Subscribe:

Ads 468x60px

TOHARA YA WAVULANA YAPAMBA MOTO SERENGETI

 WATOTO WA KIUME WALIOTAHILIWA KIENYEJI KATIKA KIJIJI CHA KENYEMONTA WILAYANI SERENGETI WAKIWA WAMEKAA WAKATI WA SHEREHE YA KUWAPONGEZA
 SHEREHE NI MTINDO MMOJA KAMA INAVYOONEKANA
 PONGEZI ZILIKWENDA SAMBAMBA NA BURUDANI YA MUZIKI WA ASILI
 NAYAWEZA MIMI
 HATA WATOTO WADOGO HAWAKUBAKI NYUMA
HAPA KILA MMOJA ALIPANDWA NA MIDADI.

MAANDAMANO YA EKARISI TAKATIFU

WAUMINI WA KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU FRANSISCO WA ASIZI MUGUMU WILAYANI SERENGETI WAKIANDAMANA SIKU YA EKARISTI TAKATIFU
MAANDAMANO KWA RIKA ZOTE KUELEKEA KANISANI
HATA WANAKWAYA WALIKUWEPO KAMA INAVYOONEKANA HAPO
PADRI ALOIS MAGABE AKIWA AMEBEBA EKARISTI TAKATIFU KAMA INAVYOONEKANA HAPO.PICHA ZOTE NA BLOG HII.

UTEGEMEZI WA MISAADA CHANZO CHA KUKARIBISHA USHOGA.



Padri Alois Magabe wa kanisa Katoliki Mugumu wilayani Serengeti
Serengeti:Nchi za  Magharibi kutoa misaada yenye masharti ya kuruhusu ushoga kwa nchi za Kiafrika ni matokeo ya kushindwa kutumia rasilimali walizo nazo kwa ajili ya kuendesha nchi zao.
Hivi karibuni kumekuwa na mjadala kwa nchi nyingi za Kiafrika kutokana na shinikizo la Nchi za Magharibi kuzishinikiza nchi za kiafrika ili zipate misaada zinatakiwa kukubali ndoa za jinsia moja.
Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Fransisco wa Asizi Mugumu wilayani Serengeti Alois Magabe  hivi karibuni akihubiri wakati wa misa ya Ekaristi Takatifu alisema utegemezi wa misaada ndiyo chanzo cha nchi hizo kutoa masharti yanayokinzana na maagizo ya Mungu kwa nchi za Kiafrika.
“Ukristo umeanzia nchi hizo za Magharibi miaka zaidi ya elfu mbili iliyopita….licha ya kujua masharti wanayoyatoa yanakinzana na maagizo ya Mungu aliyeweka ndoa ya mme na mke…..leo nchi kama za Marekani na Uingereza na washirika wao wanaziwekea masharti hayo   nchi zinazotaka misaada…sababu kubwa ni udhaifu wan chi hizi zenye rasilimali tele kutegemea misaada”alisema.
Alisema masharti kama waliyotoa kwa Uganda ni ishara tosha kuwa hawamuogopi Mungu ,na kuzitaka nchi zingine kuungana na msimamo wa Uganda kupinga ushoga kwa kuikataa misaada hiyo inayokweza utu wao ”misaada kama hii hatuhitaki bora ipotelee mbali huko”alisema na kushangiliwa.
Hata hivyo aliwataka viongozi wan chi hizo kubadili mitizamo ya kutaka kusaidiwa wakati utajiri walionao unazidi hata nchi hizo zinazotoa misaada kwa masharti,kwa kuwa wao wana nidhamu ya kukusanya na kutumia si kama ilivyo kwa nchi za kiafrika hakuna nidhamu ya matumizi ya mali za umma.
“Hiyo misaada yenye masharti wanayotaka kutoa kwa nchi zetu hizi wamekusanya Afrika kiujanja ujanja wanataka kuileta kwa masharti ya kijinga kijinga kisha wapata nafasi ya kuchota rasimali zetu”alisema.
Katika hatua nyingine alitaka serikali wilayani hapo kuhakikisha inamaliza mgogoro wa ardhi kati ya kigango cha Nyamburi cha kanisa Katoliki na serikali ya kijiji ambayo imeanzisha mnada kwenye eneo la kanisa ,hatua ambayo inaweza kuleta uvunjifu wa amani.
“Suala hili toka mwaka jana oktoba nimewaeleza lakini hakuna utekelezaji…..eneo la kanisa limeporwa kwa nguvu na baadhi ya viongozi wabovu wanaotumia nafasi zao vibaya ili kutafuta kura katika uchaguzi ujao….kwa hili nimewaandikia polisi nao wameahidi kufuatilia,maana suala hilo linaweza kupelekea uvunjifu wa amani”alibainisha.
Mwisho.

