DIWANI APIGWA NA MTOTO WA KAKA YAKE KWA SABABU ZA KISIASA
Na Blog
Oktoba 7,2013
Serengeti:DIWANI wa kata ya Majimoto wilayani Serengeti Mkoa wa Mara Rashidi
Mugare(CCM)amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili ,baada ya kupigwa na mtoto wa
kaka yake kufuatia ugomvi unaodaiwa kuwa wa kisiasa wakati wanakunywa pombe.
Tukio hilo limetokea oktoba 5
,majira ya usiku mwaka huu limethibitishwa na polisi wilayani hapa ambao wanamshikilia mtuhumiwa Makuri
Chacha(36)kutokana na tuhuma za kumpiga diwani na kumjeruhi sehemu za pua na mdomo.
Akiongea kwa njia ya simu na Blog
hii kwa njia ya simu diwani huyo amekiri
kushambuliwa na kuwa hali yake kwa sasa si nzuri na anatarajia kwenda hospitali
ya Mkoa Musoma kwa ajili matibabu,huku akishindwa kubainisha chanzo cha ugomvi
huo.
“Huyo ni mtoto wa kama yangu
ninayemfuata…alinishambulia vibaya sana na kuniumiza …huyo amewahi kumpiga mke
wangu wakati wa uchaguzi wa 2010 akamuumiza…tukakaa kama familia
tuakayamaliza…ana kisa na mimi kwa masuala ya kisiasa maana wao wako
CUF”alisema.
Alipotakiwa kuelezea chanzo ni
nini akisita sita ,kisha akasema”kuna mwenyekiti mmoja wa Cuf amekataliwa na
wananchi wao wanahisi mimi nilihusika kumng’oa …ndipo siku hiyo nilipowakuta
baa kukatokea mgogoro kisha wakaanza kunishambulia kwa maneno …hatimaye
akanivaa na kunipiga “alisema.
Mmoja wa viongozi wa serikali ya
kijiji jina limehifadhiwa alisema kisa ni diwani kwa kushirikiana na ofisa
mtendaji wa kata kufanya mapinduzi ya nafasi ya Mwenyekiti wa serikali ya
kijiji cha Nyamokhobiti Gidion Maitari(CUF)kwa madai kuwa anawashitaki wananchi
walioshiriki zoezi la kuhamisha mifugo yake na kumsababishia hasara kwa mingine
kufa,na kupotea.
“Baada ya kufanikisha mapinduzi
hayo diwani na timu yake walikutana baa wakaanza kusherehekea kuwa
wamefaulu…mwenyekiti akakata rufaa kwa Ded na Dc na kupewa tuhuma akazijibu…kwa
majibu hayo timu yake nayo ilikutana na kuanza kujipongeza kama walivyofanya
diwani na wenzake…ndipo diwani akaingia kwenye kikao kisichomhusu “alisema.
Shuhuda huyo alisema kitendo cha
diwani kuingia baa waliyokuwa wanakunywa kundi lisilo lake kuliibua mzozo na
kutupiana maneno kwa misingi ya kambi,ndipo mtuhumiwa akamsukuma diwani ambaye
alikuwa amelewa akaangukia pua na kuumia.
“Vurugu zilikuwa kubwa kwa kuwa
kaka ya diwani John Mantage alimpiga na tofali Bwire Masisi ambaye aliwahi
kugombea udiwani kwa tiketi ya Chadema kwa misingi kuwa anashabikia mwenyekiti
wa CUF…kwa kuwa hao ni ndugu ugomvi ukawa mkubwa ukahama kwenye koo ukawa wa
mlengo wa kisiasa Cuf na CCM “alibainisha.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya na
Mkurugenzi mtendaji wanatarajiwa kufika kijiji cha Nyamokhobiti oktoba 8 kujiridhisha
na hatua zilizotumika kumkataa mwenyekiti kama ni za kisheria au ni kikundi cha
watu wachache.
Mwisho.