Subscribe:

Ads 468x60px

KULALIA JAMVI KWA MFANYA ACHOME GODORO LA JILANI YAKE NA KUMUUNGUZA MTOTO


 
 MTOTO KELVIN MARWA WA MIAKA MIWILI AMELAZWA KTK HOSPITALI TEULE YA NYERERE WILAYA YA SERENGETI   AKIWA NA MAMA YAKE JACKLINE ANAYEMUUGUZA MAJERAHA YA KUCHOMWA MOTO NA JILANI YAO KUTOKANA NA WIVU WA KULALIA GODORO WAKATI YEYE ANALALIA JAMVI

Serengeti:
WIVU wa kukosa godoro  umempelekea mwanamke  mmoja wa mtaa wa uwanja wa mbuzi mjini Mugumu wilayani Serengeti kuchoma godoro la jilani yake  na kumuunguza vibaya mtoto wakati amelala.
Tukio hilo la aina yake limethibitishwa na polisi wilayani hapa  na kumtaja mtuhumiwa kuwa ni Esther Juma  linadaiwa kutokea  oktoba 30 majira ya saa 1:00 asubuhi ambapo mtoto huyo aliyetajwa kwa jina la Kelvin Marwa(2)ameungua sehemu mbalimbali za mwili na amelazwa hospitali ya wilaya kwa matibabu.
Akisimulia mkasa huo mama mzazi wa mtoto huyo akiwa hospitalini  Jackiline Godfrey(20)alisema wamekuwa na ugomvi na mtuhumiwa ambaye ni jilani yake baada ya kuwa amenunua godoro na yeye analalia jamvi,na  siku hiyo akaamua kuchoma godoro na kumuunguza mwanae.
“Nilitoka saa 12:00 alfajiri kuwahi kibaruani stendi kwenye mgahawa ninakofanya kazi…nikaacha mwanangu amelala…hurudi mapema kumwandalia chai ama uji…nikiwa kazini majira ya saa 1:00 asubuhi  nilifuatwa na mtoto wa jilani..akasema Kelvin ameungulia ndani---niliishiwa nguvughafla…kwenda nikakuta majilani wamebomoa mlango na mtoto ameungua vibaya”alisema huku akifuta machozi.
Alisema mbali na mtoto kuungua pia nguo na vitu vingine viliungua  vyote kutokana na unyama huo uliofanywa na jilani yake ambaye amekuwa akimwapia kumkomesha kwa yeye kununua godoro na kumwacha yeye akilalia jamvi.
Baadhi ya mashuhuda walisema walimwona mtuhumiwa akitoka ndani ya chumba kilichoungua akikimbia ,ghafla wakaona moshi na sauti ya  mtoto  ikisikika akilia kwa sauti kali ,katika kufuatilia wakabaini mtoto anaungua wakabomoa mlango na kumnusuru mtoto huyo.
“Kilichomsadia mtoto baada ya kuanza kuungua alijivuta hadi kwenye kona na kuacha godoro linaungua….kwa kweli ni unyama mkubwa sana aliokuwa anaufanya huyo mwanamke….kulalia jamvi kunampelekea kutaka kumuua huyo mtoto…kwa kweli kama polisi wasingewahi angeuawa”alisema shuhuda.
Balozi wa nyumba 10 eneo hilo Janet Samwel alisema baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa alianza kupigwa na kama si polisi kufika eneo hilo mapema huenda angeuawa kwa kuwa wananchi walikuwa na hasira kali dhidi ya ukatili huo.
Mratibu wa dawati la jinsia la polisi wilaya WP 5665 D/S Sijali Nyambuche alisema walilazimika kufika haraka eneo la tukio baada ya kupata taarifa za tukio ,wakabaini kuwa huenda kukatokea maafa kwa mtuhumiwa kutokana na mazingira ya tukio na hasira za wananchi.
“Kama tusingewahi ingekuwa mbaya zaidi…tulimnusuru mtuhumiwa na tunamshikilia ..taratibu zikikamilika atafikishwa mahakamani wakati wowote”alisema.
Muuguzi wa zamu wodi ya watoto Mwangwa Samson alisema mtoto huyo ameungua makalio,miguu na sehemu za siri kwa asilimia 30 na kuwa hawezi kukaa kutokana na majeraha aliyopata,na juhudi za madaktari na waganga zinaendelea kuhakikisha anapona.
Mwisho.


 BAADHI YA VITU VILIVYOBAKI KATIKA CHUMBA WALICHOKUWA WANAISHI

MAJAMBAZI YA MIFUGO YAJERUHI WAWILI KWA RISASI.

Serengeti:
WATU wawili wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Serengeti baada ya kupigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa wezi wa mifugo wakati wanafuatilia nyayo.

Mganga mwandamizi katika hospitali hiyo Dk.Tanu Waryoba amewataja majeruhi hao kuwa ni Chacha Megera(39)na Marwa Nyakimwi(21) wote wakazi wa kijiji cha Nyahende wilayani hapa.

Amesema Megera alipigwa risasi mguu wa kushoto na Nyakimwi kwenye nyonga mguu wa kulia na kutokea paja la mguu wa kushoto,na kuwa wanaendelea vizuri baada ya kupata matibabu .

Megera akiwa kitanda namba 12 wodi ya wanaume alikolazwa alisema oktoba 28 majira kati ya saa 4-5 usiku mwaka huu kulitokea wizi wa ng’ombe 9 nyumbani kwao wakati wamelala.

“Mke wa kaka yangu Kibibi Ntare alipotoka nje kujisaidia alibaini wizi huo…alipiga yowe kwa kushirikiana na wanakijiji tukaanza kufuatilia nyayo tukiwa tunakimbia…kufika eneo la mto Nyahende …tukishangaa ghafla nikapigwa risasi mguu wa kushoto”alisema.

Alisema alishindwa kuendelea na safari hiyo kutokana na maumivu makali na kulazimika kurudishwa nyumbani na kupelekwa hospitali kwa matibabu.

“Mimi nilipigwa risasi kwenye saa 6 usiku nikiwa miongoni mwa vijana wenzangu tuliokuwa mstari wa mbele…tukiwa tunakwenda kwa kasi baada ya kuwepo ishara kuwa wezi hawako mbali…ghafla nilipigwa risasi upande wa kulia wa nyonga na kutokea kushoto…niliishiwa nguvu na kulala chini”alisema Marwa Nyakimwi.

Nyakimwi aliyelazwa kitanda namba 8 alisema ilibidi akimbizwe hospitali,huku wenzake wakisonga mbele na kufanikiwa kurudisha ng’ombe wote 9 na kukamata watuhumiwa watatu kati ya sita waliohusika na tukio hilo.

Hata hivyo polisi walifanikiwa kuwaokoa watuhumiwa watatu waliokamatwa na mmoja aliyetajwa kwa jina la Mwita Malitwa(40)amelazwa hospitali ya wilaya chini ya ulinzi wa polisi.

Polisi wanasema wanaendelea na mahojiano na baadhi ya watuhumiwa na inasemekana watuhumiwa waliofanikiwa kutoroka walikimbilia maeneo ya Gibaso wilayani Tarime.

Kuhusu bunduki iliyohusika walisema ni ya kivita kwa kuwa risasi zake zilibainika ni za SMG ambazo zinatumiwa na bunduki aina ya SRA pia.
Mwisho.
Chacha Megera mmoja wa majeruhi akiwa hospitali ya wilaya ya Serengeti akiuguza majeraha ya risasi aliyopigwa wakati wakifuatilia wezi wa ng'ombe

KANISA KATOLIKI LAZINDUKA



ILI kukabiliana na changamoto za kidunia  zinazochangia kuporomoka kwa Imani ,maadili na ukiukwaji wa utawala bora kwa waumini na viongozi  kanisa  Katoliki hapa nchini limeanza kujitathimini na kuweka mikakati mipya.
Akitoa semina wakati wa ibada ya misa kwa waumini wa kanisa katoliki Parokia ya Mugumu katibu wa baraza la maketikisa jimbo la Musoma Antony Marwa alisema hatua hiyo ya haraka imetokana na tafiti zilizofanywa na wataalam wa kanisa na kukabidhi baraza la maaskofu Tanzania.
Alisema licha ya waumini kuongezeka ndani ya kanisa katoliki imani inazidi kushuka kwa kuwa hawajengwi kwa misingi mizuri na wanayumbishwa na changamoto nyingi za kidunia ikiwemo suala la madhehebu mengine.
“Kanisa limeruhusu dunia kuingia ndani na kuporomosha imani za waumini…watu wanaingia kanisani wamevaa nguo zisizo na staha …waumini hawasemi,viongozi wa kanisa wako kimya…lakini waumini wakiulizwa wanasema kanisa linaruhusu….wapi kanisa limeruhusu uchafu kama huo?”alihoji.
Alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa watakao ingia kanisa na vimini,wanaume wamevaa mregezo na heleni wafukuzwe kabla ya kuingia,na kwa wanaotoa komnio wasiwape kwa kuwa hawana sifa stahiki.
“Suala la ulevi kuna watu wanasema kanisa linaruhusu…wapi imeandikwa kwenye biblia kuwa wamewaruhusu kulewa…muwe watu wa kiasi….haya si maadili mema kwa viongozi wa kanisa na waumini lazima mageuzi yafanyike ili kujenga imani ya waumini”alisema na kushangiliwa na kanisa zima.
Akizungumzia suala la utawala bora kanisani alielezea kuwa viongozi wanaochanguliwa na waumini kuongoza baraza la walei wanatakiwa kuwa wawazi kwa kutoa taarifa za mapato na matumizi kwa waumini,ikiwemo vyanzo vyao na jinsi fedha wanazochanga zinavyofanya kazi.
“Kila wakati harambee harambee kanisani  hawasemi zinazochangwa zinafanya nini…kanisa linakwenda bila bajeti,fedha zinakusanywa kila wiki zinaishia mifukoni benki haziendi…wekeni bajeti za kuhudumia nyumba za mapadri na watawa na huduma za kiroho zinazobaki zipelekwe benki”alisema.
Katekista huyo alisema kukosekana kwa mipango kwenye makanisa kumepelekea elimu ya dini haifundishwi kwa kuwa walimu wa dini hawalipwi,wanaishi maisha magumu huku fedha zikitumiwa vibaya na imani ikiporomoka makanisani.
“Maktekista hawathaminiwi wakati ndio wanafundisha waumini wakabatizwa na kupata kipaimara…shukrani wanachangia mapadri na maaskofu waliofundisha hawapati kitu…wamekata tamaa ndiyo maana hawafundishi..wanaingiza waumini wengi wakabatizwa lakini wasiokuwa na misingi ya imani maana hawana mafunzo…wanawafanya walimu wa dini kama kibao cha matofali kikimaliza kazi hutupwa”alisisitiza.
Alisema maazimio hayo yanayotokana na semina ya wiki nzima iliyoshirikisha majimbo yote Tanzania ilifanyikia Kurasini Dar es Salaam yanatakiwa kufanyiwa kazi ili ujumbe wa Papa  mstaafu Benedict wa 16 wa kutangaza mwaka 2013 na 14 kuwa wa imani uweze kutimia.
Mwisho.

TAZAMA ILIVYOVEMA NA YA KUPENDEZA NDUGU KUKAA NA KULA KWA PAMOJA

 Ni siku njema kwa wazazi wanapowatembelea watoto shuleni,hupata nafasi ya kupitia kazi zake wapi ana kwenda vibaya ama vizuri na kushauriana na walimu,nami nilitimiza wajibu huo pale nilipomtembelea kamanda wangu Wilbroad Thibhoki Pre primary School.
 Wazazi hula pamoja na watoto wao huku wakizungumza na kuwatia moyo kama inavyoonekana hapo.


  Kamanda Wilbroad ambaye yuko Pre form one akipata maziwa kujenga afya,aliyesimama mwenye nguo nyeusi ni mdogo wake ,na aliyekaa kulia kwa mdogo wake ambao niliambatana nao.
  Kamanda Wilbroad ambaye yuko Pre form one akipata maziwa kujenga afya,aliyesimama mwenye nguo nyeusi ni mdogo wake ,na aliyekaa kulia kwa mdogo wake wakibadilishana mawazo juuya mambo ya shule.
mambo yanaendelea;

MSHITAKIWA WA MAUAJI AIDUWAZA MAHAKAMA ,AIBUKA NA KUDAI ALIUA APATE UTAJIRI.



Oktoba 26,201
KATIKA hali isiyo ya kawaida Mshitakiwa wa mauaji ya dreva bodaboda Gwitembe Yagera (68)mbele ya Hakimu wa mahakama ya wilaya ya Serengeti aliibuka na kudai kuwa yeye ndiye aliua lakini kwa kudanganywa na Sangoma kuwa akipeleka damu ya mtu atakuwa atatajirika.
Mshitakiwa huyo Suguta Turuka(19)mkazi wa kijiji cha Kenokwe wilayani hapa licha ya kuambiwa hatakiwi kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi za mauaji aliibuka na kudai kuwa ameyatenda hayo kutokana na kudanganywa na mshitakiwa mwenzake.
“Mheshimiwa hakimu nilifanya mauaji hayo mwenyewe baada ya kudanganywa na mshitakiwa mwenzangu ambaye ni mganga wa kienyeji…nilimuua Gwitembe muda mfupi baada ya kutoka kupiga ramli na kuambiwa  kama nataka kuwa tajiri nilete damu ya mtu yeyote…nikaamua kumkodi kisha nikamuua”alisema mshitakiwa na kuifanya mahakama kubaki katika mshangao mkubwa.
“Mganga alinipa masharti mbalimbali ikiwemo kuua na pia kupeleka maziwa ya ng’ombe yenye cream na kuchemshwa pamoja na mafuta ya kasuku .…vikawekwa ndani ya kopo…akasema nisifungue na kuwa nitakuta fedha nyingi siku ya kufungua….na kuwa nikikamatwa nisimtaje..hata hivyo sikupata kitu zaidi ya kuua na kukamatwa”alisema.
Mapema Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Franco Kiswaga mwendesha mashitaka wa polisi Paskael Nkenyenge aliiambia mahakama hiyo kuwa Suguta na Marsha Severino(43)ambaye ni Sangoma anayeishi Mugumu mjini wanashitakiwa kwa kosa la mauaji ya dreva boda boda Gwitembe Yagera(68).
Akisoma maelezo ya shauri la mauaji namba 27/2013 alisema washitakiwa walitenda kosa hilo oktoba 3 majira ya saa 9:00 arasili mwaka huu mpakani mwa kijiji cha Nyichoka na Kenokwe eneo lenye vichaka vingi ambapo kuna kuna mto Nyamburu ,ambapo mshitakiwa Turuka alifanya mauaji hayo ikiwa ni muda mfupi ametoka kupiga ramli kwa Severino.
Na kuwa mshitakiwa wa kwanza Suguta alimkodi marehemu Gwitembe aliyekuwa anaendesha pikipiki aina ya Toyo yenye namba za usajili T608 CKJ kwa lengo la kumpeleka nyumbani kwao Kwitete,lakini baada ya kufika eneo hilo alimtaka asimame wajadiliane,ghafla alichomoa kisu na kumchoma sehemu ya kifua upande wa kulia na kuanguka huku yeye akikimbia na kuacha kisu kikining’inia.
Hakimu Kiswaga aliamru washitakiwa warudishwe mahabusu hadi novemba 7 mwaka huu kesi hiyi itakapotajwa tena.
Mwisho.


DAKTARI MMOJA HUTIBU WAGONJWA 25,000



ASKOFU AMOSI MUHAGACHI MWENYE TAI NYEKUNDU NA MGANGA MFAWIDHI WA NYERERE HOSPITALI TEULE YA WILAYA YA SERENGETI WAKATI WA KIKAO CHA MWISHO CHA BODI ,AMBAPO WALIJADILI NAMNA YA KUKABILIANA TATIZO LA UPUNGUFU WA MADAKTARI

Oktoba 25,2013.
Serengeti:Hospitali  Teule ya  wilaya ya  Serengeti inakabiliwa na upungufu wa kada ya udaktari na utabibu kwa asilimia 43.9,hatua ambayo inapelekea daktari mmoja kuhudumia wagonjwa 25,000 badala ya 1,500.
Hospitali hiyo inayomilikiwa na kanisa la Menonite Tanzania na huendeshwa kwa ubia na serikali inahudumia wakazi wa wilaya hiyo 360,000 na kutoka wilaya zingine za mkoa huo.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dk,Calvin Mwasha aliliambia Mwananchi kuwa wanahitaji madaktari 11 lakini wapo 4,madaktari wasaidizi wanahitajika 7 lakini yupo 1na watabibu wapo 11 badala ya 13.
“Upungufu huo ni mkubwa unawalazimu madaktari waliopo kufanya kazi zaidi ya uwezo wao….kisheria daktari anatakiwa kuhudumia wagonjwa 1,500 lakini anahudumia wagonjwa 25,000 na wanatumia masaa mengi “alisema.
Kwa upande wa uuguzi alisema hospitali hiyo inahitaji afisa muuguzi(General)14 lakini wapo 4,wauguzi wasaidizi (specialist)wanahitajika 9 lakini hakuna hata mmoja,na kada hiyo wana upungufu wa watalaam kwa asilimia 74.7
Aidha alisema kuna upungufu kwenye chumba cha maiti ,huku kitengo cha Kinywa na meno wakiwa na upungufu wa wataalam kwa asilimia 25 ili kukidhi Ikama.
“Kada ya Madawa kuna upungufu wa wataalam wa madawa(Pharmacy)ni asilimia 66.6 hasa eneo la Mteknolojia…maabara kuna upungufu asilimia 11.1,uzoezaji viungo hakuna afisa tiba kwa vitendo …kuna upungufu asilimia 75…kwa kada ya afisa afya kuna upungufu wa asilimia 100”alibainisha Mwasha.
Kwa upande wake katibu wa hospitali hiyo Dk.Musuto Chirangi alisema ili kupunguza upungufu huo wanafuatilia vibali vya ajira wizarani ili waweze kuajiri wataalam wanaohitajika,”pia tunaanza kozi ya uganga ngazi ya diploma katika chuo chetu cha Kisare mwaka 2014.”alisema.
Hata hivyo ilibainika kuwa wataalam wengi wanaacha kazi na kuajiriwa na serikalini kwa madai kuwa,ajira chini ya kanisa haina maslahi mazuri,watumishi hawapati safari ama semina kama ilivyo kwenye halmashauri na serikali kuu.
Mwisho. 

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA BODA BODA ADAI ALIPEWA MASHARTI NA SANGOMA WAKE.

 PICHA ZA MATUKIO SIKU AMBAYO MAUAJI YA BODA BODA
 KISU KINACHODAIWA KILITUMIKA KUMUUA BODA BODA
MAITI IKIWASILI HOSPITALI YA WILAYA SERENGETI


 MTUHUMIWA WA MAUAJI YA BODA BODA ANASWA NA KUDAI ALIPEWA SHARTI NA SANGOMA .
Oktoba 25,2013
MTU mmoja anayetuhumiwa kuhusika na mauaji ya aliyekuwa boda boda mjini Mugumu Wilayani Serengeti Gwitembe Yagera(60)amekamatwa na kudai kuwa aliambiwa na Sangoma wake aue mtu yeyote ili apate utajiri.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara Fernandi Mtui alithibitisha kukamatwa kwa Mtuhumiwa huyo anayeshikiliwa na polisi wilayani Serengeti Elias Jonathan(23)mkazi wa kijiji cha Burunga kata ya Uwanja wa Ndege wilayani hapa,amekamatwa hivi karibuni eneo la Sirari na kuwa uchunguzi zaidi unaendelea .
Habari kutoka ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa mtuhumiwa huyo alisema kuwa alitekeleza mauaji hayo kutokana na masharti ya mganga wake ambaye anasakwa na jeshi la polisi,kuwa afanye mauaji pekee yake na kwa mtu yeyote ndipo na atapata  utajiri.
“Alisema aliamua kumkodi huyo boda boda kwa kuangalia umri wake kwa madai kuwa anakwenda Mosongo…kufika eneo la Nyisense Nyichoka akamchoma kisu na kusababisha mauaji yake na kukimbia akitelekeza kisu hapo na hakuchukua kitu chochote”kilisema chanzo cha uhakika kutoka ndani ya jeshi la polisi.
Kuhusu kukamatwa kwake  chanzo hicho kilisema baada ya kutenda unyama huo alitoroka hadi Sirari na ambako alihusika katika mauaji ya baiskeli na kukamatwa ,na baba yake alitoa ushirikiano baada ya kujua kuwa anatafutwa kwa mauaji na kunaswa na kuletwa Mugumu kuhusiana na tuhuma hizo.
Oktoba 4,mwaka huu majira ya saa 8 arasili mtuhumiwa huyo anadaiwa alimkodi Yagera kwa sharti kuwa wakifika kijijini Mosongo angemlipa fedha yake,lakini kabla ya kufika inadaiwa alimchoma kisu eneo la kushoto chini ya ubavu na kusababisha kifo chake.
Na baada ya kutenda unyama huo hakuchukua kitu na kutokea na maiti yake iligunduliwa na wapiti njia ambao walitumia simu ya marehemu kuwataarifu viongozi wa chama cha waendesha pikipiki wilayani hapo,na askari polisi.
Habari tulizozipata wakati tunaandaa taarifa hizi zinadai kuwa mtuhumiwa huyo amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Serengeti kuhusiana na tuhuma hizo,hata hivyo hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji.
Mwisho.

MTOTO ALIYEZALIWA UTUMBO UKIWA NJE APELEKWA BUGANDO




 MTOTO ALIYEZALIWA UTUMBO UKIWA NJE AKIWA CHINI YA UANGALIZI WA WAUGUZI NYERERE HOSPITALI WILAYANI SERENGETI KABLA YA KUPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA YA MWANZA


MTOTO ALIYEZALIWA UTUMBO NJE APELEKWA BUGANDO
Oktoba 22,2013.
Serengeti:HOSPITALI Teule ya Nyerere wilayani Serengeti imetoa rufaa ya mtoto  aliyezaliwa katika kijiji cha Nyichoka wilaya ya Serengeti utumbo ukiwa nje kwenda hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya matibabu zaidi.
Mtoto huyo wa kike  alizaliwa oktoba 20 mwaka huu utumbo ukiwa nje hali iliyowachanganya wazazi wake Edward Mgabo(25)na Hadija Rajabu(21) kutokana na hali aliyokuwa nayo,lakini akiwa mwenye afya njema.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dk,Calvin Mwasha amesema wamelazimika kutoa rufaa kwenda Bugando kwa kuwa hawana madaktari bingwa wa matatizo kama hayo,na hali aliyonayo anahitaji huduma za haraka ili kunusuru maisha yake.
“Matatizo kama haya hutokana na ukuaji…miezi mitatu ya mimba …viungo hutengenezwa ,hapo ndipo hutokea mambo kama hayo….ni mambo ambayo hutokea kitaalam yanajulikana na ndiyo maana kuna wanaoyashughulikia”alisema.
Alisema inapotokea inahitaji huduma za haraka sana ikiwa ni pamoja na upasuaji mara moja ili kudhibiti mambo yanayoweza kuchangia kupata maambukizi mengine.
Akisimulia tukio hilo baba wa mtoto huyo Mgabo alisema,”tukiwa tunaenda zahanati ya Nyichoka mke wangu alizidiwa na kujifungulia njiani…tulisaidiwa na watu wakamfunga kitovu mtoto …lakini utumbo ukaonekana uko nje,tukaambiwa tuwahi zahanati Muuguzi naye akasema hana uwezo twende wilayani”alisema.
Alibainisha walipofika kila mmoja anaonekana kushangaa na kusema hilo tatizo wanatakiwa kwenda Bugando”huyu ni mtoto wangu wa kwanza kwa mwanamke huyu ambaye nilimkuta na mtoto mwingine…tunapambana kupata fedha ili kuokoa maisha ya mtoto wetu “alisema kwa masikitiko.
Mama mzazi wa mtoto Hadija alisema wakati wa ujauzito hapakuwa na tatizo lolote ,na hata wakati anajifungulia njiani hapakuwa na shida kwa kuwa mtoto alikuwa mzima ,lakini alishangaa kuona utumbo uko nje na akawa amekata tamaa kama ataweza kuishi.
Muuguzi wodi la wajawazito Anjelina Biseko alisema kuwa watoto kama hao wanapofikishwa Bugando huwekwa kwenye mifuko maalum kwa muda wa miezi mitatu kisha hufanyiwa upasuaji ili kurudisha hali yake ya kawaida
Muuguzi mkuu wa hospitali hiyo Neema Mechara alisema kwa mwaka huu hilo ni tukio la kwanza kutokea,lakini kumewahi kutokea tukio kama hilo kwa mtoto kuzaliwa viungo vya ndani vikiwa nje,na wengine maumbile ya ajabu ajabu.
Mwisho.  

