haraka nimkande mtoto mwili mzima kwa maji
baridi…nilikuwa sijui kinachoendelea”alisema na kuendelea
“Kuingia chumba cha kulala
nikamkuta mtoto amelala kitandani,kumnyanyua damu zikamwagika mithili ya maji
kutoka sehemu yake ya siri…kumwangalia nikakuta amechanika sehemu zake za
siri”alisema.
Hali hiyo ilimpelekea kumwangukia
mwanae na kuanza kulia kwa uchungu na alipotaka maelezo kwa mme wake alisema
alimsukuma kwa bahati mbaya mwanae akaanguka kwenye kochi na kuchomwa na
msumari sehemu zake za siri.
“Nilipomwambia tumpeleke
hospitali akakataa tena akinitishia kunipiga kwa madai kuwa siri
itafichuka…niligundua kumbe ndiye kafanya unyama huo,nilitoka kwa nguvu hadi
kituo cha polisi na kupewa pf 3,nikimwacha hapo,lakini alikimbia na haijulikani
alipo”alisema.
Hata hivyo alipomuuliza mwanae
kilichomtokea akasema kuwa baba yake ndiye aliyemfanyia unyama,huku akishangaa
kwa kitendo hicho kwenye ndoa yao iliyodumu kwa mwaka mmoja toka novemba 2011.
Mganga mkuu wa hospitali hiyo
Dk.Kelvin Mwasha amekiri kumpokea mtoto huyo na kuwa amelazwa wodi la watoto
,kutokana na maumivu na kuvuja damu nyingi ililazimu kuongezewa damu.
“Sehemu zake za siri zilikutwa
zimeharibiwa sana ,amepata huduma ikiwa ni pamoja na kuchukua sampuli za maji
yaliyokuwa yanatoka ukeni kwa ajili ya vipimo …amekutwa yuko salama,lakini hili
tukio si la kawaida linatakiwa kulaaniwa ,na ndiyo yanaifanya wilaya kuonekana
na matukio ya ukatili”alisema.
Hivi karibuni katika uzinduzi wa
siku 16 zakupinga ukatili kamanda wa polisi mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma
alisema kunaongezeko kubwa la matukio ya ukatili,ambapo kwa mwaka huu toka
januari yameripotiwa matukio 201 ikiwa ni tofauti na mwaka 2011 matukio 148
yaliriripotiwa polisi.
Mwisho.