Subscribe:

Ads 468x60px

KILA JAMBO NA WAKATI WAKE,MANENO YA MHUBIRI,KAZI NA DAWA

MHUBIRI AMEANDIKA KATIKA BIBLIA KUWA KILA JAMBO NA WAKATI WAKE,HAPA BAADA YA KAZI YA KUGAWA MSAADA WAFANYAKAZI WA SERENGETI SERENA HOTELI WANAWEKA VEMA AFYA ZAO ,

KAZI NA DAWA,MEETING POINT MJINI MUGUMU SERENGETI

HOTELI YA SERENGETI SERENA YATOA MSAADA WA VYAKULA NGUO,BIBLIA NA VYANDARUA KWA WAZEE,WALEMAVU NA WATOTO WA MAZINGIRA MAGUMU KIJIJI CHA PARK NYIGOTI SERENGETI.

WAFANYAKAZI WA SERENGETI SERENA HOTELI ILIYOKO NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI WAKIWA WAMEKAA ,KABLA YA KUTOA MSAADA KWA WAZEE,WALEMAVU NA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU KATIKA KIJIJI CHA PARK NYIGOTI KATA YA IKOMA WILAYANI SERENGETI.

MAANDALIZI YANAENDELEA KAMA INAVYOONEKANA HAPO

BAADHI YA VITU WALIVYOGAWA.KWA MAKUNDI HAYO MSAADA HUO UNA ZAIDI YA THAMANI YA SH.LAKI NANE,NA KILA MWAKA HOTELI HIYO HUTOA MISAADA KWA JAMII INAYOWAZUNGUKA,WILAYA ZA MAGU,BARIADI,MAGU NA SERENGETI.

UGAWAJI WA MISAADA UNAENDELEA KWA MAKUNDI LENGWA.

WAMEGAWA,MCHELE,SUKARI,NGUO AINA MBALIMBALI,SEMBE,UNGA WA NGANO,VYANDARUA NA BIBLIA.

MMOJA WA WAZEE AKIPOKEA MSAADA.

MZEE MACGEGE KITARETA(102)NI MIONGONI MWA WALIOSAIDIWA.

MZEE HUYO AKISAIDIWA KUSIMAMA NA MWENYEKITI WA SERIKALI YA KIJIJI CHA PARK NYIGOTI.

BAADA YA KAZI WALIPATA NAFASI YA KUKATA KIU KAMA INAVYOONEKANA HAPO.

MTENDAJI,MKANDARASI WAGUSHI NA KUIBA SH.MIL.10 ZA UJENZI WA NYUMBA YA MGANGA MONUNA

MTENDAJI,MKANDARASI  WADAIWA KUGUSHI NA KUIBA SH.MIL.I0
Apili 25,2013.
Serengeti.
OFISA Mtendaji kijiji cha Monuna  kata ya Nyambureti Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara Juma Ntora kwa kushirikiana na Kampuni ya J.N.L. Construction and General Traders Ltd ya Musoma  wanadaiwa kughushi nyaraka na kuiba sh.mil.10 za ujenzi wanyumba ya waganga  Zahanati ya kijiji  hicho.
Mradi huo ulipata sh.34,895.295.00 kupitia Mpango wa MMAM na ziliwekwa benki ya NMB Tawi la Mugumu julai 31,2012 kwenye akaunti ya mradi wa zahanati namba 3026600268,waeka sahihi wakiwa ni wajumbe wawili na ofisa mtendaji huyo.
Wizi huo imebainika ulifanyika septemba 21,2012 ambapo badala ya kuchukua sh.7,890,000=zilizopitishwa na kamati ya ujenzi wa nyumba ya mganga Monuna ,na kuridhiwa na  aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Kimulika Galikunga kwa sasa yuko Mpanda,lakini wakaongeza namba  moja mbele na kusomeka 17,890,000.
Blogu ilibaini muhtasari wa kamati uliandaliwa na ofisa mtendaji huyo agosti 20,2012 badala ya kamati ya ujenzi ,lakini uliwekwa sahihi na Juma Kongo(Mwenyekiti)Mussa Nyandete(Katibu)Meshack O.Janes(Mjumbe)Christina Maro(mjumbe) na John Apiyo Agar(mjumbe).
Muhtasari huo ulioambatanishwa na barua yenye kumb.NoK/U/K/M./VOL10/012 unaonyesha kiwango kilichotakiwa kuchukuliwa ni 7,890,000= baada ya  mhandisi wa halmashauri hiyo Mokoro Magori ,Katibu wa afya Peter Shilingi  kwa niaba ya Mganga mkuu wa wilaya na aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji Galikunga kupitisha  hati ya ukaguzi hatua ya kwanza.
Hati hiyo Kandarasi namba LGA/063/2008-2009/8/MMAM/09 inaonyesha mkandarasi JNL.Construction and General Traders Ltd, ilisainiwa tarehe kati ya 13-17/9/2012,inatofautiana na mhitasari na barua ya kuchukua fedha ambao uliandaliwa tarehe 20,8,2012.
Malipo hayo yakiwa ni kwa ajili ya shughuli za awali za msingi,kumwaga zege la jamvi ya nyumba hiyo ya watumishi wawili wa afya.
Uchunguzi wa blogu hii ulibaini kuwa wizi huo ulifanikiwa kirahisi baada ya kuongeza tarakimu moja mbele baada ya kuwa mtendaji huyo ameacha nafasi wazi,pia kwa kutumia  jina la Solomon Eliud Nkaina toka kwenye muhtasari badala ya jina la Kampuni hali ambayo inaashiria kuwa wanakwepa mapato ya serikali kwa kutokutumia jina la kampuni.
Mweka sahihi.
Mjumbe na mweka sahihi kamati ya ujenzi wa nyumba hiyo Meshack Janes alisema wizi huo aliubani wakati alipokwenda Benki ya NMB tawi la Mugumu kuangalia salio na kubaini kati ya fedha walizoidhinisha milioni 10 ziliibwa.
“Nilipitia hapo NMB benki baada ya kutoka benki ya CRDB kupokea malipo yangu ya tumbaku…kwa kuwa mimi ni mweka sahihi nikaona ni vema kuchukua salio kwa kuwa tulishakubaliana tukifika mjini tupate muda wa kuhakiki na kutoa taarifa kwenye kamati”alisema.
Kuhusu wizi huo alisema ulianzia kwenye muhtasari aliouandaa na baada ya kuambiwa urekebishwe alitumia sahihi za wajumbe za awali na kisha kuandaa muhtasari mwingine bila kuwashirikisha na kwenda kuchota fedha hizo.
Mtendaji.
Alipotafutwa kwa njia ya Simu Ofisa mtendaji Juma Ntora alikiri kuwepo kwa tatizo na kuwa tayari anahojiwa”ninahojiwa an PCCB  kwa sasa kuhusiana na suala hilo”alisema .
Alikiri kushirikiana na mwakilishi wa kampuni kupora fedha hizo,”hata hivyo jamaaa amekimbia na kuniachia mzigo,nimekubali kulipa hizo mil.10 zote ili mambo yaishe,maana hata pesa hizo sikufanikiwa kupata mgao.
Kampuni.
Mkurugenzi wa kampuni ya ya JNL Construction and General Traders Ltd  Lameck Chacha alikiri mfanyakazi wake kuhusika na wizi huo,”niliambiwa nikafuatilia ni kweli alishirikiana na mtendaji akamwandikia kwa jina lake badala ya kampuni ,ni wizi huo na alitoroka sijui alipo”alisema.
Hata hivyo alikiri kuwa hakuna sehemu aliyotoa taarifa kuhusu mfanyakazi wake kuiba na kutoroka,kwa madai kuwa yeye anajua fedha walizokubaliana na kijiji zipo na akimaliza kazi atalipwa kama walivyokubaliana.
Serikali ya kijiji.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Damas Kongo Watanda alisema ,suala hilo wanategemea vyombo husika kuchukua hatua kwa kuwa wizi huo unaathari kubwa kwa jamii,”akina mama wanatembea zaidi ya kilometa 10 kupata huduma”alisema.
Ofisi ya Ded/Dc.
Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji na Mkuu wa wilaya imetaarifiwa na kuwa suala hilo limeishaelekezwa PCCB kwa ajili ya uchunguzi na kuchukua hatua kwa wahusika.
Mwisho.

NDUGU KUKAA KWA PAMOJA NA KWA UMOJA

NIKO NA MZEE WA ITIFAKI WA IBJ KAVU TULIFUATILIA HOTUBA YA MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA MT.AUGUSTINO(SAUT)PADRI DK,CHARLE KITIME KWENY UKUMBI WA LAVOIE CENTRE HAYUPO PICHANI WAKATI AKIFUNGA MAFUNZO YA WIKI 2 KWA WAANDISHI WA INVESTIGATIVE BUSINESS JOURNALISM KOZI ILIYOANZA JUNI 2012

 MKUU WA ITIFAKI IBJ DICKSON AKIFUATILIA KWA MAKINI
 WAANDISHI WAKIFUATILIA HOTUBA YA DK.KITIME
 DK.KITIME AKISISITIZA JAMBO KWA WAANDISHI AMBAO AMESEMA WANAYO NAFASI YA KUSAIDIA JAMII KUHUSIANA NA HALI NGUMU YA MAISHA KWA KUTAFITI NA KUFICHUA CHANZO,WAHUSIKA ILI HATUA ZIWEZE KUCHUKULIWA AMA KUWAJIBISHWA NA JAMII.
 TAZAMA ILIVYO VEMA NA  NDUGU KUKAA KWA PAMOJA NA KWA UMOJA ,HAPA WAANDISHI WA HABARI WAKIWA NA WAKUFUNZI WA CHUO KIKUU CHA MT,AUGUSTINO WAKIPATA CHAKULA
KAZI NA DAWA,AFYA ZINAJALIWA VILIVYO ILI WAWEZE KUPATA NGUVU ZA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO

ZIARA KIWANDA CHA NYANZA BOTTLE YAENDELEA

WATAALAM WA IDARA YA UTENGENEZAJI WA CHUPA ZA PLASTIKI KATIKA KIWANDA CHA NYANZA BOTTLE CO.LTD WAKITOA MAELEZO YA KITAALAM KWA WAANDISHI WA HABARI WALIOKO KWENYE MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI ZA BIASHARA CHUO KIKUU CHA MT.AUGUSTINO (SAUT)MWANZA MAFUNZO YALIYOANZA 2012 JUNI

ZIARA INAENDELEA HAPO KIWANDANI,ANAYEANGALIA NYUMA NI MKUU WA UTARATIBU WA WANA IBJ DICKSON NG'HILLY

ZIARA YA WAANDISHI WA HABARI TOKA SAUT KIWANDA CHA COCACOLA

TIMU YA INVESTIGATIVE BUSINESS JOURNALISM (IBJ)WALIOKO KWENYE MAFUNZO MAALUM CHUO KIKUU CHA MT.AUGUSTINO(SAUT)WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA  BAADHI YA MAAFISA WA KIWANDA CHA SODA CHA NYANZA BOTTLE CHA MWANZA WAKATI WALIPOFANYA ZIARA YA MAFUNZO KIWANDANI HAPO

MMOJA WA MAAFISA WA KIWANDA CHA NYANZA BOTTLE KINACHOTENGENEZASODA ZA COCACOLA KILICHOKO JIJINI MWANZA AKITOA UFAFANUZI KUHUSU SHUGHULI WAZIFANYAZO KWA WAANDISHI WA HABARI.

AFISA KILIMO,WAZABUNI WA PEMBEJEO WAPANDISHWA KIZIMBANI WAKIKABILIWA NA MAKOSA 50.

AFISA KILIMO,WAZABUNI WA PEMBEJEO WAPANDISHWA KIZIMBANI WAKIKABILIWA NA MAKOSA 50.
Aprili 11,2013
SERENGETI .

AFISA  kilimo na Mifugo wilaya ya Serengeti ,wazabuni wa pembejeo , watendaji wa vijiji,na wakulima wamefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara,wakikabiliwa na makosa 50 ya wizi wa fedha za Pembejeo zenye tahamani ya tsh,4,935,000=

Mwendesha mashitaka  Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Abdallah Idd amewataja Waliofikishwa mbele ya  Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama  hiyo, Amon Kahimba,  kuwa ni  Andrew Manyerere (55) Afisa kilimo/Mifugo wilaya, Nyitamboka Kitang’ita (61)wa kijiji cha  Majimoto, Karebu Ruji(41), Paulo Nyandito (50) wote wafanyabiashara wa pembejeo.

Wengine ni Joseph Petro (38) Afisa Mtendaji kijiji cha Rwamchanga, Damiani Nyamaheda (34) hakuwepo Mahakamani baada ya kutoroka, Emmanuel Mkamba (29)  mkulima mkazi wa kijiji cha Itununu na Pili Nyakimori (35) mkulima.

Mwendesha mashitaka aliambia Mahakama  iliyokuwa imefurika watu kuwa mwaka 2012 kwa nyakati tofauti katika vijiji vyao wanavyofanyia kazi mshitakiwa wa pili hadi wa nane wanatuhumiwa kula njama, kugushi sahihi za watu na kuchukua fedha za pembejo na kufanya tendo la
wizi.
Alisema mshitakiwa wa kwanza katika shauri hilo Andrew Manyerere ambaye ni Afisa kilimo na mifugo wilaya ya Serengeti anashitakiwa kwa kosa la uzembe baada ya kushindwa kuchukua hatua za kudhibiti wizi huo mapema.

Alisema washitakiwa saba, wakiwemo wafanyabiashara, wakulima na watumishi wa ummawaliopewa dhamana ya kusambaza  na kusimamia pembejeo kwa wakulima walikula njama na kugushi nyaraka, sahihi ambapo walijipatia fedha kati ya shilingi 100,000/= hadi 150,000/=,hata hivyo alisema viwango vya fedha na makosa yao yanatofautiana.
Akifafanua mashitaka hayo mwendesha mashitaka huyo aliiambia mahakama kuwa yanaangukia kwenye wizi kwa kuwa washitakiwa walikula njama za kuiba nakisha kuiba.

Kuhusu  mshitakiwa wa sita Damian Nyamaheda ambaye ni mfanyabiashara hakufikishwa Mahakamani kwa vile  hajakamatwa ,alisema  jeshi la polisi linaendelea
kumsaka.

Washitakiwa  wote walikana kuhusika na  mashitaka yanayowakabili ya kula njama na kugushi nyaraka  za pembejeo kujipatia fedha kinyume cha sheria walikana,na wako nje kwa dhamana  baada ya kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika hadi  aprili 23 mwaka huu  itakapotajwa tena.

PICHA ZA MATUKIO WAKATI NAKABIDHIWA TUZO

 HAPO NIKISUBIRI KUKABIDHIWA TUZO YA USHINDI WA UANDISHI MAHIRI HABARI ZA UTAWALA BORA 2012

 MKURUGENZI WA MFUKO WA VYOMBO VYA HABARI(TMF)ERNEST SUNGURA AKINIPONGEZA KABLA YA KUNIKABIDHI TUZO NA ZAWADI YA USHINDI.

HAPO NAKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI KABLA YA TUZO NA ZAWADI ZINGINE

HAPO NINAKABIDHIWA TUZO NA IPAD,HUKU AKINIHIMIZA KUHAKIKISHA MWAKA KESHO MUNGU AKIJALIA NIIBUKE NA NAFASI YA MSHINDI WA JUMLA.

PONGEZI ZILICHUKUA NAFASI KUBWA KUTOKA KWA SUNGURA ,HUKU NAMI NIKIKIRI KUWA FEDHA ZA MFUKO WA VYOMBO VYA HABARI ZIMECHANGIA MIMI KUFIKA HAPO.

picha za matukio ya Ejat

 Makamu wa kwanza wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad akiongozana na waziri wa habari michezo na Utamaduni Dk,Fenela Mkangara kuingia ukumbini Diomond Jubilee kwa ajili ya kutoa tuzo kwa waandishi mahiri 2012
 Brass band ya Jkt Mgulani ikitoa burudani
 Maalim Seif,Waziri Mkangara,Jaji Robert Kisanga Rais wa MCT,kAJUBI Mkajanga
 hapa ni muda wa chakula
afya zilijaliwa vema

TUZO ZA UMAHIRI WA UANDISHI WA HABARI 2012

 Burudani kutoka JKT zilikuwepo
waziri wa michezo habari na utamaduni Dk,Fenella Mkangara akitoa tuzo kwa mmoja wa waandishi

Matukio ya Ejat 2012

 Dickson Ng'hilly ,Ashton Balaigwa na wenzake wakiwa wakijadiliana kabla ya hitimisho la Ejat 2012
 Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisoma hotuba kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dk.Mohammed Shein wakati wa kukabidhi tuzo za uandishi mahiri
 Waandishi wa habari wa kampuni ya Mwananchi waliopata tuzo na walioingia fainali kwenye picha moja ya Mkurugenzi wa kampuni Tido Mhando,kaimu mhariri mkuu,Bakari Machumu ,Teophil Makunga
baadhi wa washindi toka Afya Redio Mwanza