Subscribe:

Ads 468x60px

AFISA KILIMO,WAZABUNI WA PEMBEJEO WAPANDISHWA KIZIMBANI WAKIKABILIWA NA MAKOSA 50.


AFISA KILIMO,WAZABUNI WA PEMBEJEO WAPANDISHWA KIZIMBANI WAKIKABILIWA NA MAKOSA 50.
Aprili 11,2013
SERENGETI .

AFISA  kilimo na Mifugo wilaya ya Serengeti ,wazabuni wa pembejeo , watendaji wa vijiji,na wakulima wamefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara,wakikabiliwa na makosa 50 ya wizi wa fedha za Pembejeo zenye tahamani ya tsh,4,935,000=

Mwendesha mashitaka  Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Abdallah Idd amewataja Waliofikishwa mbele ya  Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama  hiyo, Amon Kahimba,  kuwa ni  Andrew Manyerere (55) Afisa kilimo/Mifugo wilaya, Nyitamboka Kitang’ita (61)wa kijiji cha  Majimoto, Karebu Ruji(41), Paulo Nyandito (50) wote wafanyabiashara wa pembejeo.

Wengine ni Joseph Petro (38) Afisa Mtendaji kijiji cha Rwamchanga, Damiani Nyamaheda (34) hakuwepo Mahakamani baada ya kutoroka, Emmanuel Mkamba (29)  mkulima mkazi wa kijiji cha Itununu na Pili Nyakimori (35) mkulima.

Mwendesha mashitaka aliambia Mahakama  iliyokuwa imefurika watu kuwa mwaka 2012 kwa nyakati tofauti katika vijiji vyao wanavyofanyia kazi mshitakiwa wa pili hadi wa nane wanatuhumiwa kula njama, kugushi sahihi za watu na kuchukua fedha za pembejo na kufanya tendo la
wizi.
Alisema mshitakiwa wa kwanza katika shauri hilo Andrew Manyerere ambaye ni Afisa kilimo na mifugo wilaya ya Serengeti anashitakiwa kwa kosa la uzembe baada ya kushindwa kuchukua hatua za kudhibiti wizi huo mapema.

Alisema washitakiwa saba, wakiwemo wafanyabiashara, wakulima na watumishi wa ummawaliopewa dhamana ya kusambaza  na kusimamia pembejeo kwa wakulima walikula njama na kugushi nyaraka, sahihi ambapo walijipatia fedha kati ya shilingi 100,000/= hadi 150,000/=,hata hivyo alisema viwango vya fedha na makosa yao yanatofautiana.
Akifafanua mashitaka hayo mwendesha mashitaka huyo aliiambia mahakama kuwa yanaangukia kwenye wizi kwa kuwa washitakiwa walikula njama za kuiba nakisha kuiba.

Kuhusu  mshitakiwa wa sita Damian Nyamaheda ambaye ni mfanyabiashara hakufikishwa Mahakamani kwa vile  hajakamatwa ,alisema  jeshi la polisi linaendelea
kumsaka.

Washitakiwa  wote walikana kuhusika na  mashitaka yanayowakabili ya kula njama na kugushi nyaraka  za pembejeo kujipatia fedha kinyume cha sheria walikana,na wako nje kwa dhamana  baada ya kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika hadi  aprili 23 mwaka huu  itakapotajwa tena.
Mwisho.

1 comments:

setcoserenget.blogspot said...

Hii kali mzee au ndo nguvu mpya ya Mirumbe nini?

Post a Comment