BARAZA LA KATIBA LA ASASI
WASHIRIKI WA BARAZA LA KATIBA LA ASASI YENYE MALENGO YANAYOFANANA WILAYANI SERENGETI(SENGONET)CHINI YA UFADHILI WA THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY
TEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI
SERONERA LOJI
TEMBO NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI
HAPO AKIPATA CHAKULA KUTOKA KWENYE MATAWI YA MTI JUU
TEMBO NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI
HAPO AKIPATA CHAKULA KUTOKA KWENYE MATAWI YA MTI JUU
ABAKA
MWENYEKITI
WA KITONGOJI ATUHUMIWA KUBAKA WATOTO WAWILI WA SHULE YA MSINGI,
Agosti
17,2013.
Serengeti;MWENYEKITI
wa kitongoji cha Matumaini kijiji cha Miseke kata ya Manchira wilayani
Serengeti Machaba Morumbe(53)(CCM)anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kubaka
watoto wawili wa shule ya msingi.
Matukio hayo
yanayodaiwa kutendeka kwa nyakati tofauti yamethibitishwa na polisi wilaya na
Shirika la wasaidizi wa kisheria na Haki za Binadamu(Washehabise)na uongozi wa
hospitali teule ya Nyerere ddh yanadaiwa kutokea agosti 9 na 13 katika
kitongoji hicho mwaka huu.
Akielezea matukio
hayo akiwa eneo la polisi Mwenyekiti wa
shirika hilo Samwel Mewama alisema ,tukio la kwanza linadaiwa kutokea agosti 9
majira ya saa 10 jioni,ambapo mtuhumiwa huyo anadaiwa kumbaka mwanafunzi wa
darasa la 5 mwenye umri wa miaka 12 shule ya msingi Zakhia Meghji kijijini hapo.
“Akiwa machungani
alimsihi mtoto huyo apeleke ng’ombe mtoni na kufika huko akambaka,huku
akimtishia kutosema…hakusema kabisa licha ya kuwa na maumivu makali…lakini
alipata ushujaa baada ya mwenzake kutendewa siku nyingine naye akawaeleza wazazi wake kuhusu unyama wa
kiongozi huyo”alisema Mewama.
Kujitokeza kwa mtoto
huyo alipokelewa na dawati la jinsia la polisi Mugumu na kufunguliwa jalada
Mug/dawati 148/2013 na kupelekwa hospitali teule ya Nyerere ddh kwa uchunguzi
zaidi.
Katika tukio la pili
mtuhumiwa huyo kwa mtindo ule ule anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la 3 mwenye umri wa miaka
10 Agosti 11 majira ya saa 11.00 jioni
mwaka huu wakati akichunga ng’ombe na mbuzi.
Mtoto huyo alisema
mtuhumiwa alimwambia eneo la mtoni kuna malisho mazuri ,walipofika ghafla
akamkamata na kumvua nguo na kuanza kumwingilia huku amemziba mdomo,na
kumsababishia majeraha sehemu za siri.
Baba mzazi wa mtoto
huyo jina tunalo alibaini hali hiyo baada ya kumwona mwanae akiwa katika hali
isiyo ya kawaida,na alipoulizwa alibainisha unyama aliotendewa na kiongozi huyo
na kuchunguza walibaini amechanika vibaya na kumpeleka hospitali kupitia polisi
na kufunguliwa jalada Mug/dawati 147/2013.
Mganga wa zamu
hospitalini hapo aliyejitambulisha kwa jina moja la Nyanokwe aliyempokea na kumfanyia uchunguzi
mtoto huyo amebaini kuchanika vibaya sehemu za siri na pia katika nyonga zake.
Mganga mkuu wa
hospitali teule ya Nyerere ddh,Dk,Kelvin Mwasha amethibitisha kumpokea mtoto
huyo kuwa wamemlaza wakiendelea na matibabu,hata hivyo mtuhumiwa ametoroka
kijijini baada ya kusikia anasakwa.
Mwisho.
JINSI MWL ALIVYOMFANYIA UKATILI MWANAE
MAJERAHA ALIYOPATA MTOTO HUYO BAADA YA KUPIGWA NA BABA YAKE AMBAYE NU MWL SHULE YA MSINGI MOROTONGA WILAYANI SERENGETI ,KISHA KUMWEKEA PILIPILI NA KUMLAZIMISHA KULA KINYESI
MWANAFUNZI ALIYEFANYIWA UKATILI NA BA A YAKE AMBAYE NI MWL
MWALIMU AMFANYIA UKATILI MWANAE,AMWEKEA PILIPILI KWENYE VIDONDA NA KUMLAZIMISHA KULA KINYESI CHAKE.
Serengeti:MWALIMU wa shule ya
MsingI Morotonga wilayani Serengeti Karata Mugunda anashikiliwa na polisi kwa tuhuma
ya kumpiga kisha kumlazimisha kula kinyesi mwanae wa darasa la tano aliyedaiwa
kujisaidia ndani kwa kuogopa kwenda nje sababu ya giza.
Tukio hilo ambalo limepokelewa
kwa hisia tofauti na wananchi linadaiwa kutokea agosti 13,2013 majira yausiku
nyumbani kwa mwalimu huyo anayeishi shuleni,limethibitishwa na Mwalimu mkuu wa
shule,polisi,wanaharakati na uongozi wa hospitali teule ya Nyerere ddh.
Akisimulia tukio hilo Mwenyekiti
mtendaji wa shirika la Wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu wilaya ya Serengeti(Washehabise)Samwel
Mewama amesema ,mtoto huyo alisema aliogopa kwenda kujisaidia nje kutokana na
giza nene na kujisaidia ndani ,hatua iliyopelekea kupata adhabu hiyo.
“Baba yake licha ya kutambua umri
wake na nafasi a;liyonayo aliamua kumfanyia ukatili mwanae ikiwa ni kinyume cha
sheria ya mtoto ya mwaka 2009… kumpiga bila huruma…matako yameharibiwa kwa
viboko…kana kwamba haitoshi akachukua kitambaa na kuweka pilipili
akamwekea…kisha akamlazimisha kula kinyesi chote na hakumpa huduma ya
tiba”alisema.
Mewama alisema agosti 14 baba
yake alimlazimisha kwenda shuleni ,hata hivyo hakuweza kukaa kutokana na
vidonda matakoni”mwalimu wa darasa alipomuuliza na kueleza ,akaona hali
aliyonayo akanipigia simu…nilikwenda kumchukua nikampeleka hospitali kupitia polisi”alibainisha.
Alisema kabla ya kwenda alimpigia
simu baba yake lakini akamjibu aendelee na hatua anayoona inafaa ,na kulazimika
kumfikisha hospitali Teule ya Nyerere ddh,hata hivyo alipokea simu ya vitisho
kutoka kwa mwalimu huyo kuwa hana imani na chakula anachompa,hali iliyompelekea
kumkabidhi Mwalimu mkuu wa shule hiyo aliyemtaja kwa jina la Mlay,ambaye naye
alitishwa na mtuhumiwa.
Kutokana na vitisho hivyo Mwalimu
Mlay alilazimika kutoa taarifa polisi na mtuhumiwa kukamatwa na polisi wamesema
atafikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya taratibu kukamilika,huku mtoto
akiwa amekabidhiwa ndugu zake kwa uangalizi zaidi.
Akiongea kwa wasiwasi mtoto huyo
alisema ,hiyo ni mara ya tatu anapigwa na kuumizwa yeye na ndugu zake,na kuwa
mama yao aliachika kutokana na vipigo na mama yao mdogo ndiye anawachongea yeye
na ndugu zake watano ili wafukuzwe hapo.
Mmoja wa wanafunzi wa darasa la
tano jina tunalo alisema tabia ya kupiga si kwa watoto wake tu hana wanafunzi
darasani anawachapa bila utaratibu maalum,na walimu wanajua lakini wanaonekana
kumwogopa kuwa ni mkorofi.
Baadhi ya walimu wamesema matukio
ya kupiga watoto ni ya mara kwa mara lakini hilo ni kubwa zaidi nainapaswa
sheria ichukue mkondo wake.
Mganga wa zamu Hooka Paul alisema
majeraha hayo ni makubwa na anapaswa kupata kinga ya tetenasi kwa kuwa
amechelewa kupata matibabu,na kisaikolojia mtoto huyo ameathirika kwa kuwa anastuka
mara kwa mara.
Polisi wanaendelea na mahojiano
kwa walimu wengine na wamesema utaratibu ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Mwisho.
CHADEMA WAKUSANYA MAONI YA RASIMU
CHOPA YA CHADEMA ILIYOMBEBA KATIBU MKUU WA CHADEMA DK.WILBROAD SLAA IKIWAAMBAA KIWANJA CHA KILOMBELO JIJINI ARUSHA KWA AJILI YA BARAZA LA KATIBA .
CHOPA LA CHADEMA
DR WILBROAD SLAA AKIWASILI UWANJA WA KILOMBELO JIJINI ARUSHA
BAADHI YA WANANCHI WAKIFUATILIA MKUTANO WA BARAZA LA KATIKA KIWANJA CHA KILOMBELO JIJINI ARUSHA
CHOPA LA CHADEMA
DR WILBROAD SLAA AKIWASILI UWANJA WA KILOMBELO JIJINI ARUSHA
BAADHI YA WANANCHI WAKIFUATILIA MKUTANO WA BARAZA LA KATIKA KIWANJA CHA KILOMBELO JIJINI ARUSHA
UKUKWAJI HAKI ZA BINADAMU
WALIMU WALALAMIKIWA KWA UBAGUZI WA UKABILA.
Serengeti:UBAGUZI wa kikabila,ukiukwaji wa Haki
za Binadamu unadaiwa kutawala zoezi la kuhamisha wafugaji katika kijiji cha
Nyamokhobiti kata ya Maji moto Tarafa ya
Ngoreme wilayani Serengeti,umevuka mipaka hadi shuleni .
Ubaguzi huo umeanza kuleta madhara kufuatia baadhi ya watoto
wa wafugaji wa jamii ya Wakenye kutoka wilaya ya Butiama waliokuwa wanasoma
Isereserekutokwenda shule kwa madai ya ubaguzi kutoka kwa walimu wa shule hiyo
ambao wengi ni kabila la Wangoreme wazawa wa kijiji hicho.
Alex Mang’era(68)mfugaji alisema aliingia kijijini hapo mwaka
2003 kwa kuridhiwa na serikali ya kijiji na mkutano mkuu,na wanae watatu
wanaosoma hapo kwa sasa hawaendi shule kutokana na ubaguzi ulio ndani ya jamii
na walimu wa shule.
“Wanangu Kadogo Alex wa darasa la 6,Neema na Habibu wa darasa
3 hawaendi shule…wanabaguliwa na wanafunzi,jamii nahadi walimu kuwa ni Wakenye
warudi kwao Butiama ….wamezaliwa na kuanzia shule hapa..mimi nimekaa miaka
10…nimepiga kura hapa…ubaguzi huu ni mbaya sana”alisema kwa masikitiko.
Alisema shule hiyo yenye walimu 7 watano ni wazawa wakijijini
hapo na wanaishi kwenye miji yao ,badala ya kutekeleza majukumu yao wamegeuka
kuwa sehemu ya jamii,wanashiriki vikao vya kimila ritongo na matokeo yake
wanapeleka ubaguzi shuleni.
Moroni Nyancharu(30)wa
kitongoji Getenga kijijini hapo anasema
katika zoezi hilo mtoto wake Bhoke Mroni
wa darasa la kwanza haendi shule kwa kuhofia usalama wake,na kubaguliwa .
”Walimu wanatutukana sisi kuwa Watoto wa Wakenye ni wajinga
hamjui kusoma…na wanafunzi nao wanatutukana kuwa sisi ni watu wa kuja…njiani
mkipita jamii inatuzomea kuwa Makenye mrudi wilayani kwenu…hatuna raha
shuleni”anasema mwanafunzi wa darasa la tatu jina tunalo.
Ofisa elimu akiri.
Ofisa elimu ufundi wilaya Christopher Mossi alikiri kuwa
walimu karibu wote ni wazawa wa kijijini hicho,”ni kweli ni hapo…kwa malalamiko
hayo tunafuatilia kwa kuwa yanalenga kuwanyima elimu hao watoto”alisema.
Mwenyekiti wa serikali
ya kijiji cha Iseresere Mosi Ng’ombe alipotakiwa kujibu tuhuma za kuwapokea
wafugaji na sasa amewakana,alisema yeye hawezi kulizungumzia hilo labda aulizwe
mkuu wa mkoa ama Dc.
Agizo la RC latekelezwa na wazee wa mila badala
yaSerikali ya kijiji.
Katika hali isiyo ya kawaida
ambayo imechangia ukiukwaji wa Haki za Binadamu agizo la Mkuu wa Mkoa wa
Mara John Tupa la kuhamisha wafugaji
haramu linatekelezwa na wazee wa mila chombo kisicho cha kiserikali.
Uamzi huo umelalamikiwa na makundi ya wanaharakati akiwemo
Mbunge wa jimbo hilo Dk,Stephen Kebwe ambaye aliiambia blog hii kuwa chombo hicho hushughulikiwa masuala ya
ulinzi na usalama ,lakini hakina nguvu kwa maagizo ya kiserikali kama hayo.
“Zoezi lilikuwa na nia njema lakini njia zilizotumika si
sahihi…huwezi tumia ritongo kwa agizo la serikali wakati inavyombo vyake…uonevu
,ukiukwaji haki utatendeka…pia kuna udhaifu katika zoezi hilo maana hakuna
waraka wenye maelekezo alioutoa kwa watekelezaji,hii inaweza kuleta
vurugu”alisema Mbunge.
Alikwenda mbali zaidi na kudai ameishamwambia mkuu wa mkoa
ajaribu kuangalia vema suala hilo kwa kuwa tafsri ya mhamiaji haramu
ijulikane,na wabainishwe na wananchi ,kwa kuwa watu walipokea kwa utaratibu
,wameishi miaka mingi,wanamazao,wana vitu kuwaondoa kwa kutumia ritongo
hawatapata muda wa kuweka sawa mali zao,wala kusikilizwa.
Wazee wa mila wafunga
zizi kwa dawa.
Mbali na malalamiko ya ubaguzi na ukiukwaji haki za
binadamu,wazee wa mila wamelazimika kufunga zizi la ng’ombe wa Simion Maitari
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Nyamokhobiti kijiji jilani kwa kuweka
matawi ya miti ambayo inaaminika kuwa wamezindika ng’ombe wakirudi humo
watakufa,na wao ndio wenye uwezo wa kuzindua tego hilo.
Majeruhi.
Wakati Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara Ferdinand Mtui na Mwenyekiti wa serikali ya
kijiji cha Iseresere Mosi Ng’ombe kudai kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa wakati wa
zoezi la kuwafukuza wafugaji,Mwananchi imebaini watu wawili kujeruhiwa kwa kupigwa na
kukatwa kwa sime.
Polisi kituo cha Maji moto kimekiri kuwapokea majeruhi hao na
kuwapa Pf 3 agosti 5 ,mwaka huu iliyosainiwa ditektivu Mohammed ambayo nakala
yake tumeiona ,pia hati ya kuwakamata watuhumiwa George Rabani na Mohi Morigo
kwa kosa kujeruhi Ref No MAJ/RB/281/2013 hata hivyo hawajakamatwa
Wanaharakati.
Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la Wasaidizi wa
Kisheria na Haki za Binadamu (Washehabise)Samwel Mewama anasema zoezi hilo
limekiuka haki za binadamu,kwa kuwa linavunja katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka
1977.
“Ibara ya 17,uhuru wa mtu kwenda atakako,sheria ya 1984 na ibara ya 24 haki ya kumiliki mali,kwa
kitendo hiki kilichofanyika ni uvunjaji wa katiba,watu wamekosa haki ,watoto
wanashida ya chakula,wameacha mazao,chombo kinachotumika kutekeleza si cha
kisheria,tutahakikisha haki inatendeka,maana mhamiaji haramu anawezaje kuchagua
kiongozi yeye akawa halali”anasema.
Rc
Mkuu wa mkoa wa Mara John Tupa anasema waraka wake amesambaza
kwa wakuu wa wilaya,na kuwa mwisho wa zoezi hilo ni agosti 16 mwaka huu,hata
hivyo waraka huo wakuu wa wilaya hawajausambaza kwa viongozi wa vijiji .
Mwisho.
JELA MIAKA MINANE KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO
ALIYEKUTWA NA MENO YA
TEMBO AHUKUMIWA MIAKA 8 JELA.
Serengeti:MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi mfawidhi wa
wilaya ya Serengeti imemhukumu Idd Abdallah
Adamu (39 ) mkazi wa Nyakato Mwanza miaka 8 jela kwa kosa la kupatikana na meno ya tembo kilo 46 yenye thamani ya sh, 26,250,000 .
Katika kesi hiyo ya uhujumu
uchumi namba 59/2011 washitakiwa wengine kwenye shitaka hilo Lameck
James (29) mkazi wa Sirari, Kasika John(46) mkazi wa Ushashi Bunda na Mwita
John(44) mkazi wa kijiji cha Kibeyo wilaya ya Serengeti wameachiwa huru kutokana na udhaifu wa polisi
kushindwa kuwasilisha fedha sh.3,835,000 walizokutwa nazo mahakamani kama ushahidi siku ya tukio.
Hakimu Amon Kahimba wa mahakama
hiyo alisema,mshitakiwa Adamu amekumbwa na adhabu kufuatia ushahidi
uliowasilishwa mahakamani hapo kuanzia maelezo ya polisi ,mahakamani na
mashahidi kuwa vipande vinne vya meno ya tembo vilikutwa ndani ya chumba
alichokuwa amelala nyumba ya wageni ya Leopard.
Na kuwa alikiri kununua meno hayo,kwa
washitakiwa wawili kwa sh,2,400,000 na
washitakiwa Lameck James na Kasika John walikiri kununua vipande hivyo vya meno kwa mshitakiwa wanne Mwita John
kwa sh,200,000,na fedha walizokutwa nazo hotelini sh,3,835,000 hazikuwasilishwa
mahakamani kama kielelezo licha ya washitakiwa kuzidai.
“Kutokana na maelezo yote ya
ushahidi na washitakiwa ,mahakama inamhukumu Idd Abdallah miaka minane jela…na
wengine wanaachiwa huru kutokana na uzembe wa polisi..wote hawa wangehukumiwa
kama mpelelezi wa kesi na aliyekuwa Oc Cid wilayani hapo kwa sasa Mkuu wa
Operesheni Mkoani Arusha Paul Ngonyani aliyewakamata,kuwapekua,lakini hakufika
kutoa ushahidi mahakamani licha ya kuitwa na wala fedha alizowakutana nazo
hazikuwasilishwa kama ushahidi”alisema.
