ALIYEKUTWA NA BUNDUKI YA KIJESHI,RISASI 96 NA NYARA ZA TAIFA AFUNGWA
MIAKA 15 JELA.
Na Anthony Mayunga-Serengeti
Oktoba 30,2012.
MAHAKAMA ya Hakimu mkazi wa wilaya ya Serengeti imemhukumu mkazi
mmoja wa kijiji cha Motukeri kata ya Natta wilayani hapa kwenda jela miaka
15 kwa makosa ya kukutwa na bunduki ya kivita aina ya smg,risasi 96 na
nyara za taifa.
Aliyekumbwa na adhabu hiyo mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo Franco
Kiswaga ni Sabasaba Nyagekubwa(31) baada ya kukiri makosa yote manne
yaliyokuwa yanamkabili alipofikishwa mahakamani oktoba 29 mwaka huu.
Akitoa hukumu hiyo hakimu Kiswaga alisema mahakama hiyo imemtia
hatiani mtuhumiwa huyo baada ya kukubali makosa manne yaliyokuwa
yanamkabili ikiwemo kula njama za kuingia hifadhini bila kibali.
Makosa mengine ikiwa ni kukutwa na silaha ya kivita aina ya SMG ambaye
kisheria hapaswi kukaa nayo raia ,kukutwa na risasi 96 kinyume cha
sheria na kukutwa na nyara za taifa vipande 10 vya nyama ,mikia 6 ya
nyumbu na mayai manne ya mbuni.
“Kutokana na makosa hayo ambayo ni kinyume cha sheria na ambayo
yanaonekana kukithiri unahukumiwa kwenda jela miaka 15 ili iwe
fundisho kwa wengine ,kwa kuwa hatujui hiyo silaha kwa muda uliokaa
nayo umeitumiaje”alisema hakimu.
Katika utetezi wake mtuhumiwa aliomba mahakama imuhurumie kwa kuwa ni
kosa lake la kwanza kukaa na bunduki ya kijeshi na hakuweza kuisumbua
mahakama na ndiyo maana aliposomewa makosa yake alikubali yote.
Mapema oktoba 29 mwaka huu mwendesha mashitaka mrakibu msaidizi wa
polisi Alfred Marimi aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa
oktoba 25,majira ya saa 11 alfajiri mwaka huu katika kijiji cha
Motukeri alikamatwa akiwa na silaha,risasi na nyara za taifa.
Mbali nay eye watuhumiwa wengine waliokamatwa katika tukio hilo ni
Timoth Omoke(20) mkazi wa Kisii nchini Kenya na Pius Mayenga mkazi wa
kijiji cha Kyandege wilayani Bunda ambaye alikana mashitaka yote na
kurudishwa mahabusu hadi novemba 13,2012 itakapotajwa tena.
Mtuhumiwa baada ya kukubali kosa kesi hiyo iliahirishwa hadi oktoba 30
2012 siku moja kwa ajili ya hukumu,hata hivyo kosa moja la kukutwa na
nyara bado linaendelea novemba 13 mwaka huu kwa kuwa ni uhujumu uchumi wanasubiri kibali
ili iweze kusikilizwa.
Raia wa Kenya naye ahukumiwa.
Wakati huo huo Omoke raia wa Kisii nchini Kenya aliyekutwa nyumbani
kwa Nyagekubwa amehukumiwa kifungo cha miezi 6 jela ama kulipa faini
ya tsh,250,000= baada ya kubainika kuishi nchini bila kibali.
Omoke ambaye kibali chake kilibainika kuisha toka oktoba 7 mwaka huu
amepelekwa gerezani baada ya kushindwa kulipa kiasi hicho.
Mwisho.
wakamatwa na smg,rissasi 96 na nyara za taifa
WAKAMATWA NA SMG,RISASI 96 NYARA IKIWEMO MAYAI YA MBUNI,
Na Anthony
Mayunga-serengeti
Oktoba 29,2012.
WATU watatu wakazi wa
kitongoji cha Mageriga kijiji cha Motukeri kata ya Natta wilayani Serengeti
wamekamatwa na bunduki ya kivita aina ya Smg ,risasi 96,vipande 10 vya nyara za nyama pori na mayai 4 ya mbuni.
Tukio limetokea ikiwa ni siku chache katika kijiji cha
Makundusi kata hiyo tembo watatu walidaiwa kuuawa kwa njia ya sumu na meno yake
kuchukuliwa na watu wasiojulikana.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na watuhumiwa walikamatwa kwa kati ya
oktoba 25 na 26 katika maeneo tofauti ya wilaya za Serengeti na Bunda.
Kukamatwa kwao kunatokana na taarifa za wananchi polisi na
Tanapa ambao baada ya kukithiri matukio ya ujangili wanahaha kila kona
kuhakikisha mtandao huo unadhibitiwa kabla ya kuleta madhara makubwa.
Watuhumiwa wanaoshikiliwa na jeshi hilo ni Sabasaba Nyagekubwa (31)aliyekutwa na silaha
na risasi hizo zikiwa chini ya godoro wamelalia na kuwataja wenzake ambao ni Pius Mayengo mkazi wa
Kyandege wilayani Bunda na Timoth mkazi
wa Kisii Kenya.
Mkisii huyo alidai kuwa yeye alifika kwa mtuhumiwa huyo
kutoa mahari baada ya kumtorosha binti wa mtuhumiwa e ,madai ambayo yanapingwa
na baadhi ya majilani kwa madai kuwa huo ni mtandao wao wa kuvusha nyara kwenda nchini Kenya .
Habari kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinadai kuwa
Nyagekubwa alikamatwa oktoba 25 majira ya saa 11 alfajiri akiwa kwa hawala yake
na kuwampeleka nyumbani walipokuta silaha na risasi zikiwa zimefungwa kwenye
mfuko.
Bunduki hiyo aina ya SMG inadaiwa ni ya kisasa kwa kuwa ina stendi za kusimamisha wakati wa
kutenda uharifu,inadaiwa kuingizwa nchini kutokea nchi za Rwanda na Burundi kupitia
Kigoma na mtu mmoja ambaye inadaiwa aliingia kijijini hapo akijifanya mganga wa
kienyeji(Sangoma)
Sangoma huyo ambaye jina lake limehifadhiwa anasakwa alitajwa na mtuhumiwa kuwa ndiye
aliyeingiza silaha na risasi kwa lengo la kuwindia tembo na uhalifu mwingine na
kuwa hata soko la nyara ndiye anajua.
Watuhumiwa walikutwa harusini .
Kwa mjibu wa habari hizo inasemekana watuhumiwa wengine
walifanikiwa kutoroka baada ya kukutwa kwenye harusi na polisi katika kudhibiti
watu wote watuhumiwa wakafanikiwa kutoroka .
Wengine walitaarifiwa
kwa simu na kutoroka na nyara.
Habari hizo zinasema kuwa
watuhumiwa wengine walitaarifiwa na hawala wa Nyagekubwa kwa njia ya simu baada ya polisi kuchukua simu
ya mtuhumiwa na wengine huku moja ikifichwa ndiyo ilisaidia watuhumiwa kutoroka
na nyara walizokuwa nazo.
Mtuhumiwa anakesi
mbili za nyara kwa majina tofauti.
Imebaini kuwa mtuhumiwa Nyangekubwa anakabiliwa na kesi
mbili za kukutwa na nyara kwa majina tofauti na moja akidaiwa kuruka dhamana na
alipokamatwa kwa tukio kama hilo aliandika jina lake halisi.
Kesi ya kwanza aliandika jina la Ndalahwa Makaranga tukio la mwaka 2010 ambalo aliruka dhamana.
Silaha za kivita
huingizwa kutokea Kigoma.
Matukio ya watu kuingiza silaha kutokea mkoani Kigoma
yanazidi kushika kasi kwa ajili ya uwindaji wa tembo na uhalifu
mwingine,ikiwemo mtandao uliowahi kutikisa bunge lililopita kwa kuwataja
watuhumiwa ambao walipewa dhamana kinyamera licha ya kukamatwa na Smg 4 na
risasi zaidi ya 460.
Watuhumiwa walifutiwa
kesi.
Hata hivyo wale watuhumiwa waliokamatwa na shehena ya silaha
hizo na kelele kusambaa hadi bungeni walifutiwa mashitaka kinyamera katika
mazingira ambayo inadaiwa kutawaliwa na rushwa kwamba hawana mashitaka ya
kujibu.
Kuachiwa kwao kuliibua maswali mengi kutoka Tanapa kwa kuwa
wanakamata watuhumiwa na vielelezo
ikiwemo bunduki za kivita lakini polisi huwaachia linadaiwa kusimamiwa na
aliyekuwa mkuu wa upelelezi wilaya ya Serengeti,ambaye kutokana na kashifa hiyo
ameshushwa cheo na kupelekwa ofisi ya kamanda wa upelelezi mkoa wa kipolisi
Tarime na Rorya.
Hata hivyo baada ya kubainika waliachiwa kwa mazingira ya
rushwa watuhumiwa baadhi walikamatwa tena kwa maelekezo ya ngazi za juu za
jeshi la polisi na wako chini ya kamanda wa polisi mkoa wa Mara huku
wakiendelea kuwasaka wengine.
Mwisho,itaendelea.
mwanafunzi atuhumiwa kwa kuua kwa mshare familia yake yakimbia kwa kuhofu kuuawa
MWANAFUNZI WA
SEKONDARI ATUHUMIWA KUUA KWA MSHARE,
Na Anthony
Mayunga-Serengeti.
Oktoba 27,2012.
MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika sekondari ya Busawe
kata ya Majimoto wilayani Serengeti mkoani Mara Peter Lucas Wambura(17)anasakwa
na polisi kwa tuhuma za kumpiga mshare kifuani Chacha Damiani Mangali(18) na
kufa papo hapo.
Tukio hilo linalodaiwa kutokea oktoba 26,majira ya saa 2
mwaka huu usiku nyumbani kwa marehemu
Mangali limethibitishwa na uongozi wa kitongoji na polisi linahusishwa na wivu
wa kimapenzi.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho Daud Mgendi aliliambia
Mwananchi Jumapili kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni jilani yake na marehemu
alimpiga mshare kifuani na kufa papo hapo wakati anafungua mlango atoke nje ya
nyumba yake.
“Sababu hazijajulikana kuwa ni vijana waliokuwa wanalingana
huenda wamegongana kwa wanawake ,maana inaonekana marehemu alifungua mlango
akidhani ni mambo ya kawaida ndipo akapigwa mshare kifuani na kupiga kelele
kisha akakata roho”alisema Mwenyekiti.
Alisema mara baada ya kutenda unyama huo mtuhumiwa aligeuka
kama kichaa na kitishia usalama wa wananchi kwa kuwa alikuwa na upinde na
mishare mingi ,na kutokana na giza walishindwa kumdhibiti na kutokomea kusiko
julikana.
“Kumdhibiti ilikuwa vigumu kwa kuwa alionekana kuwa kama kichaa
na kutishia watu kwa kurusha mishare ovyo na kutokana na giza kila mtu aliamua
kuchukua tahadhari kwa kuwa hakuwa katika hali ya kawaida”alisema.
Baba mzazi wa marehemu Damiani Mangali akiongea na gazeti
hili kwa njia ya simu alisema kuwa kijana wake alikuwa hajaoa na wanahisi
huenda wamegongana kwa wanawake kwa kuwa hakuna madai mengine ambayo
ameyasikia.
“Kama ingekuwa deni tungesikia lakini kwa matatizo ya
wanawake mara nyingi huwa siri zao maana wote walikuwa vijana na
majilani,nilipigiwa simu na kaka yake na marehemu kuhusiana na tukio
hilo,tunaendelea kufuatilia chanzo lakini inauma kifo cha ghafla namna hii bila
hata kuwaeleza sababu”alisema.
Polisi wilayani hapa waanaendelea na uchunguzi ikiwa ni
pamoja na kumsaka mtuhumiwa ,ambapo wameomba wananchi watoe ushirikiano wa
chanzo na alikojificha kwa kuwa anaweza kusababisha madhara makubwa zaidi.
Hivi karibuni mwanafunzi mmoja wa kidato cha pili Mugumu sekondari
wilayani wilayani hapa Mwang’omba
Kegocha(16)amefikishwa katika mahakama ya wilaya kwa tuhuma ya kumchoma kisu Chacha Pasta(29)
Tukio ambalo linadaiwa lilitokea wakati wanacheza kamali
ambapo mtuhumiwa inadaiwa alikuwa ana mdai marehemu ths 5,000 na katika kudaiana wakakorishana ndipo
akamchoma kisu ubavuni na kufa papo hapo.
Mwisho.
FAMILIA YA MWANAFUNZI ANAYETUHUMIWA KUUA KWA MSHARE YATOWEKA KIJIJINI
KWA HOFU YA KUUAWA. NaAnthony Mayunga-Serengeti Oktoba 28,2012. FAMILIA ya mwanafunzi wa kidato cha tatu sekondari ya Busawe wilayani Serengeti Peter Lucas Wambura(17)anayesakwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga mshare kifuani Chacha Damiani Mangali(18)imetoweka kijijini hapo na malizao zikiwemo kuku kwa hofu ya kuuawa. Kutoweka kwao kunadaiwa kutokea oktoba 27,usiku mwaka huu baada ya kubaini kuwa Mangali ameaga dunia kufuatia kupigwa mshare wa sumu kifuani na mtuhumiwa akimtuhumu kuwa na uhusiano wa mapenzi na mdogo wake anayesoma kidato cha pili sekondari ya Busawe. Kwa mjibu wa habari kutoka kijijini hapo zilizothibitishwa na kamanda wa tarafa hiyo Inspekta Abdallah Idd ambaye alikuwa eneo la tukio zinadai kuwa familia hiyo ilitokomea kusikojulikana wakiwa wamebeba kila kitu ikiwemo kuku. Hofu yao ikiwa wananchi wangeweza kuwadhulu kwa kitendo kilichofanywa na kijana wao ,tukio ambalo linadaiwa kushuhudiwa na mama wa mtuhumiwa akimpongeza kijana wake kwa kumchoma mshare Mangali kwa kuwa alikuwa alikuwa anachangia kuharibu mwenendo wa mtoto wake kimasomo. Inadaiwa kuwa siku ya tukio marehemu Mangali alikwenda kwao na mtuhumiwa kwa lengo la kukutana na mpenzi wake huyo,tukio lililomuudhi mtuhumiwa na kuchukulia kama dharau kwa familia kwa kuwa walikuwa wameishamkata uhusiano wa mapenzi na binti huyo kwa kuwa ni mwanafunzi. “Walipigana kwanza hapo nje kwa kuwa wote walikuwa kama wanalingana ,mtuhumiwa baada ya kuona amezidiwa nguvu aliingia ndani na kutoka na upinde na mshare mwenzake akidhani ana tania ndipo akamchoma kifuani ,lakini akafanikiwa kuuchomoa na kutoa taarifa kwao kwa kuwa ni majilani”alisema mmoja wa wanafamilia jina limehifadhiwa. Hata hivyo familia ya marehemu ilimwita mama wa mtuhumiwa ambaye alisema alichokuwa anatafuta amekipata,wakati wanajiandaa kwenda hospitali aliaga dunia kwa kile kinachodaiwa alizidiwa na sumu yam share huo. Hata hivyo jamii imesema itamnasa mtuhumiwa na familia hiyo kwa kuwa hawataweza kukwepa zaidi ya kuchelewa kukamatwa,kwa kuwa tukio hilo ni la kusikitisha na ambalo liliibua hisia kali za watu. Habari za uhakika zinadai kuwa kutoroka kwa familia hiyo kulitokana na hisia za kuweza kuuawa kwa kuwa si watu wa jamii hiyo na ukoo wa aliyeuawa ni mkubwa ,huenda wakawa wamekimbilia maeneo mengine huku mtuhumiwa akawa hakuambatana nao. Mwenyekiti wa kitongoji hicho Daud Mgendi aliliambia Mwananchi kuwa tukio hilo lilitokea oktoba 26,majira ya saa 2 usiku mwaka huu nyumbani kwa marehemu likihusishwa na migogoro ya mapenzi. |
MUUZA UREMBO ANUSURIKA KUUAWA BAADA YA KUKUTWA AKIMPAKA
RANGI ZA KUCHA MKE WA BODABODA.
Na Anthony Mayunga-Mara
Oktoba 29,2012.
BODA BODA wa baiskeli mtaa wa Nyasho C,Manispaa ya Musoma
anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kujeruhi watu watatu waliokuwa wanamzuia
asimkate kwa panga muuza urembo baada ya
kumkuta akimpaka mke wake rangi ya kucha.
Tukio hilo limetokea oktoba 27 majira ya saa 6 mchana mwaka
huu katika maeneo ya Nyansho C’katika manispaa hiyo limethibitishwa na kamanda
wa polisi wa mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma.
Kamanda huyo amemtaja mtuhumiwa anayeshikiliwa kuwa ni Chacha Wandiba Masincha(25)ambaye ni boda
boda wa baiskeli ambaye aliwajeruhi kwa kuwakata na panga watu watatu ambao
walifikishwa hospitali kwa matibabu wakatibiwa
na kuruhusiwa.
“Mtuhumiwa alimkuta muuza urembo ambaye aliombwa na mke wa
mtuhumiwa Anita Chacha(19)akitaka kumpaka rangi mke wake alichukua panga kwa
lengo la kumkata ndipo watu wakajitokeza kusaidia asilete madhara “alisema
kamanda.
Alisema katika purukushani hizo watu watatu waliokatwa ni Nyairabu Mwita(22)mkulima na mkazi wa
Nyasho C’,Kichonge Wandiba(19)mkulima mkazi wa eneo hilo na Marwa
Wambura(20)ambaye ni boda boda eneo hilo.
“Majeruhi wametibiwa katika kituo cha afya Nyasho na
kuruhusiwa kuondoka kwa kuwa hali zao hazikuwa mbaya ,lakini mtuhumiwa tunaye
na tunategemea kumfikisha mahakamani taratibu zikikamilika”alibainisha kamanda
Mwakyoma.
Hata hivyo muuza urembo alikimbia na kuacha mali zake ambazo
ziliharibiwa na mtuhumiwa ambaye alionekana kupandwa na hasira kwa kile
kilichobainika kuwa ni wivu wa kimapenzi dhidi ya mkewe.
Baadhi ya mashuhuda walidai kuwa tatizo ni wivu wa kimapenzi
na kutoaminiana kati yake na mkewe kwa kuwa mfumo wa wanawake kupakwa rangi ni
la kawaida siku hizi.
Mwisho.
mwanafunzi atuhumiwa kwa kuua kwa mshare
MWANAFUNZI WA
SEKONDARI ATUHUMIWA KUUA KWA MSHARE,
Na Anthony
Mayunga-Serengeti.
Oktoba 27,2012.
MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika sekondari ya Busawe
kata ya Majimoto wilayani Serengeti mkoani Mara Peter Lucas Wambura(17)anasakwa
na polisi kwa tuhuma za kumpiga mshare kifuani Chacha Damiani Mangali(18) na
kufa papo hapo.
Tukio hilo linalodaiwa kutokea oktoba 26,majira ya saa 2
mwaka huu usiku nyumbani kwa marehemu
Mangali limethibitishwa na uongozi wa kitongoji na polisi linahusishwa na wivu
wa kimapenzi.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho Daud Mgendi aliliambia
Mwananchi Jumapili kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni jilani yake na marehemu
alimpiga mshare kifuani na kufa papo hapo wakati anafungua mlango atoke nje ya
nyumba yake.
“Sababu hazijajulikana kuwa ni vijana waliokuwa wanalingana
huenda wamegongana kwa wanawake ,maana inaonekana marehemu alifungua mlango
akidhani ni mambo ya kawaida ndipo akapigwa mshare kifuani na kupiga kelele
kisha akakata roho”alisema Mwenyekiti.
Alisema mara baada ya kutenda unyama huo mtuhumiwa aligeuka
kama kichaa na kitishia usalama wa wananchi kwa kuwa alikuwa na upinde na
mishare mingi ,na kutokana na giza walishindwa kumdhibiti na kutokomea kusiko
julikana.
“Kumdhibiti ilikuwa vigumu kwa kuwa alionekana kuwa kama kichaa
na kutishia watu kwa kurusha mishare ovyo na kutokana na giza kila mtu aliamua
kuchukua tahadhari kwa kuwa hakuwa katika hali ya kawaida”alisema.
Baba mzazi wa marehemu Damiani Mangali akiongea na gazeti
hili kwa njia ya simu alisema kuwa kijana wake alikuwa hajaoa na wanahisi
huenda wamegongana kwa wanawake kwa kuwa hakuna madai mengine ambayo
ameyasikia.
“Kama ingekuwa deni tungesikia lakini kwa matatizo ya
wanawake mara nyingi huwa siri zao maana wote walikuwa vijana na
majilani,nilipigiwa simu na kaka yake na marehemu kuhusiana na tukio
hilo,tunaendelea kufuatilia chanzo lakini inauma kifo cha ghafla namna hii bila
hata kuwaeleza sababu”alisema.
Polisi wilayani hapa waanaendelea na uchunguzi ikiwa ni
pamoja na kumsaka mtuhumiwa ,ambapo wameomba wananchi watoe ushirikiano wa
chanzo na alikojificha kwa kuwa anaweza kusababisha madhara makubwa zaidi.
Hivi karibuni mwanafunzi mmoja wa kidato cha pili Mugumu sekondari
wilayani wilayani hapa Mwang’omba
Kegocha(16)amefikishwa katika mahakama ya wilaya kwa tuhuma ya kumchoma kisu Chacha Pasta(29)
Tukio ambalo linadaiwa lilitokea wakati wanacheza kamali
ambapo mtuhumiwa inadaiwa alikuwa ana mdai marehemu ths 5,000 na katika kudaiana wakakorishana ndipo
akamchoma kisu ubavuni na kufa papo hapo.
Mwisho.
mwanafunzi atuhumiwa kwa kuua kwa mshare
MWANAFUNZI WA
SEKONDARI ATUHUMIWA KUUA KWA MSHARE,
Na Anthony
Mayunga-Serengeti.
Oktoba 27,2012.
MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika sekondari ya Busawe
kata ya Majimoto wilayani Serengeti mkoani Mara Peter Lucas Wambura(17)anasakwa
na polisi kwa tuhuma za kumpiga mshare kifuani Chacha Damiani Mangali(18) na
kufa papo hapo.
Tukio hilo linalodaiwa kutokea oktoba 26,majira ya saa 2
mwaka huu usiku nyumbani kwa marehemu
Mangali limethibitishwa na uongozi wa kitongoji na polisi linahusishwa na wivu
wa kimapenzi.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho Daud Mgendi aliliambia
Mwananchi Jumapili kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni jilani yake na marehemu
alimpiga mshare kifuani na kufa papo hapo wakati anafungua mlango atoke nje ya
nyumba yake.
“Sababu hazijajulikana kuwa ni vijana waliokuwa wanalingana
huenda wamegongana kwa wanawake ,maana inaonekana marehemu alifungua mlango
akidhani ni mambo ya kawaida ndipo akapigwa mshare kifuani na kupiga kelele
kisha akakata roho”alisema Mwenyekiti.
Alisema mara baada ya kutenda unyama huo mtuhumiwa aligeuka
kama kichaa na kitishia usalama wa wananchi kwa kuwa alikuwa na upinde na
mishare mingi ,na kutokana na giza walishindwa kumdhibiti na kutokomea kusiko
julikana.
“Kumdhibiti ilikuwa vigumu kwa kuwa alionekana kuwa kama kichaa
na kutishia watu kwa kurusha mishare ovyo na kutokana na giza kila mtu aliamua
kuchukua tahadhari kwa kuwa hakuwa katika hali ya kawaida”alisema.
Baba mzazi wa marehemu Damiani Mangali akiongea na gazeti
hili kwa njia ya simu alisema kuwa kijana wake alikuwa hajaoa na wanahisi
huenda wamegongana kwa wanawake kwa kuwa hakuna madai mengine ambayo
ameyasikia.
“Kama ingekuwa deni tungesikia lakini kwa matatizo ya
wanawake mara nyingi huwa siri zao maana wote walikuwa vijana na
majilani,nilipigiwa simu na kaka yake na marehemu kuhusiana na tukio
hilo,tunaendelea kufuatilia chanzo lakini inauma kifo cha ghafla namna hii bila
hata kuwaeleza sababu”alisema.
Polisi wilayani hapa waanaendelea na uchunguzi ikiwa ni
pamoja na kumsaka mtuhumiwa ,ambapo wameomba wananchi watoe ushirikiano wa
chanzo na alikojificha kwa kuwa anaweza kusababisha madhara makubwa zaidi.
Hivi karibuni mwanafunzi mmoja wa kidato cha pili Mugumu sekondari
wilayani wilayani hapa Mwang’omba
Kegocha(16)amefikishwa katika mahakama ya wilaya kwa tuhuma ya kumchoma kisu Chacha Pasta(29)
Tukio ambalo linadaiwa lilitokea wakati wanacheza kamali
ambapo mtuhumiwa inadaiwa alikuwa ana mdai marehemu ths 5,000 na katika kudaiana wakakorishana ndipo
akamchoma kisu ubavuni na kufa papo hapo.
Mwisho.
Subscribe to:
Posts (Atom)