TAMISEMI YACHELEWESHA RORYA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII.

Wanufaika
                                







Pori la Selous lawekwa kwenye orodha ya Urithi wa Dunia ulio hatarini




Na Mwandishi wetu
20th June 2014

Waziri Maliasli na Utalii,Mh. Lazaro Nyalandu
Pori la Akiba la Selous limeingizwa katika orodha ya maeneo ya Urithi wa Dunia yaliyo hatarini. Uamuzi huu umefikiwa katika Mkutano wa 38 wa Kamati ya Urithi wa Dunia unaoendelea jijini Doha-Qatar.

Uamuzi wa kuingiza pori la Selous kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyo hatarini unalenga kuongeza uelewa wa jamii kitaifa na kimataifa kuhusu matatizo yanayolikabili eneo hilo ili kuwezesha upatikanaji wa misaada ya hali na mali ili kulirejesha katika hadhi yake ya asili.

Taarifa ya msemaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii, imesema kuwa tangu pori la akiba la Selous lilipowekwa kwenye orodha maeneo ya Urithi wa Dunia, hali yake kwa ujumla iliendelea kuwa nzuri na ya kuridhisha.

Hata hivyo, taaarifa ilieleza kuwa kuanzia mwaka 2010 hali ya pori hilo  pamoja na maeneo mengine nchini yamekumbwa na wimbi kubwa la ujangili, hususani wa Tembo na kuwa  hali hii imesababisha kupungua kwa idadi ya tembo katika mfumo ikolojia wa Selous kutoka tembo 70,000 mwaka 2006 hadi kufikia tembo 13,084 mwaka 2013.

Ilieleza kuwa kupungua kwa idadi ya wanyama katika Pori la Selous kuliilazimu Serikali kuchukua hatua za haraka kudhibiti hali hii ambazo ni pamoja na kuliongezea uwezo wa rasilimali fedha kwa kurejesha utaratibu wa awali wa kubakiza asilimia 50 ya mapato; kuandaa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kuhifadhi tembo na kuunda vikosi maalum vya pamoja miongoni mwa taasisi za wanyamapori vya kupambana na  ujangili katika kanda 11 nchini.

Pia, kuongeza idadi ya wahifadhi wanyamapori 105 ambao 40 kati yao walipangiwa eneo la kazi la Pori la akiba la Selous pamoja na usaili wa kuajiri wahifadhi wengine 437 umefanyika na kati yao 200 watapangiwa kazi katika pori la akiba la Selous.

Taarifa ilieleza kuwa Vilevile serikali iliongeza idadi ya vitendea kazi yakiwamo magari mapya nane, helikopta moja, ukarabati wa mitambo na magari, kuboresha huduma za jamii kwa watumishi pamoja na kukarabati miundo mbinu ya barabara, nyumba za watumishi na viwanja vya ndege.

Pori la akiba la Selous ni mojawapo kati ya maeneo saba yaliyo kwenye orodha ya Urithi wa Dunia nchini. Maeneo mengine ni Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Magofu ya Kilwa Kisiwani na Magofu ya Songo Mnara, Michoro ya Mimbani ya Kondoa, na Mji Mkongwe Zanzibar.

Malengo makuu na faida ya kuweka eneo kwenye orodha ya urithi wa dunia ni pamoja na kuwa na nguvu ya pamoja kimataifa ya kusimamia uhifadhi wa eneo; kujulikana kimataifa kama kivutio chenye sifa maalum cha utalii; kutumika kwa tafiti mbalimbali za uhifadhi pamoja; na kuvutia misaada ya kimataifa ya kiuhifadhi.

Kamati ya Urithi wa Dunia imeainisha vigezo 10 vinavyowezesha eneo kuorodheshwa kwenye orodha ya urithi wa dunia. Pori la akiba la Selous liliorodheshwa mwaka 1982.
CHANZO: NIPASHE