MTOTO AZALIWA UTUMBO UKIWA NJE

 MTOTO WA KIKE AMEZALIWA UTUMBO UKIWA NJE KIJIJI CHA NYICHOKA WILAYANI SERENGETI
 WAUGUZI HOSPITALI TEULE YA NYERERE WILAYANI SERENGETI WAKIMUANDAA MTOTO HUYO KWA AJILI YA KUMPELEKA HOSPITALI YA BUGANDO KWA MATIBABU.
 SAMWEL LUNGANG'A MKAZI WA KIJIJI CHA MBALIBALI WILAYANI SERENGETI AKIPELEKWA WODI YA WANAUME HOSPITALI YA WILAYA KWA AJILI MATIBABU KUFUATIA KUKATWA KATWA WAKATI WAKIWA KWENYE HARUSI KIJIJINI HAPO.
 LUNGANG'A AKIVULIWA KOTI LAKE KWA AJILI YA KUPATA MATIBABU
HAPO AMELAZWA KWA AJILI YA MATIBABU

WANANCHI WAUA WATATU KWA TUHUMA ZA WIZI-BUTIAMA


WATATU WAUAWA NA WANANCHI KWA KUWATUHUMU KUHUSIKA NA WIZI-MARA

Oktoba 11,2013
WAKAZI wa Bukima wilaya ya Butiama mkoani Mara wamewaua watu watatu  kwa kuwakata kwa mapanga,kuwapiga mawe sehemu mbalimbali za mwili baada ya kuwatuhumu kuhusika na jaribio la wizi  katika kijiji cha Kwitare  kata ta Makojo.
Tukio hilo limetokea oktoba 8 majira ya saa 12:00 alfajiri kijijini hapo limethibitishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Mara,mkuu wa wilaya hiyo na uongozi wa kijiji.
Waliouawa ni Masola Magesa Magoti(40)mkazi wa Bukima ,Sagaya Mussa Sagaya(30)mkazi wa kijiji cha Bugoji wilaya ya Butiama, ambaye inadaiwa alikuwa mwizi sugu na alikuwa chini ya uangalizi wa polisi kutokana na kuhusika katika unyang’anyi wa kutumia silaha,na Chikaka Chikaka(32)mkazi wa kijiji Tegeruka.
Mkuu wa wilaya hiyo Anjelina Mabula amesema kutokana na kukithiri kwa matukio ya wizi na mauaji amesema itapigwa kura ya siri kijijini hapo kubaini watu wanaijihusisha na wizi,mauaji na wanaowahifadhi ili hatua ziweze kuchukuliwa.
Amesema sambamba na upigaji kura za siri pia kutakuwa na madaftari ya wakazi wa kila kitongoji ,kujua wageni wanaoingia,na kuwa kukitokea uhalifu viongozi wa eneo hilo watashughulikiwa.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wamesema kuwa uamzi huo ni matokeo ya kukosa imani na polisi kwa kuwa watuhumiwa wakifikishwa kituoni huachiwa na matukio yanazidi,hivyo njia pekee ya kukomesha uhalifu ni kuwaua.

Maelezo hayo yamepingwa na kaimu mkuu wa polisi wilaya ya Butiama Abubakari Kunga kuwa wananchi wanapotakiwa kwenda kutoa ushahidi hawaendi na matokeo yake watuhumiwa huachiwa.

Kauli ya wananchi kukoma imani na vyombo vya serikali yamesemwa pia na Dc wa Tarime John Henjewelle kuwa wanapoitwa kuchukua majeruhi polisi husema hawana mafuta,lakini muda huo huo wakiambiwa kuna magendo mafuta hupatikana.

Hali hiyo pia inajitokeza kwa askari wa taasisi za uhifadhi tembo wanapovamia mashamba na makazi ya watu,hudai hawana magari,risasi ama mafuta ,lakini wakiambiwa kuna jangili magari humiminika eneo hilo kwa muda mfupi. 

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Fernandi Mtui amewataka wananchi kutojichukuliwa sheria mikononi kwa kuwa ni kosa,badala yake wawapeleke watuhumiwa polisi na watoe ushirikiano wanapohitaji,hata hivyo hakuna mtu anashikiliwa kutokana na tukio hilo.
Mwisho.

TEMBO AVAMIA KIJIJI NA KUUAA NG'OMBE MMOJA


TEMBO WAVAMIA KIJIJI NA KUUA NG’OMBE

Oktoba 7,2013

HOFU imetanda kwa wakazi wa kijiji cha Makundusi kata ya Natta wilayani Serengeti kufuatia kundi kubwa la tembo kuvamia kijijini na kusababisha kifo cha ng’ombe na uharibifu wa mazao.

Tukio hilo limethibitishwa na uongozi wa kijiji na ofisi ya wanyama pori wilaya kuwa limetokea oktoba 3 majira ya saa 8 arasili mwaka huu katika eneo la Makundusi ambapo inadaiwa tembo hao wamepiga kambi kwa zaidi ya siku mbili.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Juma Porini alisema kuwa siku ya tukio tembo  kati 30-40 waliokuwa wamepiga kambi jilani na kijiji hicho walivamia kundi la ng’ombe na kuchanga nyika wakati wanachunga.

“Wachungaji wakakimbia ..ng’ombe nao wakaanza kukimbia,lakini kuna tembo mmoja ambaye amekatika mkia ambaye inadaiwa mwaka jana na mwaka huu ameua ng’ombe alianza kufukuza ng’ombe na kufanikiwa kumnasa mmoja kwa mkonga”alisema.

Alisema kuwa baada ya kumnasa alimbamiza kwenye mti kisha akaanza kumkanyaga na 
kumtoboa toboa hadi akafa,kisha akaanza kutafuta wengine lakini wakawa wamekimbia.


“Mara baada ya mauaji hayo wakaondoka na kukaa jilani na mpaka wa kijiji..jioni wanarudi kijijini na kuharibu mazao,kwa ujumla wananchi walikuwa wamejitahidi kulima mahindi lakini kwa hali ilivyo hawataambua kitu,maana wanyama hawa wameamua kupiga kambi kabisa”alisema.

Alisema walilazimika kutoa taarifa ofisi ya wanyama pori wilaya ambao walisema hawana gari,na kuomba msaada kwa hifadhi ya Jamii(WMA)ambao nao hawakufika,hata kampuni ya Singita Grumeti Reserves hawakufika kwa wakati.

Na kuwa hata walipofika walidai hawana risasi hali inayotia shaka utendaji wake,kwa kuwa halmashauri ilipewa gari na kampuni ya Singita Grumeti Reserves kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la tembo,pia kila mwaka wanalipwa sh.mil.200 na kampuni hiyo,ambazo hazijasaidia idara zaidi ya madiwani kulipana posho za vikao.

Mjumbe wa serikali ya kijiji hicho Peter Magari alisema wananchi wana hofu kubwa ya kupoteza maisha kwa kuwa mbinu walizokuwa wanatumia kufukuza tembo sasa hazina maana kwa kuwa tembo wanaonekana wamezizoea.

“Tumekuwa tukitumia tochi kubwa kwa kukusanyana na mwanga unakuwa mkali huku tunapiga kelele,tembo wanakimbia …lakini kwa sasa badala ya kukimbia wanatufukuza hii inaonyesha wazi wameishazoea …kama hali ni hivyo inatishia usalama wetu”alisema.

Alisema tembo huyo mwaka 2012 aliua ng’ombe wawili mali ya Charles Machera na Mwanzoni mwa mwaka huu ameua ng’ombe mmoja na tukio hilo ni tatu anafanya madhara hayo.

Kaimu afisa wanyamapori wilaya Cathbert Boma alikiri kupata taarifa na kuwa hawakuwa na gari na kudai kuwa wameishaweka utaratibu kwa askari wa idara hiyo walioko Grumeti wanatakiwa kutaarifiwa.

“Tatizo la tembo kuvamia maeneo ya vijiji linazidi kuongezeka kwa kuwa wanapokuwa wanawindwa ndani hukimbilia nje…kwa hiyo tatizo hili linasumbua sana maeneo mbalimbali “alisema.

Hivi karibu Tembo alivunja uzio na kumuua Faru aitwaye Limpopo aliyekuwa amehifadhiwa katika eneo la Kijiji hicho na kampuni ya Singita Grumeti Reserves.
Mwisho.

DIWANI APIGWA


DIWANI APIGWA NA MTOTO WA KAKA YAKE KWA SABABU ZA KISIASA
Na  Blog
Oktoba 7,2013
Serengeti:DIWANI wa kata ya Majimoto  wilayani Serengeti Mkoa wa Mara Rashidi Mugare(CCM)amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili ,baada ya kupigwa na mtoto wa kaka yake kufuatia ugomvi unaodaiwa kuwa wa kisiasa wakati wanakunywa pombe.
Tukio hilo limetokea oktoba 5 ,majira ya usiku mwaka huu limethibitishwa na polisi wilayani  hapa ambao wanamshikilia mtuhumiwa Makuri Chacha(36)kutokana na tuhuma za kumpiga diwani  na kumjeruhi sehemu za pua na mdomo.
Akiongea kwa njia ya simu na Blog hii kwa njia ya simu  diwani huyo amekiri kushambuliwa na kuwa hali yake kwa sasa si nzuri na anatarajia kwenda hospitali ya Mkoa Musoma kwa ajili matibabu,huku akishindwa kubainisha chanzo cha ugomvi huo.
“Huyo ni mtoto wa kama yangu ninayemfuata…alinishambulia vibaya sana na kuniumiza …huyo amewahi kumpiga mke wangu wakati wa uchaguzi wa 2010 akamuumiza…tukakaa kama familia tuakayamaliza…ana kisa na mimi kwa masuala ya kisiasa maana wao wako CUF”alisema.
Alipotakiwa kuelezea chanzo ni nini akisita sita ,kisha akasema”kuna mwenyekiti mmoja wa Cuf amekataliwa na wananchi wao wanahisi mimi nilihusika kumng’oa …ndipo siku hiyo nilipowakuta baa kukatokea mgogoro kisha wakaanza kunishambulia kwa maneno …hatimaye akanivaa na kunipiga “alisema.
Mmoja wa viongozi wa serikali ya kijiji jina limehifadhiwa alisema kisa ni diwani kwa kushirikiana na ofisa mtendaji wa kata kufanya mapinduzi ya nafasi ya Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Nyamokhobiti Gidion Maitari(CUF)kwa madai kuwa anawashitaki wananchi walioshiriki zoezi la kuhamisha mifugo yake na kumsababishia hasara kwa mingine kufa,na kupotea.
“Baada ya kufanikisha mapinduzi hayo diwani na timu yake walikutana baa wakaanza kusherehekea kuwa wamefaulu…mwenyekiti akakata rufaa kwa Ded na Dc na kupewa tuhuma akazijibu…kwa majibu hayo timu yake nayo ilikutana na kuanza kujipongeza kama walivyofanya diwani na wenzake…ndipo diwani akaingia kwenye kikao kisichomhusu “alisema.
Shuhuda huyo alisema kitendo cha diwani kuingia baa waliyokuwa wanakunywa kundi lisilo lake kuliibua mzozo na kutupiana maneno kwa misingi ya kambi,ndipo mtuhumiwa akamsukuma diwani ambaye alikuwa amelewa akaangukia pua na kuumia.
“Vurugu zilikuwa kubwa kwa kuwa kaka ya diwani John Mantage alimpiga na tofali Bwire Masisi ambaye aliwahi kugombea udiwani kwa tiketi ya Chadema kwa misingi kuwa anashabikia mwenyekiti wa CUF…kwa kuwa hao ni ndugu ugomvi ukawa mkubwa ukahama kwenye koo ukawa wa mlengo wa kisiasa Cuf na CCM “alibainisha.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi mtendaji wanatarajiwa kufika kijiji cha Nyamokhobiti oktoba 8 kujiridhisha na hatua zilizotumika kumkataa mwenyekiti kama ni za kisheria au ni kikundi cha watu wachache.
Mwisho.

DREVA BODA AUAWA KWA KUCHOMWA KISU NA ABIRIA WAKE


 madreva boda boda wa mji wa Mugumu wilayani Serengeti wakitoka kijiji cha Nyichoka wilayani humo ,eneo ambalo dreva boda boda Gwitembe Yagera aliuawa na mtu aliyekuwa amemkodi

 Kisu kinachodaiwa kutumika kumchoma na kusababisha kifo cha Gwitembe Yagera(62)dreva boda boda mkazi wa kijiji cha Kisangura
Boda boda wakiwa katika eneo la hospitali teule ya Nyerere ddh 
Gwitembe Yagera dreva wa boda boda aliyeuawa kwa kuchomwa kisu na abiria aliyemkodi