UKOSEFU WA MAJI NYAMONGO WANANCHI WAZIDI KUIKABA KOO
HALMASHAURI.
Na Anthony Mayunga-Nyamongo.
Septemba 6,2012.
HALMASHAURI ya Wilaya ya
Tarime na Kampuni ya African Barrick North Mara wameendelea kulaumiwa na
wananchi kwa kushindwa kutatua tatizo la maji safi na salama kwa wakazi wa
Nyamongo.
Mapema wiki hii gazeti hili
lilifanya uchunguzi katika vijiji vinavyozunguka mgodi huo ili kubaini wa utekelezaji wa ahadi za serikali kwa wakazi
wa maeneo yanayozunguka mgodi huo baada ya chanzo cha mto Tighite kuharibiwa na
sumu toka mgodi wa Gokona unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick North
Mara.
Mwenyekiti wa serikali ya
kijiji cha Kewanja Tanzania O’mtima ameliambia blogu hii kuwa tatizo la maji
safi na salama ni kubwa kwa wakazi wa kijiji chake kwa kuwa serikali imeshindwa
kutimiza ahadi zake kwa wakati.
“Visima vimechimbwa na
kutelekezwa havitoi maji,badala yake kampuni inatum,ia gari kusambaza maji
ambayo serikali haijawahi kutuambia kama wameyapima na kubaini ni safi na
salama ,kwa kuwa kampuni inadai yanatoka mgodini”alisema.
Alisema baadhi ya maeneo
magari hayafiki kutokana na ubovu wa barabara hivyo wananchi wanapata shida
kubwa kupata maji “hakuna nafuu yoyote maana tungekuwa na maji ya bomba
tungesema limetatuliwa si kama ilivyo kwa kuletewa na gari maeneo mengine
halifiki”alisema O’Mtima.
Alikwenda mbali na kudai kuwa
viongozi wa serikali wamebaki kuzungumzia kwenye majukwaa wakati hakuna
utekelezaji wowote ya maagizo ya toka mwaka 2009.
Hata alibainisha kuwa
wamefunga mkataba na mgodi kuhakikisha kila mwaka wanawachimbia visima virefu
viwili na wameanza mwaka huu ambapo yeye katika kitongoji cha Magina ambacho
kina hali mbaya zaidi wamechimbiwa visima viwili.
Afisa maji.
Afisa maji wilaya ya Tarime
Madaraka Mahando alikiri halmashauri kuchimba visima lakini havijatumika kwa
kukosa maji huku akirusha lawama kwa jamii kuwa iliviharibu kabla ya kutumika.
“Kuna tatizo la kisiasa maana
wananchi baadhi ya maeneo walikata na
kudumbukiza udongo,taarifa zipo mpaka wizarani,na Mkurugenzi baada ya kuwa
umefuatilia amesema akitoka safari naye anataka tuzunguke naye kubaini vingapi
havifanyi kazi”alisema.
Alivitaja visima
walivyochimba kuwa ni vinne “vile vya Task Force kama serikali ilivyoelekeza
tumechimba Matongo viwili,Kewanja 1 na Nyakunguru kitongoji cha Itandura kimoja
lakini baadhi havifanyi kazi”alisema.
Hata hivyo alishindwa
kuthibitisha kama maji yanayosambazwa kwa gari na kampuni ni safi na salama na
yamepimwa na mamlaka gani.
Kampuni.
Mmoja wa maafisa katika mgodi
wa North Mara upande wa maji Saimoni Shayo alikiri kusambaza maji kwa gari
kutokana na kuwa maeneo mengi hayana maji kwa kuwa hakuna visima.
“Tunawasambazia maji ambayo
tunatumia sisi ,wakati wa usiku kwa kuwa hatuyatumii ndipo tunachota
kuwapelekea hata hivyo hayatoshi ,tuna mpango wa kuchimba visima viwili viwili
kila kijiji kwa kila mwaka”alisema.
Alidai kuwa mpango mwingine
ni kutandaza mabomba ambao unategemea kukamilika mwaka 2014,kuhusu visima vingi
kutokuwa na maji “si kwamba kote hakuna maji kwingine kuna madini tembo ambayo
hayafai kwa matumizi hiyo ni kitaalam si kwamba mgodi ndio umeharibu”alisema.
Hata hivyo alipingana na
halmashauri na kauli za serikali kutoa maagizo kwa kampuni kuhakikisha
wanawapatia vyanzo mbadala vya maji baada yamto Tighite kuchafuliwa na sumu
kutoka mgodini kwa madai kuwa hawana waraka wowote wa serikali wa kuwataka
kufanya hivyo.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment