WALIMU WALALAMIKIWA KWA UBAGUZI WA UKABILA.
Serengeti:UBAGUZI wa kikabila,ukiukwaji wa Haki
za Binadamu unadaiwa kutawala zoezi la kuhamisha wafugaji katika kijiji cha
Nyamokhobiti kata ya Maji moto Tarafa ya
Ngoreme wilayani Serengeti,umevuka mipaka hadi shuleni .
Ubaguzi huo umeanza kuleta madhara kufuatia baadhi ya watoto
wa wafugaji wa jamii ya Wakenye kutoka wilaya ya Butiama waliokuwa wanasoma
Isereserekutokwenda shule kwa madai ya ubaguzi kutoka kwa walimu wa shule hiyo
ambao wengi ni kabila la Wangoreme wazawa wa kijiji hicho.
Alex Mang’era(68)mfugaji alisema aliingia kijijini hapo mwaka
2003 kwa kuridhiwa na serikali ya kijiji na mkutano mkuu,na wanae watatu
wanaosoma hapo kwa sasa hawaendi shule kutokana na ubaguzi ulio ndani ya jamii
na walimu wa shule.
“Wanangu Kadogo Alex wa darasa la 6,Neema na Habibu wa darasa
3 hawaendi shule…wanabaguliwa na wanafunzi,jamii nahadi walimu kuwa ni Wakenye
warudi kwao Butiama ….wamezaliwa na kuanzia shule hapa..mimi nimekaa miaka
10…nimepiga kura hapa…ubaguzi huu ni mbaya sana”alisema kwa masikitiko.
Alisema shule hiyo yenye walimu 7 watano ni wazawa wakijijini
hapo na wanaishi kwenye miji yao ,badala ya kutekeleza majukumu yao wamegeuka
kuwa sehemu ya jamii,wanashiriki vikao vya kimila ritongo na matokeo yake
wanapeleka ubaguzi shuleni.
Moroni Nyancharu(30)wa
kitongoji Getenga kijijini hapo anasema
katika zoezi hilo mtoto wake Bhoke Mroni
wa darasa la kwanza haendi shule kwa kuhofia usalama wake,na kubaguliwa .
”Walimu wanatutukana sisi kuwa Watoto wa Wakenye ni wajinga
hamjui kusoma…na wanafunzi nao wanatutukana kuwa sisi ni watu wa kuja…njiani
mkipita jamii inatuzomea kuwa Makenye mrudi wilayani kwenu…hatuna raha
shuleni”anasema mwanafunzi wa darasa la tatu jina tunalo.
Ofisa elimu akiri.
Ofisa elimu ufundi wilaya Christopher Mossi alikiri kuwa
walimu karibu wote ni wazawa wa kijijini hicho,”ni kweli ni hapo…kwa malalamiko
hayo tunafuatilia kwa kuwa yanalenga kuwanyima elimu hao watoto”alisema.
Mwenyekiti wa serikali
ya kijiji cha Iseresere Mosi Ng’ombe alipotakiwa kujibu tuhuma za kuwapokea
wafugaji na sasa amewakana,alisema yeye hawezi kulizungumzia hilo labda aulizwe
mkuu wa mkoa ama Dc.
Agizo la RC latekelezwa na wazee wa mila badala
yaSerikali ya kijiji.
Katika hali isiyo ya kawaida
ambayo imechangia ukiukwaji wa Haki za Binadamu agizo la Mkuu wa Mkoa wa
Mara John Tupa la kuhamisha wafugaji
haramu linatekelezwa na wazee wa mila chombo kisicho cha kiserikali.
Uamzi huo umelalamikiwa na makundi ya wanaharakati akiwemo
Mbunge wa jimbo hilo Dk,Stephen Kebwe ambaye aliiambia blog hii kuwa chombo hicho hushughulikiwa masuala ya
ulinzi na usalama ,lakini hakina nguvu kwa maagizo ya kiserikali kama hayo.
“Zoezi lilikuwa na nia njema lakini njia zilizotumika si
sahihi…huwezi tumia ritongo kwa agizo la serikali wakati inavyombo vyake…uonevu
,ukiukwaji haki utatendeka…pia kuna udhaifu katika zoezi hilo maana hakuna
waraka wenye maelekezo alioutoa kwa watekelezaji,hii inaweza kuleta
vurugu”alisema Mbunge.
Alikwenda mbali zaidi na kudai ameishamwambia mkuu wa mkoa
ajaribu kuangalia vema suala hilo kwa kuwa tafsri ya mhamiaji haramu
ijulikane,na wabainishwe na wananchi ,kwa kuwa watu walipokea kwa utaratibu
,wameishi miaka mingi,wanamazao,wana vitu kuwaondoa kwa kutumia ritongo
hawatapata muda wa kuweka sawa mali zao,wala kusikilizwa.
Wazee wa mila wafunga
zizi kwa dawa.
Mbali na malalamiko ya ubaguzi na ukiukwaji haki za
binadamu,wazee wa mila wamelazimika kufunga zizi la ng’ombe wa Simion Maitari
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Nyamokhobiti kijiji jilani kwa kuweka
matawi ya miti ambayo inaaminika kuwa wamezindika ng’ombe wakirudi humo
watakufa,na wao ndio wenye uwezo wa kuzindua tego hilo.
Majeruhi.
Wakati Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara Ferdinand Mtui na Mwenyekiti wa serikali ya
kijiji cha Iseresere Mosi Ng’ombe kudai kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa wakati wa
zoezi la kuwafukuza wafugaji,Mwananchi imebaini watu wawili kujeruhiwa kwa kupigwa na
kukatwa kwa sime.
Polisi kituo cha Maji moto kimekiri kuwapokea majeruhi hao na
kuwapa Pf 3 agosti 5 ,mwaka huu iliyosainiwa ditektivu Mohammed ambayo nakala
yake tumeiona ,pia hati ya kuwakamata watuhumiwa George Rabani na Mohi Morigo
kwa kosa kujeruhi Ref No MAJ/RB/281/2013 hata hivyo hawajakamatwa
Wanaharakati.
Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la Wasaidizi wa
Kisheria na Haki za Binadamu (Washehabise)Samwel Mewama anasema zoezi hilo
limekiuka haki za binadamu,kwa kuwa linavunja katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka
1977.
“Ibara ya 17,uhuru wa mtu kwenda atakako,sheria ya 1984 na ibara ya 24 haki ya kumiliki mali,kwa
kitendo hiki kilichofanyika ni uvunjaji wa katiba,watu wamekosa haki ,watoto
wanashida ya chakula,wameacha mazao,chombo kinachotumika kutekeleza si cha
kisheria,tutahakikisha haki inatendeka,maana mhamiaji haramu anawezaje kuchagua
kiongozi yeye akawa halali”anasema.
Rc
Mkuu wa mkoa wa Mara John Tupa anasema waraka wake amesambaza
kwa wakuu wa wilaya,na kuwa mwisho wa zoezi hilo ni agosti 16 mwaka huu,hata
hivyo waraka huo wakuu wa wilaya hawajausambaza kwa viongozi wa vijiji .
Mwisho.