KIKUNDI CHA VICOBA CHAPATA MKOPO
WA TREKTA,
Na Anthony Mayunga-Serengeti
3,0ktoba 2012.
KIKUNDI cha Jipe Moyo
(VICOBA)kijiji cha Nyambureti kata ya Nyambureti wilayani Serengeti kinatarajia
kulima ekari 30 za mpunga baada ya kupata mkopo wa trekta kutoka Suma JKT lenye
thamani ya tsh,mil.21.9
Kikundi hicho ni kwanza kati ya
vikundi vya Vicoba zaidi ya 80 vilivyopo wilayani hapo kupata mkopo wa treka
ambao wataulipa kwa kipindi cha miaka minne.
Mbele ya Mbunge wa jimbo hilo
Dk,Stephen Kebwe katibu wa kikundi hicho---- alisema wanategemea kulima ekari
hizo za mpunga kama mradi wa kikundi lakini kwa mwanachama mmoja mmoja
watamlimia ekari moja kwa gharama nafuu .
Alisema watawalimia na wananchi
wengine kwa kulipia ili waweze kulipa mkopo huo ambao wanaamini wataweza kwa
kuwa malengo yao kwa kuwa kikundi hicho kiongeza uzalishaji ili kuongeza mapato
ya kikundi na wanakikundi wenyewe.
“Kama kikundi tumechangia
tsh,mil.6.9 ili kupata kikundi ambazo zimetokana na kununua hisa wenyewe,faini
na faida inayotokana na mikopo ya wanachama kwenye mifuko yetu ya asilimia 10
kwa tsh,100,000=”alisema.
Alisema licha ya kuwa kikundi
kina miaka miwili wanachama wameweza kunufaika kwa kukopa kwa ajili ya biashara
zao,hatua ambayo inaonyesha mafanikio kwa kuwa lengo ni kuhakikisha wananufaika
kiuchumi.
Kuhusu malengo ya baadae ni kuwa
mawakala wa kuuza pembejeo katika eneo hilo ili kuwarahisishia wananchi kupata
kuzipata haraka tofauti na sasa wanalazimika kwenda wilayani zaidi ya kilometa
50.
Akizungumzia Changamoto zinazowakabili
alisema mtaji mdogo,trekta kutokuwa na tela ambalo lingewasaidia kusomba mizigo
mbalimbali ikiwemo mbolea kupeleka shambani na kumwomba Mbunge awasaidie
kututua changamoto hiyo.
Naye Katakata Sangi mmoja wa
wanachama alibainisha kunufaika kwa mikopo kwenye kikundi ambao umekuza mtaji
wake kutoka 200,000 alizokuwa nazo sasa amefikisha tsh,mil.1 kwa kuuza soda na
dizeli na anasomesha watoto wawili sekondari
kupitia mfuko wa elimu wa kikundi.
Kwa upande wake mbunge Dk,Kebwe
aliwataka walitunze vizuri ili liweze kuwanufaisha kiuchumi,kwa kuwa watakuwa
wameachana na kilimo cha mkono na hivyo wataongeza uzalishaji.
Kikundi hicho cha Vicoba
kilianzishwa juni 27,2010 kikiwa na wanachama 30 kati yao wanaume wakiwa 18 na
wanawake 12.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment