WENYEVITI WAKATAA POSHO YA
SENSA TSH,15,000=,
“Makarani wahofu kukabidhi madodoso mpaka walipwe,
Na Anthony Mayunga-Mara.
Septemba 5,2012.
WAKATI zoezi la Sensa
likiongezewa siku hadi tarehe 8,viongozi wa vitongoji wilayani Tarime wamekataa
kupokea malipo ya tsh,15,000 kwa siku
zote za kazi hiyo.
Hali hiyo inatokana na
kutofautiana kwa Malipo hayo kwa kila wilaya ndani ya mkoa mmoja ,licha ya wote
kudai waraka kutoka ofisi ya mkoa.
Baadhi ya wenyeviti wa
vitongoji wilayani humo ambao hawakupenda kutaja majina yao waliliambia gazeti hili kuwa hawako
tayari kulipwa kiasi hicho kwa kazi hiyo waliyoifanya.
“Tumezoea kutumiwa kama watu
tusiokuwa na majukumu ya kifamilia,toka utekelezaji wa miradi hadi sensa,yaani
unalipwa tshs 15,kwa siku 7 wastani wa
tsh,2,000= kwa siku ambazo hazitoshi hata mlo wa mchana,hii ni dharau kubwa
sana”alisema mmoja wao.
Walidai kuwa walilazimika
kuacha shughuli za kilimo na kushinda wakizunguka na makarani ambao walikuwa
wakipwa tsh,35,000= kwa siku, na kuwa wameamua kuziacha ili serikali ifaidike.
“Wengine kwa kazi hizi hizi
walilipwa tsh,50,000= wilayani Serengeti,Bunda tunasikia walilipwa tsh,20,000=
sisi tsh,15,000= mkoa huo huo kuna kitu kinaendelea maana hata fedha ya
uhamasishaji watu wamekula sisi ndio tulifanya kazi ya hamasa na kushawishi
wananchi”walisema .
Walisema hata posho kwa mwezi
wenyeviti wa vijiji kwa wilaya hiyo wanalipwa tsh,5,000= kwa mwezi licha ya
kuwa wanakabiliwa na kazi nyingi za kuhamasisha maendeleo.
Mratibu wa sensa wilaya hiyo
aliyejitambulisha kwa jina moja la Juma alikiri wenyeviti kukataa fedha hizo
kwa madai kuwa ni kidogo.
“Ni kweli wamekataa
tunaendelea kushughulikia ili waweze kuchukua kwa kuwa hawakuwemo kwenye
hesabu,waliokuwa wanatajwa ni wenyeviti wa mitaa,watendaji wa vijiji na kata ,hivyo
sisi hatuna mitaa tukawaingiza wenyeviti”alisema.
Alisema kuwa katika utafiti
wake alibaini kuwa wilaya hiyo inalipa kiasi kikubwa ikilinganisha na Rorya na
Serengeti ,hata hivyo wilaya ya Serengeti walilipa tsh,50,000 kama
ilivyokuwa imeelekezwa awali,lakini mkoa ukabadilisha viwango.
Kwa wilaya ya Rorya wenyeviti
wa vitongoji walilipwa tsh,10,000= kama mkoa
ulivyoelekzwa,hata hivyo hawakushiriki zoezi hali iliyopelekea makarani
kuzunguka wenyewe.
Katibu tawala mkoa wa Mara
Clement Lujaji akizungumzia suala la malipo ya wenyeviti wa vitongoji alisema
waraka ulisambazwa kwa waratibu wote kutokana na kuwa hawakuwemo kwenye
mchakato na kuwa halmashauri zilikuwa na nafasi ya kuwalipa zaidi ya hapo
kulingana na mapato yao.
Blogu hii imebaini kuwa baadhi
ya makarani hawakuweza kuendelea na zoezi la sensa licha ya kuongeza siku kwa
kile kinachodaiwa kuwa maelekezo hayo hayafafanuliwi jinsi watakavyolipwa.
Na kuwa walilipwa nusu ya
posho na hawajalipwa nusu iliyosalia ,hata madodoso hata waliokamilisja hawajakabidhi kwa kuwa
hawajalipwa,na wanahofu kukabidhi bila kulipwa fedha zao hali .
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment