MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPA AKIWA NA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII KHAMISI KAGASHEKI,WENGINE NI MKURUGENZI WA TANAPA ALLAN KIJAZI
MKUU WA MKOA WA MARAJOHN TUPA,MKURUGENZI WA WANYAMA PORI TANZANIA PROFESA ALEXANDRE SONGORWA NA BAADHI YA WATU WALIOAMBATANA NA WAZIRI MKUU WA THAILAND UWANJA WA NDEGE SERONERA
CHAKULA HIKI KILITUMIKA KWA WAGENI WA THAILAND NA WATANZANIA HOTEL YA FOUR SESSION SAFARI LTD
WAZIRI KAGASHEKI,KIJAZI NA MMOJA WA WAGENI WALIOKUWEPO ZIARA YA SHINAWATRA
Utalii wamkuna Waziri Mkuu wa Thailand
Kwa ufupi
Alisema
kutokana na ziara hiyo, Tanzania na Thailand zimekubaliana na kutiliana saini
mkataba wa miaka mitatu wa ushirikiano katika kulinda, kuendeleza na kukomesha
biashara haramu ya wanyamapori.
Dar es
Salaam. Ziara ya siku tatu ya Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra
imemvutia kiongozi huyo na kuahidi kufanya ziara binafsi katika mbuga za
wanyama akiambatana na familia yake.
Akizungumza
wakati wa kumuaga waziri huyo aliyeondoka nchini jana, Waziri wa Maliasili na
Utalii, Balozi Khamisi Kagasheki, alisema ziara ya Shinawatra imekuwa ya
mafanikio makubwa kwa taifa.
Alisema
kiongozi huyo ameahidi kurudi nchini wakati wowote akipata nafasi.
“Amesema
anakwenda lakini atarudi katika ziara ya kibinafsi yeye na mume wake, mtoto
wake na ndugu zake na tumemwambia akiwa tayari atufahamishe,” alisema Balozo
Kagasheki.
Alisema
kutokana na ziara hiyo, Tanzania na Thailand zimekubaliana na kutiliana saini
mkataba wa miaka mitatu wa ushirikiano katika kulinda, kuendeleza na kukomesha
biashara haramu ya wanyamapori.
Mkataba
huo ulisainiwa na Balozi Kagasheki na Naibu Waziri Mkuu wa Thailand Plodprasop
Suraswad, aliyeambatana na Shinawatra.
Akizungumzia
manufaa ya mkataba huo, Waziri Kagasheki alisema utasaidia taifa kuongeza
mapato kupitia sekta ya maliasili kwa kuongeza watalii.