VURUGU ZAZUKA NYAMONGO NYUMBA
ZAIDI YA 35 ZATEKETEZWA,10 ZAHARIBIWA,WAKIGOMBEA VIFUSI VYA DHAHABU.
Na Anthony Mayunga-Mara
Oktoba 6,2012.
NYUMBA 35 zimeteketezwa kwa moto
na nyingine 10 kubomolewa katika kitongoji cha Gonsala kijiji cha Kewanja eneo
la Nyamongo na watu wanaodaiwa wa koo ya Wanyabasi chanzo ikiwa ni ugomvi wa
mawe yanayodaiwa ya dhahabu kutoka mgodi wa Gokona.
Tukio hilo limethibitishwa na kaimu
kamanda wa mkoa wa kipolisi Tarime na Rorya na uongozi wa kijiji cha Kewanja
linadaiwa kutokea oktoba 5,majira ya kati ya saa 2 -3 usiku mwaka huu .
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji
cha Kewanja Tanzania O’mtima amesema chanzo ni vijana wanaovamia vifusi vya
mawe yaliyotupwa na mgodi wa African Barrick North Mara (intruda)ambao wameweka
mipaka ya kwa misingi ya koo ya Wanyabasi na Wanyamongo.
“Kabla ya kutokea unyama huo kuna
kijana mmoja alikatwa katwa na pikipiki mbili kuchomwa moto kumbe ni koo ya
Wanyabasi ,tukio limetokea oktoba 5,majira ya saa 12 jioni na baadae ikatolewa
taarifa kuwa amefariki,usiku ndipo kundi la vijana wa koo hiyo wakavamia na
kuchoma nyumba hizo”alisema.
Alisema mgogoro huo umekuwepo kwa
muda ambapo vijana wa koo ya Wanyabasi wamekata mipaka ndani ya kijiji chake
ambapo hawaruhusu vijana wa koo ya Wanyamongo kwenda kuchukua mawe
yanayodhaniwa kuwa na dhahabu yaliyotupwa na mgodi ,hali ambayo hawakubaliani
nayo.
“Mgodi uko kijijini kwangu lakini
vijana wa koo ya Wanyabasi kutoka vijiji na kata zingine wameweka masharti
wakati wote ni Intruda na hawana haki ya kumiliki kifusi hicho kama ambavyo wa
kijijini kwangu hawana haki,huo ndio mwanzo wa vurugu”alisema.
Katika vurugu hizo anadai hakuna
mtu aliyejeruhiwa wala kufa lakini vitu vimeporwa na watu wanahaha kuhama kwa
kuwa taarifa zimezagaa kuwa watarudi usiku kufanya unyama zaidi.
Muathirika.
Augustino Sasi mmoja wa
waliothiriwa na vurugu hizo anadai nyumba 6 za familia yak wake zimeteketezwa
“ni jilani na walipokuwa polisi lakini unyama unatendeka wako kimya wanamaliza
kazi ndipo wanajitokeza tumeshangaa sana mbona wakisikia Intruda magari
hujazana na mabomu kwa nini hili hawakujitokeza haraka”alisema.
Alisema mgogoro huo unatakiwa
kupatiwa ufumbuzi kwa kuwa madhara yake yatakuwa makubwa zaidi kwa jamii hizo
ambazo kimsingi ni ndugu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
serikali ya kijiji cha Wegita kata ya Kibasuka inakokaa koo ya Wanyabasi Kermani Nyakiha alisema matukio hayo
yamefanywa na vijana wala wazee hawahusiki na hawajui,lakini wamekaa kikao ili
kukomesha hali hiyo,
Kaimu Kamanda wa polisi .
Kaimu Kamanda wa mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya Sebastian
Zakaria alikiri kuwa hali ilikuwa mbaya na sasa kumetulia baada ya kupeleka
nguvu kubwa za kuzuia vurugu hizo.
“Ni kweli nyumba zimechomwa ni
kama 28 hivi ni vibanda walikuwa wametegesha hawakai watu na zingine za kudumu
kama 9 zimebomolewa lakini hazikuwa na watu ndani “alisema.
Alikiri baada ya mtu mmoja kuuawa
ambaye hakumtaja jina lakini anatoka koo ya wanyabasi ndio kichocheo cha
vurugu,pia ugomvi wa vifusi ambavyo anakiri viko kijiji cha Kewanja vinapelekea
uhasama.
“Tumekaa na koo ya Wanyabasi leo
lengo ni kuweka mambo sawa tumeshirikisha wazee wa mila lakini koo ya
Wanyamongo vijana wanawadharau wazee wa
mila hawataki kuwasikiliza ,lengo ni
kuwapatanisha”alisemakamanda.
Aidha vurugu hizo zilipelekea
huduma za usafiri kusitishwa kwa kuwa kuna baadhi ya magari yaliharibiwa
,lakini hali imetulia na magari yanayofanya safari zake Tarime na Mugumu
yanapita kwa ulinzi wa polisi.
Kuhusu ulinzi anadai umeimarishwa
na wameongeza nguvu kuhakikisha wanadhibiti vurugu hizo.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment