Subscribe:

Ads 468x60px

TAMKO LA JUKWAA LA KATIBA

Kamati ya Utendaji
Tanzania Citizen’s Information Bureau (TCIB), Legal and Human Rights Centre (LHRC), The Leadership Forum, Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Tanzania
Media Women Association (TAMWA), Pemba Association of Civil Society Organization (PACSO), Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG), Youth Partnership Countrywide
(YPC), Association of Non Governmental Organization in Zanzibar (ANGOZA), Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP), Trade Union Congress of Tanzania (TUCTA),
Women Fighting AIDS in Tanzania (WOFATA), TGNP Mtandao
JUKWAA LA KATIBA TANZANIA
P. O. Box 78466, Plot No. 201 Block 46 Kijitonyama, Adjacent to
Kijitonyama UDSM Hostel Flats,
Dar Es Salaam, TANZANIA
Tel: +255 22 2773795 Fax: +255 22 2773764 Cell: 0783 993088
E-mail: jukwaa.katiba@gmail.com,info@jukwaalakatibatz.com Web
site: www.jukwaalakatibatz.com
APRILI 25, 2014
MCHAKATO WA KATIBA MPYA TANZANIA: TULIKOTOKA, TULIPO
NA TUENDAKO
TAMKO RASMI KUTOKANA NA TATHIMINI YA JUKWAA LA KATIBA
TANZANIA KUHUSU UNAOENDELEA WA KATIBA MPYA, 2010-2014
1.0. UTANGULIZI
Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) tukiwa wadau muhimu wa mchakato wa
Katiba Mpya hususani katika utoaji elimu na ufuatiliaji kwa ajili ya uandaaji
wa katiba mpya nchini Tanzania tumetafakari na kufanya tathmini ya kina ya
mchakato wa kuelekea katiba Mpya Tanzania tangu kuanza kwa mchakato
kupitia tamko la Mheshimiwa Rais la tarehe 31.12.2010 hadi leo ijumaa tarehe
25.4.2014 siku moja kabla ya tarehe ambayo katiba mpya ingekamilika rasmi,
kutiwa saini na kutangazwa rasmi, kama ilivyofikiriwa wakati wa kuanza kwa
Mchakato. Kwa kukumbushana tu, Katiba Mpya ya Tanzania ilipangwa
kuzinduliwa rasmi siku ya kesho sambamba na Maadhimisho ya miaka 50 ya
Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar! Kwa bahati mbaya, na kama
ushauri wetu wa kitaalam ulivyoelekeza mapema mwaka 2011, mwenendo wa
Mchakato wa Katiba umepelekea kuibuka kwa matukio kadhaa katikati ya
safari na kufanya kukamilika kwa Mchakato ndani ya kipindi kilichoazimiwa
Kamati ya Utendaji
Tanzania Citizen’s Information Bureau (TCIB), Legal and Human Rights Centre (LHRC), The Leadership Forum, Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Tanzania
Media Women Association (TAMWA), Pemba Association of Civil Society Organization (PACSO), Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG), Youth Partnership Countrywide
(YPC), Association of Non Governmental Organization in Zanzibar (ANGOZA), Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP), Trade Union Congress of Tanzania (TUCTA),
Women Fighting AIDS in Tanzania (WOFATA), TGNP Mtandao
mwanzoni kushindikana. Ukweli ni kwamba tunaingia siku ya kesho tukiwa sio
tu hatuna Katiba bali pia mchakato wa Katiba ukiwa uko njia panda kama
tutakavyofafanua katika tamko hili.
2.0. HATUA MCHAKATO AMBAZO MCHAKATO WA KATIBA
UMEPITIA TANGU KUANZA KWAKE TAREHE 31 DISEMBA 2010:
NA TAREHE TUKIO MHUSIKA
1 31 Disemba
2010
Kutangazwa kuanza kwa
mchakato wa Katiba Mpya
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete
2 Januari –
Februari 2011
Mabishano juu ya endapo
Mchakato huu ni wa Kuandika
Katiba Mpya au kurekebisha
Katiba ya JMT, 1977
Wanasiasa, Wananchi,
AZAKI, Vyombo vya
Habari
3 Februari 2011 Muswada Mfano wa kwanza
waandaliwa chini ya uongozi
wa AZAKI na kukabidhiwa
serikalini kutoa mwongozo kwa
matayarisho ya Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba
JUKWAA LA KATIBA
TANZANIA, Ofisi ya
Mwandishi Mkuu wa
Miswada ya Sheria
serikalini, AG Chambers
4 8 Machi 2011 Muswada wa Kwanza wa sheria
ya mabadiliko ya katiba kwa
Kiingereza
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete, Baraza la
Mawaziri, Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Wizara ya
Katiba na Sheria,
mashirika ya Kiraia na
Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
5 Juni, 2011 Bunge Kuukataa Muswada wa
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba
kwa kuwa ulikuwa katika
kiwango duni na pia ulikuwa
katika lugha ya Kiingereza
BUNGE LA
TANZANIA
6 Novemba 2011 Baadhi ya Wabunge wa kambi Kambi rasmi ya
Kamati ya Utendaji
Tanzania Citizen’s Information Bureau (TCIB), Legal and Human Rights Centre (LHRC), The Leadership Forum, Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Tanzania
Media Women Association (TAMWA), Pemba Association of Civil Society Organization (PACSO), Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG), Youth Partnership Countrywide
(YPC), Association of Non Governmental Organization in Zanzibar (ANGOZA), Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP), Trade Union Congress of Tanzania (TUCTA),
Women Fighting AIDS in Tanzania (WOFATA), TGNP Mtandao
rasmi ya upinzani kutoka nje ya
Bunge wakilalamikia uburuzaji
katika mjadala wa Muswada wa
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba
Upinzani Bungeni
7 30 Novemba
2011
Kurejeshwa kwa Muswada
Bungeni, kujadiliwa na
Kupitishwa na Bunge la
Tanzania kwa Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba Na. 8 ya
2011
BUNGE LA
TANZANIA
8 Disemba –
Januari 2012
Mazungumzo ya kuleta
muafaka na maelewano kati ya
Mheshimiwa Rais na vyama
mbalimbali vya Siasa, asasi za
Kidini na makundi ya Kiraia,
Ikulu, Dar es Salaam
Mheshimiwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania
9 April – Mei,
2012
Uteuzi na kuanza rasmi kwa
kazi ya Tume ya Mabadiliko ya
Katiba
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete, Bunge la
Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na
wananchi kupitia
mashirika ya kiraia
10 Novemba, 2013 Tume yaomba na kuongezewa
muda wa kukamilisha kazi yake
kwa miezi miwili zaidi
Tume ya Mabadiliko ya
Katiba
11 6 Februari 2014 Kuchapishwa kwa toleo jipya la
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba
linalounganisha matoleo yote ya
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba
tangu Novemba (2011),
Februari (2012), Juni (2013) na
Oktoba, (2013) na kuzaa sheria
moja kwa mujibu wa Sheria ya
Urekebu Sheria.
Mwanasheria Mkuu wa
Serikali
12 Machi 19, 2014 Kuvunjwa rasmi kwa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba
Tume ya Mabadiliko ya
Katiba
Kamati ya Utendaji
Tanzania Citizen’s Information Bureau (TCIB), Legal and Human Rights Centre (LHRC), The Leadership Forum, Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Tanzania
Media Women Association (TAMWA), Pemba Association of Civil Society Organization (PACSO), Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG), Youth Partnership Countrywide
(YPC), Association of Non Governmental Organization in Zanzibar (ANGOZA), Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP), Trade Union Congress of Tanzania (TUCTA),
Women Fighting AIDS in Tanzania (WOFATA), TGNP Mtandao
13 18 Februri 2014 Uteuzi wa wajumbe wa Bunge
Maalum la Katiba na kuanza
kazi rasmi kwa Bunge Maalum
la Katiba
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete, Bunge la
Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Baraza la
Wawakilishi Zanzibar na
mashirika ya kiraia
14 18 Februari –
20 Machi 2014
Mjadala wa Kanuni za Bunge
Maalum la Katiba ndani ya
Bunge na Kupitia Kamati ya
Kanuni
Sekretarieti ya Bunge la
Jamhuri ya Muungano
na Baraza la
Wawakilishi, Kamati ya
Kanuni ya Bunge
Maalum la Katiba
15 28 April 2014 Bunge Maalum la Katiba
kusitishwa kwa muda kupisha
Bunge la Bajeti na kwenda
kujipanga vizuri zaidi
Bunge Maalum la Katiba
16 18 Machi 2014 Uwasilishaji rasmi wa Rasimu
ya Katiba Bungeni
Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba,
Jaji Joseph Sinde
Warioba
17 Machi, 2014 Uzinduzi rasmi wa Bunge
Maalum la Katiba
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete
18 April, 2014 Mjadala wa Sura ya Kwanza na
ya Sita katika mtindo wa
Kamati na Bunge zima
Kamati za Bunge
Maalum la Katiba,
Bunge Maalum la Katiba
19 28 April 2014 BUNGE MAALUM
KUSITISHWA hadi Agosti
2014 kupisha Bunge la Bajeti
Bunge Maalum la Katiba
3.0. YATOKANAYO NA TATHMINI
3.1. SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA NI CHANGAMOTO
NA CHANZO CHA MATATIZO YOTE YA MCHAKATO!
Kamati ya Utendaji
Tanzania Citizen’s Information Bureau (TCIB), Legal and Human Rights Centre (LHRC), The Leadership Forum, Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Tanzania
Media Women Association (TAMWA), Pemba Association of Civil Society Organization (PACSO), Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG), Youth Partnership Countrywide
(YPC), Association of Non Governmental Organization in Zanzibar (ANGOZA), Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP), Trade Union Congress of Tanzania (TUCTA),
Women Fighting AIDS in Tanzania (WOFATA), TGNP Mtandao
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba sura ya 83 ya mwaka 2012 ndiyo chanzo cha
matatizo na mkwamo wa Mchakato wa kuandika katiba mpya nchini Tanzania kwa
namna tatu :-
3.1.1 Watunga sheria wenyewe yaani wabunge wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ambao ni wanufaika au waathirika wa
matokeo ya mchakato wa kuandika katiba mpya walijiweka
ndani ya Bunge Maalum la Katiba ili kulinda maslahi yao ya
baadaye. Bunge pia lina mamlaka ya kutenga bajeti ya
uendeshaji wa mchakato ikiwemo posho zao kama wabunge wa
Bunge Maalum la Katiba. Kumekuwa na mgongano mkubwa
wa kimaslahi kuhusu wabunge na Mchakato wa Katiba Mpya.
3.1.2 Kuingia moja kwa moja kwa Wabunge wote wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wajumbe wote wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika Bunge Maalum la
Katiba kumeleta utata na ugumu mkubwa katika mchakato wa
Bunge Maalum la Katiba. Kwanza, mivutano ya kivyama ndani
ya Bunge Maalum la Katiba inatokana na mazoea ya mivutano
ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Baraza la Wawakilishi Zanibar kati ya vyama vikuu vya
upinzani na Chama tawala. Pili, kuna mgongano wa moja kwa
moja wa kimaslahi kuhusu wanasiasa na maslahi yao ya kivyeo
na kimapato. Tatu, hata utata kidogo ukijitokeza kuhusu Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba kutakuwa kahuna uwezekano wa
kuutatua kisheria mpaka kusitishwa kwa Bunge Maalum na
kuitishwa kwa mabunge ya kawaida. Hii yote inaleta shida !
3.1.3 Sheria ya Mabadiliko ya Katiba sura ya 83 ya Sheria za
Tanzania imempa Rais madaraka makubwa sana katika hatua
zote sita za mchakato wa Katiba Mpya, yeye ana sauti na
mamlaka makubwa sana ya kufanya maamuzi kuanzia
kutangaza kuanza/kusitishwa kwa mchakato, kutungwa na
kurekebishwa kwa sheria, uteuzi, uendeshaji na uvunjaji wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Uteuzi wa wajumbe wa Bunge
Maalum la Katiba, uzinduzi, uendeshaji na uvunjaji wa Bunge
Kamati ya Utendaji
Tanzania Citizen’s Information Bureau (TCIB), Legal and Human Rights Centre (LHRC), The Leadership Forum, Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Tanzania
Media Women Association (TAMWA), Pemba Association of Civil Society Organization (PACSO), Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG), Youth Partnership Countrywide
(YPC), Association of Non Governmental Organization in Zanzibar (ANGOZA), Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP), Trade Union Congress of Tanzania (TUCTA),
Women Fighting AIDS in Tanzania (WOFATA), TGNP Mtandao
Maalum la Katiba na usimamizi wa mchakato mzima wa
Katiba.
3.2. KUKOSEKANA KWA UTASHI WA KWELIKWELI NA NIA
YA KISIASA YA KUPATA KATIBA MPYA
3.2.1 Pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete kuonesha nia njema ya kuanzisha
mchakato wa kuandika katiba Mpya hapa Tanzania, nia hiyo
haionekani kuwa ndani ya serikali ya Chama cha Mapinduzi
kwa ujumla wake. Kwa vitendo na maneno ya watendaji
waandamizi wa serikali ya Tanzania, JUKWAA LA
KATIBA TANZANIA tunachelea kuamini kuwa ipo nia ya
dhati na ya kweli ya kuhakikisha kuwa nchi yetu inapata
Katiba Mpya inayotokana na maoni ya Watanzania
wenyewe. Kwa mwelekeo wa mijadala ya hivi karibuni
ndani na nje ya Bunge Maalum la Katiba pamoja na
serikalini, nia ya watawala inaonekana kuwa ni kutaka
kufanya mabadiliko madogo madogo katika Katiba ya sasa
kama ilivyo sera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
kuacha kila kitu kama kilivyo. Kwa mtazamo wetu, hiyo
inapingana na nia na kiu ya watanzania kuona kuwa
Mchakato wa Kuandika Katiba Mpya unaleta mapinduzi ya
Kikatiba yatakayokuwa chachu ya nchi yetu kuongozwa kwa
misingi ya uwazi, uhuru, demokrasia na kuheshimu utu wa
mtu na haki za binadamu.
3.2.2 Mapungufu katika sheria inayoongoza Mchakato huu ni
makubwa kiasi kwamba utata wa mchakato mzima ni wa
Kisheria. Kwa mfano, Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilivyo
sasa inashindwa kutoa mwelekeo thabiti wa nini cha kufanya
inapofikia hali ya sintofahamu na mkanganyiko wa
mchakato kama ilivyo sasa. Mianya hiyo ya Kisheria
imepelekea utata katika utungaji Kanuni za Bunge Maalum
la Katiba hadi kuleta mkanganyiko na kufanya Bunge
kutofikia muafaka katika maeneo kadhaa ikiwemo aina ya
Kamati ya Utendaji
Tanzania Citizen’s Information Bureau (TCIB), Legal and Human Rights Centre (LHRC), The Leadership Forum, Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Tanzania
Media Women Association (TAMWA), Pemba Association of Civil Society Organization (PACSO), Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG), Youth Partnership Countrywide
(YPC), Association of Non Governmental Organization in Zanzibar (ANGOZA), Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP), Trade Union Congress of Tanzania (TUCTA),
Women Fighting AIDS in Tanzania (WOFATA), TGNP Mtandao
kura katika kupitisha vifungu vya rasimu, idadi inayohitajika
katika kupitisha jambo ndani ya Bunge Maalum pamoja na
mambo mengine kadhaa. Hata malalamiko yaliyopo hivi
sasa juu ya baadhi ya makundi kutokuwa na uwakilishi
ndani ya Bunge Maalum la Katiba ni suala lenye mizizi yake
kaika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Suala hii limeleta
hisia kuwa liliwekwa hivyo makusudi kisheria ili CCM iwe
na wajumbe wengi kuliko makundi mengine ndani ya Bunge
Maalum la Katiba na hivyo kupitisha vifungu vya Katiba
kwa urahisi bila kuhitaji maridhiano na pande zenye mawazo
tofauti.
3.2.3 Imekuwa ni dhahiri pia kuwa kunakosekana utashi na
uelewa juu ya namna ambavyo Bunge Maalum la Katiba
huendesha shughuli za uptishaji Masharti ya rasimu ya
Katiba. Kwa mfano, ingawa upitishaji vifungu kwa kura sio
mtindo wa kidemokrasia wa upitishaji masharti ya Katiba,
tumeshuhudia viongozi wakitia msisitizo wa matumizi ya
kura kwenye kufikia maamuzi ya Bunge Maalum la Katiba.
Kwa maoni yetu, upitishaji wa Katiba unahitaji kutokana na
maridhiano, makubaliano, muafaka na sio tu KURA.
3.3. UFUNGUZI, MJADALA NA KUONDOKA KWA UKAWA
NDANI YA BUNGE MAALUM LA KATIBA
3.3.1 Tumetathmini pia jinsi Bunge Maalum la Katiba lilivyoanza.
Kwa mtazamo wetu, Ufunguzi wa bunge maalum la katiba
ulifanyika vibaya kinyume na matarajio ya walio wengi nchini
tena kwa kupindisha na kuvunja Kanuni na Sheria. Kwa mujibu
wa Kanuni za BungeMaalum la Katiba, hotuba ya Rais ya
ufunguzi wa Bunge Maalum ulipaswa kufanywa kabla ya
uwasilishaji rasmi wa Rasimu ya Katiba Mpya. Ilishangaza sana
kuwa rasimu iliwasilishwa kabla ya ufunguzi rasmi wa Bunge
Maalum ambayo ilizidi kuchochea kuligawa zaidi Bunge
kivyama, kimisimamo na kiitikadi. Mjadala tangu Bunge
Maalum la Katiba kuanza ulikuwa hauna afya njema kwani
Bunge lilijaa kuzomeana, maslahi ya vyama, maslahi ya
Kamati ya Utendaji
Tanzania Citizen’s Information Bureau (TCIB), Legal and Human Rights Centre (LHRC), The Leadership Forum, Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Tanzania
Media Women Association (TAMWA), Pemba Association of Civil Society Organization (PACSO), Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG), Youth Partnership Countrywide
(YPC), Association of Non Governmental Organization in Zanzibar (ANGOZA), Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP), Trade Union Congress of Tanzania (TUCTA),
Women Fighting AIDS in Tanzania (WOFATA), TGNP Mtandao
vikundi, kura ya siri na wazi, wingi, uchache, matusi, kejeli,
uchochezi, kashfa na ubabe. Bunge lilikosa kabisa maridhiano,
muafaka, kuvumiliana na kuzingatia maslahi ya Taifa.
3.3.2 Kitendo cha wajumbe wa UKAWA kutoka nje ya Bunge
Maalum la Katiba ni pigo kubwa kwa mchakato wa kuandika
katiba mpya kwani wameondoka Bungeni makundi yote mawili
yakiwa na majeraha ya kutukanana na kukashifiana sana ndani
ya Bunge. Kundi lililobaki linaloongozwa na Tanzania Kwanza
haliwezi kamwe kuendelea na mchakato wa katiba peke yake
kwani litapata uhalali wa kisheria ila halitapata uhalali wa
kisiasa ambao ni muhimu sana kuhalalisha mchakato mzima.
Aidha, ni makosa makubwa sana kwa Bunge Maalum kuingia
katika zoezi muhimu la kubadili Kanuni wakati zaidi ya
wabunge 190 wakiwa wamesusia vikao vya Bunge Maalum la
Katiba na wako nje ya Bunge !
3.3.3 Kitendo cha kumbeza Mwenyekiti na kazi iliyofanywa na Tume
ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Sinde
Warioba ambako kuliongozwa na Rais, Mawaziri pamoja na
wajumbe wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiongozwa
na kundi la Tanzania Kwanza bungeni kimezidi kuligawa
Bunge Maalum la Katiba kati ya wanaounga mkono Rasimu na
wale wanaopinga Rasimu. Kitendo hiki pia kimeligawa taifa
kwa mtindo huo huo. Wito wetu ni kwamba lazima kumbeza
Warioba kuishe na tujikite kama taifa kujadili Maudhui ya
Rasimu ya Katiba badala ya kuendeleza malumbano.
3.3.4 Kwa tathimini ya JUKATA, nje ya Bunge pia kumekuwa na
mgawanyiko mkubwa kati ya wanaounga mkono Rasimu kama
ilivyo na wale wanaopinga Rasimu kwa mtazamo wa Muundo
wa Muungano. Aidha, Mgawanyiko huo unazidi kuchochewa na
wanasiasa kinyume cha misingi ya uandishi wa Katiba Mpya
ambao huhitaji maridhiano zaidi badala ya mivutano.
4.0. KAZI ILIYOKO HUKO TUENDAKO
Kamati ya Utendaji
Tanzania Citizen’s Information Bureau (TCIB), Legal and Human Rights Centre (LHRC), The Leadership Forum, Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Tanzania
Media Women Association (TAMWA), Pemba Association of Civil Society Organization (PACSO), Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG), Youth Partnership Countrywide
(YPC), Association of Non Governmental Organization in Zanzibar (ANGOZA), Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP), Trade Union Congress of Tanzania (TUCTA),
Women Fighting AIDS in Tanzania (WOFATA), TGNP Mtandao
4.1.1 Kama Taifa, tukubali kwamba sote tangu awali tulikosea kwa
namna moja au nyingine, kwa waliokuwa Bungeni na nje ya
bunge. Tunawaomba viongozi wa dini watuongoze kufanya
toba ya Taifa. Hii itatusaidia kutibu majeraha yaliyotokea kwa
kipindi chote cha mchakato.
4.1.2 Kutokana na utaratibu wa kufunga tovuti ya Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, JUKATA tumechukua baadhi ya
majukumu yaliyokuwa ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa
kutundika nyaraka zote za Tume kwenye tovuti ya JUKATA
anwani www.jukwaalakatibatz.com . Pia, nakala halisi za
Rasimu na Randama zinapatikana ofisi za JUKATA iliyopo
Mwenge Karibu na Hospitali ya Mama Ngoma mkabala na
zilizokuwa hosteli za Kijitonyama za wanachuo wa Chuo Kikuu
cha Dar es salaam. Tumefanya yote haya kizalendo ili
kuwawezesha wananchi kuendelea kupata nyaraka hizi muhimu
kwa ustawi na uendelevu wa Taifa letu kwa miaka 50 hadi 100
ijayo.
4.1.3 Pia, tukubali kuwa tunayo Rasimu ya katiba ambayo imetokana
na maoni ya watanzania na hivyo ipo haja ya kuiheshimu. Pia,
ni wajibu wa Bunge Maalum kuijadili na kuinyoosha
panapohitajika lakini bila kuishambulia na kuwashambulia
wajumbe wa TUME iliyoratibu utayarishaji wake kana kwamba
walitunga kutoka vichwani mwao. Hatuna budi tusahihishe
makosa yetu kwenye mchakato wa katiba na hasa kwa
kurekebisha sheria ya mabadiliko katiba ili kuweka sawa
mambo yenye utata yahusuyo elimu ya uraia, demokrasia ya
mijadala na mamlaka ya wananchi katika mchakato huu wa
Katiba ili yakae sawa. Aidha, fedheha ya matusi, vijembe,
mipasho, kebehi na dharau inayoendelea ndani ya Bunge
Maalum la Katiba na miongoni mwa wanasiasa nje ya Bunge
lazima ifike Mwisho na Bunge Maalum lijifunze kuendeshwa
kwa hoja na mijadala tulivu badala ya fujo na kuzomeana.
4.1.4 Kwa kuwa tunaendelea kuishi kama taifa, ni vema tufanye
mabadiliko madogo (Minimum Reforms) kwenye katiba yetu
Kamati ya Utendaji
Tanzania Citizen’s Information Bureau (TCIB), Legal and Human Rights Centre (LHRC), The Leadership Forum, Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Tanzania
Media Women Association (TAMWA), Pemba Association of Civil Society Organization (PACSO), Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG), Youth Partnership Countrywide
(YPC), Association of Non Governmental Organization in Zanzibar (ANGOZA), Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP), Trade Union Congress of Tanzania (TUCTA),
Women Fighting AIDS in Tanzania (WOFATA), TGNP Mtandao
iliyopo ili kukidhi mahitaji yetu ya sasa turekebishe Tume yaya
Taifa uchaguzi (Muundo na Uteuzi wake), tuingize wagombea
binafsi, Sheria ya uchaguzi (Serikali za mitaa na uchaguzi
mkuu) zibadilishwe.
5.0 Mwisho, Mchakato wa Katiba umefikia njia panda. Kwa kukerwa na
hilo, pamoja na fedha nyingi ambazo nchi yetu imekwishatumia, Jukwaa la
Katiba Tanzania (JUKATA) tunajitolea kuratibu maridhiano miongoni mwa
makundi ya kisiasa ya nini kifanyike na tunafikiria kuwaalika watu wawili
mashuhuri na wenye heshima kubwa hapa Afrika Mashariki, barani Afrika na
duniani kote ili wasaidie kusimamia unasuaji wa Mchakato huu wa Katiba
Mpya kwa kukutanisha pande MUHIMU za Mchakato wa Katiba (kuanzia
Vyama vya Siasa, Asasi za Wananchi na Taasisi zote muhimu zilizoguswa na
Mchakato huu hadi sasa). Tumemwalika Mheshimiwa Jaji Mkuu Mstaafu wa
Tanzania Ndugu Barnabas Samatta kuwa Mwenyekiti wa Jopo hili la usuluhishi
na Ndugu Patrice L.O.Lumumba (PLO) kutoka Kenya kuwa Msuluhishi
Mwenza katika jambo hili muhimu kwa uhai wa Taifa letu. Tulipofika hatuwezi
kutoka bila juhudi madhubuti za kusikiliza na kusuluhisha pande muhimu za
Mchakato wa Katiba. Tusipokuwa na usuluhishi, Mchakato wa Katiba Mpya
utakwama kabisa !
Taifa ni kubwa kuliko vyama na makundi ya kisiasa. Vyama vitakufa na
kupotea lakini Taifa litadumu milele.
MUNGU IBARIKI TANZANIA!
Deus M.Kibamba
Mwenyekiti
25 Aprili 2014

0 comments:

Post a Comment