WANAHARAKATI WATAKIWA
KUANDAMANA KUPINGA MAUAJI NYAMONGO.
Na Anthony Mayunga-Nyamongo.
Septemba 11,2012.
SIKU moja tu baada ya polisi
kujeruhi watu 6 kwa mabomu ya machozi wakiwa majumbani kwaoWanaharakati na
mashirika ya kiraia wilayani Tarime
wameombwa kufanya maandamano ya hiari
kupinga mauaji na vitendo vya kikatili vinavyofanywa na askari polisi
wanaolinda mgodi wa African Barrick Gold North Mara.
Wito huo wakati waandishi wa
habari hapa Tanzania wakiandamana kimya kimya kulaani mauaji ya kikatili ya
aliyekuwa mwandishi wa habari wa Channel ten mjini Iringa katika kijiji cha
Nyololo na raia wasiokuwa na hatia yanayofanywa na polisi.
Mtafiti kutoka Kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu(LHRC)Onesmo Ole ngurumwa akiongea na gazeti hili alisema
zaidi ya watu 30 wameuawa na jeshi la polisi katika mgodi wa African Barrick
North Mara kwa kipindi cha kuanzia 2009-sasa.
“Matukio hayakomi kila wakati
wananchi wanauawa ,inabidi wanaharakati na mashirika ya kiraia mkoani Mara
kuunganisha nguvu na kufanya maandamano ya amani ili kupinga mauaji na ukatili
wanaofanyiwa wananchi hao ambao hawajawekewa mazingira mazuri”alisema.
Ole ngurumwa ambaye ni
mfuatiliaji wa karibu wa mauaji yanayotokea Nyamongo alisema kwa kipindi cha
mwaka 2009 watu 21waliuliwa na polisi
ama na walinzi wa mgodi huo.
Na kuwa mauaji yanaongezeka
kila mwaka hivyo inatakiwa wanaharakati na mashirika ya kiraia kujitokeza ili
kupinga ukatili huo.
“Kabla hawajauza ama
kukodisha mgodi huo vitendo hivyo vinatakiwa kukomeshwa kwa kuwa ikiachwa
watawarithisha wawekezaji wengine,tulaani vitendo hivyo”alisema.
Akizungumzia ulipuaji wa
mabomu hadi kwenye makazi ya watu alisema ni utendaji mbovu wa jeshi hilo kwa
kuwa hali hiyo ikiachwa iendelee madhara yanazidi kuwa makubwa.
Alibainisha kuwa serikali ni
chanzo kwa kuwa imeunda vikundi vya wachimbaji wadogo lakini hawakuwahi
kusaidiwa zaidi ya kuahidiwa kila kukicha.
Ushirika wa wachimbaji walia na ahadi hewa.
Mwenyekiti wa Ushirika wa wachimbaji
wadogo Tarime Daud Makona alisema licha ya kusajiri ushirika wao mwaka 2010
hawajawahi kupata msaada wowote toka wizara ya Nishati na madini.
“Mauaji yanayoendelea
Nyamongo yana mkono wa serikali,maana kama wangekuwa wametuwezesha wachimbaji o
kusababisha vifo,naibu waziri Masele alikuja akaahidi,Waziri Profesa Sospeter
Muhongo ameelezwa,hakuna kitu”alisema kwa uchungu.
Wakati analalamika serikali
kutowasaidia Waziri Mkuu Mizengo Pinda ziarani Geita katika mgodi wa Mugusu
alihimiza uundaji wa ushirika wa wachimbaji wadogo kuwa watasaidiwa na
serikali.
Mtandao wa mashirika kukutana kutoa tamko.
Mratibu wa mtandao wa
mashirika yasiyo ya kiserikali Tarime(Tangonet)Bonny Matto alisema wanakutana
kesho(leo)na moja ya agenda ni kutoa tamko juu ya mauaji na ukatili unaoendelea
wilayani hapo.
Wakati huo huo habari zinadai
kuwa majeruhi wa mabomu yanayodaiwa kurushwa na polisi wakati wanawafukuza
vijana wanaodaiwa kuvamia kifusi hali zao zinaendelea vizuri.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment