MWENYEKITI
WA KITONGOJI ATUHUMIWA KUBAKA WATOTO WAWILI WA SHULE YA MSINGI,
Agosti
17,2013.
Serengeti;MWENYEKITI
wa kitongoji cha Matumaini kijiji cha Miseke kata ya Manchira wilayani
Serengeti Machaba Morumbe(53)(CCM)anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kubaka
watoto wawili wa shule ya msingi.
Matukio hayo
yanayodaiwa kutendeka kwa nyakati tofauti yamethibitishwa na polisi wilaya na
Shirika la wasaidizi wa kisheria na Haki za Binadamu(Washehabise)na uongozi wa
hospitali teule ya Nyerere ddh yanadaiwa kutokea agosti 9 na 13 katika
kitongoji hicho mwaka huu.
Akielezea matukio
hayo akiwa eneo la polisi Mwenyekiti wa
shirika hilo Samwel Mewama alisema ,tukio la kwanza linadaiwa kutokea agosti 9
majira ya saa 10 jioni,ambapo mtuhumiwa huyo anadaiwa kumbaka mwanafunzi wa
darasa la 5 mwenye umri wa miaka 12 shule ya msingi Zakhia Meghji kijijini hapo.
“Akiwa machungani
alimsihi mtoto huyo apeleke ng’ombe mtoni na kufika huko akambaka,huku
akimtishia kutosema…hakusema kabisa licha ya kuwa na maumivu makali…lakini
alipata ushujaa baada ya mwenzake kutendewa siku nyingine naye akawaeleza wazazi wake kuhusu unyama wa
kiongozi huyo”alisema Mewama.
Kujitokeza kwa mtoto
huyo alipokelewa na dawati la jinsia la polisi Mugumu na kufunguliwa jalada
Mug/dawati 148/2013 na kupelekwa hospitali teule ya Nyerere ddh kwa uchunguzi
zaidi.
Katika tukio la pili
mtuhumiwa huyo kwa mtindo ule ule anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la 3 mwenye umri wa miaka
10 Agosti 11 majira ya saa 11.00 jioni
mwaka huu wakati akichunga ng’ombe na mbuzi.
Mtoto huyo alisema
mtuhumiwa alimwambia eneo la mtoni kuna malisho mazuri ,walipofika ghafla
akamkamata na kumvua nguo na kuanza kumwingilia huku amemziba mdomo,na
kumsababishia majeraha sehemu za siri.
Baba mzazi wa mtoto
huyo jina tunalo alibaini hali hiyo baada ya kumwona mwanae akiwa katika hali
isiyo ya kawaida,na alipoulizwa alibainisha unyama aliotendewa na kiongozi huyo
na kuchunguza walibaini amechanika vibaya na kumpeleka hospitali kupitia polisi
na kufunguliwa jalada Mug/dawati 147/2013.
Mganga wa zamu
hospitalini hapo aliyejitambulisha kwa jina moja la Nyanokwe aliyempokea na kumfanyia uchunguzi
mtoto huyo amebaini kuchanika vibaya sehemu za siri na pia katika nyonga zake.
Mganga mkuu wa
hospitali teule ya Nyerere ddh,Dk,Kelvin Mwasha amethibitisha kumpokea mtoto
huyo kuwa wamemlaza wakiendelea na matibabu,hata hivyo mtuhumiwa ametoroka
kijijini baada ya kusikia anasakwa.
Mwisho.