Mbunge wa jimbo la Serengeti Dk,Stephen Kebwe ameapa kuonana na waziri wa miundo mbinu ili kumaliza utata ambao umeanza kujitokeza wa jiji la Mwanza kutaka kubadili jina la uwanja wa ndege kuitwa Serengeti wakati tayari Serengeti wameishapata kibali cha kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa wa serengeti
MABADILIKO YA JINA LA UWANJA WA
NDEGE MWANZA ,WAKUU WA MIKOA WATOA KAULI TOFAUTI.
Na Anthony Mayunga-Mara
Oktoba 4,2012.
SAKATA la Serengeti kutumika kama jina jipya la uwanja wa ndege wa kimataifa Mwanza wa wakuu wa mikoa watoa kauli tofauti , mkuu wa mkoa wa Mara adai wanajadiliana vizuri
wa Mwanza akisisitiza kuwa mchakato uko
idara ya uchukuzi.
Hivi karibuni Mbunge wa jimbo la
Serengeti Dk,Stephen Kebwe akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mjadala
unaoendelea Mwanza kutaka kutumia jina hilo aliwataka Mwanza watafute jina
jingine.
Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tupa
akiongea na Mwananchi kuhusiana na sakata hilo alikiri kuwa mjadala huo upo na
wanaendelea kujadiliana na mkuu wa mkoa wa Mwanza na watapata muafaka.
“Hilo linazungumzika mimi na
mwenzangu mkuu wa mkoa wa Mwanza tunaendelea kujadiliana naamini tutapata
muafaka,maana hili halitashindikana tutapata muafaka mzuri na hata ngazi za juu
zipo zitatoa ushauri”alisema.
Alisema kuwa na viwanja vingi
itasaidia kupata wageni wengi ,hivyo mjadala huo wanalenga kuumaliza vizuri kwa
majadiliano ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda vizuri na kuahidi kuwa taarifa
itatolewa .
Wakati Mkuu wa Mkoa wa Mara
akidai wako kwenye majadiliano mazuri Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist
Ndukilo alipoulizwa na Mwananchi mjadala huo unaendeleaje na hatima yake
alisema suala hilo litatolewa taarifa.
“Nasema mtajulishwa na wala si
sasa maana mchakato wake umeishapelekwa wizara ya uchukuzi kama mnataka taarifa
fuatilieni huko “alisema kwa mkato.
Wakati majibu yakitofautiana ya
wakuu wa mikoa mbunge wa jimbo la Serengeti dk,Kebwe amesisitiza kuwa msimamo
wake wa kuwataka waache kutumia jina hilo kwa kuwa tayari wameishapata kibali
cha ujenzi wa uwanja wa kimataifa wa Serengeti ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya
Rais Jakaya Kikwete kwa wakazi wa wilaya na Taifa ilimkurahisishia wageni
kufika hifadhini kwa urahisi.
Pia amesema anakwenda kuonana na watendaji wa wizara ya mambo ya anga ili
kumaliza mvutano huo ambao hauna maslahi kwa taifa kwa kuwa Mwanza wangeweza
kukuza hifadhi za Saanane na Lubondo kwa kuita uwanja huo.
Aliuchukulia mjadala huo
unaendeshwa Mwanza kufifisha juhudi za watu ambao wameishajitokeza kujenga
uwanja huo kama Kampuni ya Singita Grumeti Reserves kupitia kwa mmiliki wake
Paul John Tudor raia wa Marekani.
Uwanja wa ndege wa Kimataifa
Serengeti unajengwa kwa ubia wa kampuni ya Grumeti reserves,halmashauri na
Serikali kuu,tayari wana hati ya ekari 5,000 na wananchi wameishalipwa fidia
ikiwemo kuhamishwa kwa shule ya Msingi Burunga na kujengwa maeneo mengine.
Rais Kikwete katika kampeini zake
na mikiutano mingine ikiwemo hotuba za mwisho wa mwezi amekuwa akizungumzia
dhamira ya kujenga uwanja huo Mugumu lengo likiwa ni kuwawezesha wageni kutua
hapo na kuingia hifadhi ya Taifa ya Serengeti na mapori ya akiba kwa madai kuwa
wanapotelemkia Kilimanjaro ama Mwanza wanasafiri umbali mrefu na hayo ni
malalamiko yao.
Kujengwa uwanja huo kutafungua
milango ya kiuchumi kwa jamii na taifa kwa kuwa kutakuwa na ongezeko la wageni
wengi ambao walikuwa hawapendi kufika hifadhi hiyo kutokana na umbali na ubovu
wa miundo mbinu ya barabara.
Hivi karibuni katika wiki ya
tamasha la utalii mkoani Mwanza hoja ya kutaka jina hilo litumike kwa ajili ya
uwanja wa ndege wa Mwanza ambao unakarabatiwa kwa lengo la kuwa wageni
wataongezeka iliibuka na kuzua mjadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya
kijamii.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment