Serengeti:MWALIMU wa shule ya
MsingI Morotonga wilayani Serengeti Karata Mugunda anashikiliwa na polisi kwa tuhuma
ya kumpiga kisha kumlazimisha kula kinyesi mwanae wa darasa la tano aliyedaiwa
kujisaidia ndani kwa kuogopa kwenda nje sababu ya giza.
Tukio hilo ambalo limepokelewa
kwa hisia tofauti na wananchi linadaiwa kutokea agosti 13,2013 majira yausiku
nyumbani kwa mwalimu huyo anayeishi shuleni,limethibitishwa na Mwalimu mkuu wa
shule,polisi,wanaharakati na uongozi wa hospitali teule ya Nyerere ddh.
Akisimulia tukio hilo Mwenyekiti
mtendaji wa shirika la Wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu wilaya ya Serengeti(Washehabise)Samwel
Mewama amesema ,mtoto huyo alisema aliogopa kwenda kujisaidia nje kutokana na
giza nene na kujisaidia ndani ,hatua iliyopelekea kupata adhabu hiyo.
“Baba yake licha ya kutambua umri
wake na nafasi a;liyonayo aliamua kumfanyia ukatili mwanae ikiwa ni kinyume cha
sheria ya mtoto ya mwaka 2009… kumpiga bila huruma…matako yameharibiwa kwa
viboko…kana kwamba haitoshi akachukua kitambaa na kuweka pilipili
akamwekea…kisha akamlazimisha kula kinyesi chote na hakumpa huduma ya
tiba”alisema.
Mewama alisema agosti 14 baba
yake alimlazimisha kwenda shuleni ,hata hivyo hakuweza kukaa kutokana na
vidonda matakoni”mwalimu wa darasa alipomuuliza na kueleza ,akaona hali
aliyonayo akanipigia simu…nilikwenda kumchukua nikampeleka hospitali kupitia polisi”alibainisha.
Alisema kabla ya kwenda alimpigia
simu baba yake lakini akamjibu aendelee na hatua anayoona inafaa ,na kulazimika
kumfikisha hospitali Teule ya Nyerere ddh,hata hivyo alipokea simu ya vitisho
kutoka kwa mwalimu huyo kuwa hana imani na chakula anachompa,hali iliyompelekea
kumkabidhi Mwalimu mkuu wa shule hiyo aliyemtaja kwa jina la Mlay,ambaye naye
alitishwa na mtuhumiwa.
Kutokana na vitisho hivyo Mwalimu
Mlay alilazimika kutoa taarifa polisi na mtuhumiwa kukamatwa na polisi wamesema
atafikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya taratibu kukamilika,huku mtoto
akiwa amekabidhiwa ndugu zake kwa uangalizi zaidi.
Akiongea kwa wasiwasi mtoto huyo
alisema ,hiyo ni mara ya tatu anapigwa na kuumizwa yeye na ndugu zake,na kuwa
mama yao aliachika kutokana na vipigo na mama yao mdogo ndiye anawachongea yeye
na ndugu zake watano ili wafukuzwe hapo.
Mmoja wa wanafunzi wa darasa la
tano jina tunalo alisema tabia ya kupiga si kwa watoto wake tu hana wanafunzi
darasani anawachapa bila utaratibu maalum,na walimu wanajua lakini wanaonekana
kumwogopa kuwa ni mkorofi.
Baadhi ya walimu wamesema matukio
ya kupiga watoto ni ya mara kwa mara lakini hilo ni kubwa zaidi nainapaswa
sheria ichukue mkondo wake.
Mganga wa zamu Hooka Paul alisema
majeraha hayo ni makubwa na anapaswa kupata kinga ya tetenasi kwa kuwa
amechelewa kupata matibabu,na kisaikolojia mtoto huyo ameathirika kwa kuwa anastuka
mara kwa mara.
Polisi wanaendelea na mahojiano
kwa walimu wengine na wamesema utaratibu ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Mwisho.