Alikwenda mbali hakimu huyo na
kudai kuwa kosa la kujihusisha na biashara ya meno ya tembo mazingira yake wangekutwa na mzigo au pesa,lakini wao
walikutwa na pesa katika nyumba ya kulala wageni ya Galaxy Motel ,lakini
hazikuwasilishwa mahakamani.
Aliomba jeshi la polisi nchini
liwachukulia hatua kali Paulo Ngonyani ,kwa kushindwa kufika kutoa ushahidi
kwenye kesi hiyo licha ya kuitwa mara tatu,na mpelelezi wa shitaka hilo Ditektivu
Sajenti Yona,kwa kutowasilisha fedha za
washitakiwa ambazo wamezidai na mahakama ikaagiza ziwasilishwe mahakamani..
Mapema mwendesha mashitaka
inspekta msaidizi wa Polisi Abdallah Idd aliitaka mahakama hiyo kutoa adhabu
kali kwa mshitakiwa ili liwe fundisho kwa wengine kwa kuwa makosa ya uhujumu
uchumi yamekithiri hapa nchini.
Katika utetezi wake Adamu aliomba
ahurumiwe kwa kuwa ni kosa lake la kwanza ,ana watoto 5,mke na watu
wanaomtegemea.
Februari 18,2013 katika mahakama hiyo mshitakiwa
huyo aliyehukumiwa aliyekuwa akijifanya Mmachinga anayetembeza vyombo kutoka
Mwanza aliachiwa huru na mahakama hiyo
katika kesi 184/2011 ya uhujumu uchumi baada ya kukamatwa katika nyumba
ya kulala wageni ya Silent Inn mjini Mugumu wakiwa na meno mawili ya tembo.
Katika kesi hiyo ilimhusisha
mmiliki wa nyumba hiyo Julius Mwita Marwa(43)waliachiwa na Hakimu Amon Kahimba
kwa kutumia kifungu cha sheria namba 235 cha mwenendo wa makosa ya jinai
kilichorekebishwa mwaka 2002 kwa madai kuwa upande wa mashitaka ulikuwa dhaifu.
Mwisho.
MADHIRA YA WAFUGAJI SERENGETI
BAADHI YA WANAHARAKATI KUTOKA SHIRIKA LA WASAIDIZI WA KISHERIA NA HAKI ZA BINADAMU WILAYANI SERENGETI WAKIWA NA BAADHI YA WAFUGAJI KATIKA MAENEO WALIYOFUKUZWA
FAMILIA HIYO NI YA MWENYEKITI WA SERIKALI YA KIJIJI CHA NYAMOKHOBITI KATA YA MAJI MOTO KIJIJI JILANI NA ISERESERE NAYO IMEFUKUZWA KAMA WAHAMIAJI HARAMU
MZOGA WA NG'OMBE ALIYEKUFA BAADA YA KUPIGWA NA WANANCHI WAKATI WA ZOEZI LA KUHAMISHWA |
UKATILI WAFUGAJI
Add caption |
HAPO NI OFISI YA SERIKALI YA KIJIJI CHA NYAMOKHOBITI KATA YA MAJIMOTO WILAYNI SERENGETI
NG'OMBE HUYO ALIACHWA BAADA YA KUPIGWA NA WANARITONGO WAKATI WA KUHAMISHA WAFUGAJI ,ALIBAKI BAADA YA KUSHINDWA KUTEMBEA,WAPO WALIOKUFA KWA KIPIGO NA KUZAMISHWA MTO MARA,KUPOTEA.
NYUMBA HIYO ILIEZULIWA NA WANANCHI WALIOKUWA WAKITEKELEZA AGIZO LA MKUU WA MKOA JOHN TUPA,HATA HIVYO HAWANA WARAKA WA MAELEKEZO .FAMILIA ILIPOTEZA NG'OMBE WAKATI WA ZOEZI HILO LINALODAIWA KUKIUKA HAKI ZA BINADAMU.
BODABODA
MAKAMANDA WA CHAMA CHA WAEBDESHA PIKIPIKI(BODA BODA )WILAYANI SERENGETI WAKIWA WAMEMDHIBITINMWENZAO BAADA YA KUKIUKA MAADILI YA WALIYOJIWEKEA WAKATI WANAPOKUWA KWENYE MIKUTANO YAO.
CHINI YA ULINZI KWA KUKIUKA MAADILI
UTII BILA SHURUTI KWA BODA BODA
BODA CHINI YA ULINZI
CHINI YA ULINZI KWA KUKIUKA MAADILI
UTII BILA SHURUTI KWA BODA BODA
BODA CHINI YA ULINZI
TEMBO ALIVYOMUUA FARU
THE CITIZEN SUNDAY August 4,
2013
Elephant kills Protected rhino in bizarre fight
By Anthony
Mayunga and Syriacus Buguzi The Citizen Reporters
In Summary
In Summary
The
bizarre incident occurred at Nyabikwabe area in Natta ward on Thursday evening
and has compelled conservationists and game experts to scratch their heads
hard, in attempts to find appropriate answers to the killing.
Serengeti/Dar
es Salaam. In what has puzzled game officers and authorities, an elephant
reportedly killed one of two heavily protected rhinos at Makunduzi village in a
reserve run by Singita Grumeti Fund.
The
bizarre incident occurred at Nyabikwabe area in Natta ward on Thursday evening
and has compelled conservationists and game experts to scratch their heads
hard, in attempts to find appropriate answers to the killing.
The
incident was confirmed by both the wildlife director, Prof Alexander Songorwa
and the management of Singita Grumeti reserve.
Prof
Songorwa said the rhino called Limpopo, was one of the two remaining out of the
five brought to the reserve from South Africa in 2007. The animals were
famously referred to as ‘Kikwete Rhinos’ in recognition to efforts by President
Jakaya Kikwete to have the rare white Rhinos bred in the country.
President
Kikwete personally received the huge animals that are among major tourist
attractions when they were first flown in from South Africa. Three of them
vanished in circumstances that include killings by brazen poachers. The
President ordered a manhunt for the perpetrators, in the wake of which one
Thomas Nchagwa was arrested and arraigned in court in 2010.
He was
charged under economic sabotage laws, but the suspect and those who had bailed
him subsequently disappeared.
The rhino
killed on Thursday was male and the youngest. “It was aged 11 when it met its
sudden demise,” said Prof Songorwa.
He said
the rhino, which was well protected in a fenced enclosure, was furious when it
spotted the elephant that had entered its habitat by tearing through the fence.
“It
charged at the elephant to chase it out, igniting what looked like a furious
fight between the two animals. They fought for some time before the rhino was
overpowered and lost the fight,” he explained.
He said
one of the elephant tusks pierced the rhino’s underbelly while the second one
sank deep into the rhino’s hump, killing it instantly. “It has taught us a big
lesson,” he said, noting that poaching was the only threat to such rare animals
until that fateful day.
In
reaction to inquiries by The Citizen on Sunday on the security of the animals
in the reserves, Prof Songorwa explained that the incident happened so suddenly
that it was not easy for the wardens to intervene during the fight.
He said
no one expected that the elephant could trespass into the rhino’s enclosure at
that time. It is reported that the fighting occurred in the twilight hours and
the wardens’ attention was drawn when the rhino was already dead.
He said following the death of the male rhino, efforts were underway to find
a replacement since the rhinos customarily live in pairs.The management of the company declined to comment but game warders confessed that intrusion by elephants into the area had never occurred previously.
Rare phenomenon
In a separate interview, an expert in tourism management said such incidences usually happen but the cases were very rare.
‘’Fighting usually occurs when the animals struggle to win feeding grounds. Both the elephant and rhino are browsers; they feed on green leaves on top of trees. This leaves a competing ground for them,’’ said Mr Asantael Melita, Ngorongoro’s principal tourism officer.
Mr Malita explained that one animal was likely to kill on its rival, depending on which one is older or bigger in size, but swiftly pointed out that such behaviour was usually abnormal amongst the animals.
‘’An elephant can knock a rhino over and trample it by driving a tusk through its chest. If the elephant is older, it’s likely to kill the rhino,’’ he further explained.
TEMBO AUA FARU
KUUAWA KWA FARU HUYO KUMETHIBITISHWA NA MKURUGENZI WA WANYAMA PORI TANZANIA PROFESA ALEXANDRE SONGORWA NA KUDAI KUWA WALIKUWA KWENYE ENEO MAALUM KAMA MRADI WA KAMPUNI HIYO,NA KUWA TEMBO DUME ALIPOINGIA KATIKA HIMAYA YA FARU HAO KULIPELEKEA FARU KUCHACHAMAA NA KUMFUKUZA NDIPO AKAMCHOMA KWA JINO LAKE SEHEMU YA MOYO NA KUMBANA SEHEMU YA NUNDU NA KUFA PAPO HAPO.
MBALI NA UJANGILI WA WANYAMA HAO PIA TEMBO NA FARU NI WANYAMA WASIOPATANA NA HUISHI KWA KUKWEPANA.
WATHAILAND WAFURAHIA UTALII SERENGETI
NIKIWA NA MIHAYO NA MUSSA KIKAZI ZAIDI WAKATI WA ZIARA YA WAZIRI MKUU WA THAILAND YINGLUCK SHIWANATRA
MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPA AKIWA NA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII KHAMISI KAGASHEKI,WENGINE NI MKURUGENZI WA TANAPA ALLAN KIJAZI
MKUU WA MKOA WA MARAJOHN TUPA,MKURUGENZI WA WANYAMA PORI TANZANIA PROFESA ALEXANDRE SONGORWA NA BAADHI YA WATU WALIOAMBATANA NA WAZIRI MKUU WA THAILAND UWANJA WA NDEGE SERONERA
CHAKULA HIKI KILITUMIKA KWA WAGENI WA THAILAND NA WATANZANIA HOTEL YA FOUR SESSION SAFARI LTD
WAZIRI KAGASHEKI,KIJAZI NA MMOJA WA WAGENI WALIOKUWEPO ZIARA YA SHINAWATRA
Utalii wamkuna Waziri Mkuu wa Thailand
MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPA AKIWA NA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII KHAMISI KAGASHEKI,WENGINE NI MKURUGENZI WA TANAPA ALLAN KIJAZI
MKUU WA MKOA WA MARAJOHN TUPA,MKURUGENZI WA WANYAMA PORI TANZANIA PROFESA ALEXANDRE SONGORWA NA BAADHI YA WATU WALIOAMBATANA NA WAZIRI MKUU WA THAILAND UWANJA WA NDEGE SERONERA
CHAKULA HIKI KILITUMIKA KWA WAGENI WA THAILAND NA WATANZANIA HOTEL YA FOUR SESSION SAFARI LTD
WAZIRI KAGASHEKI,KIJAZI NA MMOJA WA WAGENI WALIOKUWEPO ZIARA YA SHINAWATRA
Utalii wamkuna Waziri Mkuu wa Thailand
Kwa ufupi
Alisema
kutokana na ziara hiyo, Tanzania na Thailand zimekubaliana na kutiliana saini
mkataba wa miaka mitatu wa ushirikiano katika kulinda, kuendeleza na kukomesha
biashara haramu ya wanyamapori.
Dar es
Salaam. Ziara ya siku tatu ya Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra
imemvutia kiongozi huyo na kuahidi kufanya ziara binafsi katika mbuga za
wanyama akiambatana na familia yake.
Akizungumza
wakati wa kumuaga waziri huyo aliyeondoka nchini jana, Waziri wa Maliasili na
Utalii, Balozi Khamisi Kagasheki, alisema ziara ya Shinawatra imekuwa ya
mafanikio makubwa kwa taifa.
Alisema
kiongozi huyo ameahidi kurudi nchini wakati wowote akipata nafasi.
“Amesema
anakwenda lakini atarudi katika ziara ya kibinafsi yeye na mume wake, mtoto
wake na ndugu zake na tumemwambia akiwa tayari atufahamishe,” alisema Balozo
Kagasheki.
Alisema
kutokana na ziara hiyo, Tanzania na Thailand zimekubaliana na kutiliana saini
mkataba wa miaka mitatu wa ushirikiano katika kulinda, kuendeleza na kukomesha
biashara haramu ya wanyamapori.
Mkataba
huo ulisainiwa na Balozi Kagasheki na Naibu Waziri Mkuu wa Thailand Plodprasop
Suraswad, aliyeambatana na Shinawatra.
Akizungumzia
manufaa ya mkataba huo, Waziri Kagasheki alisema utasaidia taifa kuongeza
mapato kupitia sekta ya maliasili kwa kuongeza watalii.
MKATABA WA ULINZI WA MALIASILI WASAINIWA
TANZANIAYATILIANASAINI NA THAILAND MKATABA
WA KULINDA MALIASILI NA KUKOMESHA
UJANGILI,
Julai 31,2013.
Serengeti:SERIKALI ya Tanzania
imetiliana saini mkataba wa maelewano wa
miaka mitatu wa ushirikiano wa kulinda na kuendeleza maliasili na Utalii na
Jamhuri ya Kifalme ya watu wa Thailand.
Mkataba huo umesainiwa na Waziri
wa Maliasili na Utalii balozi Khamisi Kagasheki kwa niaba ya serikali ya
Tanzania na Naibu Waziri Mkuu wa
Thailand Plodprasop Suraswad aliyeambatana na Waziri Mkuu wa Thailand
Yingluck Shinawatra kwenye ukumbi wa Four Session Safari Hotel Ltd iliyoko hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Akizungumzia manufaa ya mkataba
huo Waziri Kagasheki amesema hatua hiyo itasaidia taifa kuongeza mapato kupitia
sekta ya Maliasili kwa kuongeza watalii kutoka milioni moja kwa sasa kama
ilivyo kwa nchi ya Thailand pamoja na raslimali chache wanapata watalii hadi
milioni 22 kwa mwaka.
“Tunataka mchango wa maliasili katika pato la Taifa utoke asilimia 17 …hali hiyo ikienda sambamba na kuongeza pato
la wananchi….maana Thailand kupitia utalii pato la Mwananchi ni dola 5,000 kwa
mwaka …na ndio mpango wa taifa wa
20-25”alisema.
Waziri wa uwezeshaji na Uwekezaji
Dk,Mary Nagu amesema mkataba huo
unafungua fursa za uwekezaji ambao utainua pato la taifa katika sekta ya
utalii,pia kilimo na madini.
“Tanzania tuna fursa nyingi
lakini hatujafanya vizuri kwa ajili ya kujipatia mapato….tuna maliasili nzuri
na kubwa tunawazidi Kenya …lakini wao wana vitanda 11,000 wakati sisi
tunavitanda 6,000 sasa tunakusudia kukuza kwa kasi sekta hii kwa kushirikiana
na nchi ambazo zinamwelekeo na zinazofanya vizuri”alisema.
Alisema ili kuhakikisha
watanzania wananufaika na uwekezaji kama huo ,kwa upande wa madini serikali
haitauza madini ghafi bali kuyatengeneza na kuwa vito ili yaongezewe thamani
,na watanzania wakipewa fursa ya kwanza kwa kuangalia watakavyonufaika.
Alisema ziara hiyo imekuja siku
chache baada ya viongozi wa mataifa ya China,Marekani na Uingereza kutiliana
mikataba ya kimaendeleo na taifa la Tanzania..
Mkurugenzi wa Wanyamapori
Tanzania Profesa Alexander Songorwa
alisema ,wanategemea kuimarisha utalii na kupunguza tatizo la ujangili kwa kuwa
nchi hizo zote zitahusika katika masuala ya ulinzi na usimamizi.
“Soko la meno ya Tembo kutoka
Tanzania ni kubwa nchini Thailand na China …kwa mkataba huu sasa nao
watashiriki kukabiliana na vitendo hivyo vya uharifu,na hiyo nafasi itatusaidia
sisi kudhibiti hali hiyo…maana ujangili wa tembo ni changamoto kubwa kwa
uhifadhi hapa Tanzania”alisema.
Mapema Mhifadhi Mkuu wa hifadhi
ya Taifa ya Serengeti William Mwakilema akitoa taarifa ya hifadhi hiyo alisema
mbali na kuwa kivutio kikubwa kwa wageni,bali wanakabiliwa nanchangamoto za
askari wachache wa ulinzi wa wanyama pori,nyumba za askari ,maji ,barabara za
ndani na jamii zinazowazunguka .
Kwa upande wa falme za Thailand
walisema ,Raslimali za Tanzania zikilindwa na kusimamiwa vema zitasaidia kuinua
uchumi kwa kasi kubwa,kwa kuwa wana vitu ambavyo havipo katika maeneo
mengine,lakini hawajafanya vizuri.
Mwisho.
SAINI YA MAKUBALIANO
WAZIRI MKUU WA THAILAND YINGLUCK SHANAWATRA AKIANGALIA MCHORO WA MZUNGUKO WA NYUMBU
WANAKABIDHIANA MKATABA WA MAELEWANO
TEMBELEA www.antonymayunga.blogspot.com
UWANJA WA NDEGE WA SERONERA KIKAZI WAKATI TUKIMSUBIRI WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA KIFALME YA THAILAND SHINAWATRA
HATKUWA PEKEE YETU HAWA NI BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI NA MAAFISA WA USALAMA WA THAILAND WAKIWA UWANJA WA NDEGE SERONERA KUMSAUBIRI WAZIRI MKUU
WAZIRI WA UWEZESHAJI NA UWEKEZAJI DK.MARY NAGU AKIHOJIWA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA HOTEL YA FOUR SESSION SAFARI LTD,ILIYOKO HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI
MAZINGIRA YA HOTELI YA FOUR SESSION SAFARI LTD YANAPENDEZA
CHAKULA HII UNAPATA HOTELINI HAPO
WAKATI MWINGINE WAHITAJI KUPUMZIKA NA KUFURAHIA UUAMBAJI WA MUNGU
KAMA ILIVYO HAPO
WAKATI MWINGINE HUACHI KAMERA KAMA ILIVYO KWA ASKARI KWA KUWA MATUKIO MENGINE NI YA KUSTUKIZA HASA UWAPO MAENEO YA HIFADHINI
HATKUWA PEKEE YETU HAWA NI BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI NA MAAFISA WA USALAMA WA THAILAND WAKIWA UWANJA WA NDEGE SERONERA KUMSAUBIRI WAZIRI MKUU
WAZIRI WA UWEZESHAJI NA UWEKEZAJI DK.MARY NAGU AKIHOJIWA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA HOTEL YA FOUR SESSION SAFARI LTD,ILIYOKO HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI
MAZINGIRA YA HOTELI YA FOUR SESSION SAFARI LTD YANAPENDEZA
CHAKULA HII UNAPATA HOTELINI HAPO
WAKATI MWINGINE WAHITAJI KUPUMZIKA NA KUFURAHIA UUAMBAJI WA MUNGU
KAMA ILIVYO HAPO
WAKATI MWINGINE HUACHI KAMERA KAMA ILIVYO KWA ASKARI KWA KUWA MATUKIO MENGINE NI YA KUSTUKIZA HASA UWAPO MAENEO YA HIFADHINI
Subscribe to:
Posts (Atom)