Subscribe:

Ads 468x60px

Vurugu zuka nyamongo nyumba zaidi ya 35 zateketezwa kwa moto




 

VURUGU ZAZUKA NYAMONGO NYUMBA ZAIDI YA 35 ZATEKETEZWA,10 ZAHARIBIWA,WAKIGOMBEA  VIFUSI VYA DHAHABU.
Na Anthony Mayunga-Mara
Oktoba 6,2012.

NYUMBA 35 zimeteketezwa kwa moto na nyingine 10 kubomolewa katika kitongoji cha Gonsala kijiji cha Kewanja eneo la Nyamongo na watu wanaodaiwa wa koo ya Wanyabasi chanzo ikiwa ni ugomvi wa mawe yanayodaiwa ya dhahabu kutoka mgodi wa Gokona.

Tukio hilo limethibitishwa na kaimu kamanda wa mkoa wa kipolisi Tarime na Rorya na uongozi wa kijiji cha Kewanja linadaiwa kutokea oktoba 5,majira ya kati ya saa 2 -3 usiku mwaka huu .

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kewanja Tanzania O’mtima amesema chanzo ni vijana wanaovamia vifusi vya mawe yaliyotupwa na mgodi wa African Barrick North Mara (intruda)ambao wameweka mipaka ya kwa misingi ya koo ya Wanyabasi na Wanyamongo.

“Kabla ya kutokea unyama huo kuna kijana mmoja alikatwa katwa na pikipiki mbili kuchomwa moto kumbe ni koo ya Wanyabasi ,tukio limetokea oktoba 5,majira ya saa 12 jioni na baadae ikatolewa taarifa kuwa amefariki,usiku ndipo kundi la vijana wa koo hiyo wakavamia na kuchoma nyumba hizo”alisema.

Alisema mgogoro huo umekuwepo kwa muda ambapo vijana wa koo ya Wanyabasi wamekata mipaka ndani ya kijiji chake ambapo hawaruhusu vijana wa koo ya Wanyamongo kwenda kuchukua mawe yanayodhaniwa kuwa na dhahabu yaliyotupwa na mgodi ,hali ambayo hawakubaliani nayo.

“Mgodi uko kijijini kwangu lakini vijana wa koo ya Wanyabasi kutoka vijiji na kata zingine wameweka masharti wakati wote ni Intruda na hawana haki ya kumiliki kifusi hicho kama ambavyo wa kijijini kwangu hawana haki,huo ndio mwanzo wa vurugu”alisema.

Katika vurugu hizo anadai hakuna mtu aliyejeruhiwa wala kufa lakini vitu vimeporwa na watu wanahaha kuhama kwa kuwa taarifa zimezagaa kuwa watarudi usiku kufanya unyama zaidi.

Muathirika.
Augustino Sasi mmoja wa waliothiriwa na vurugu hizo anadai nyumba 6 za familia yak wake zimeteketezwa “ni jilani na walipokuwa polisi lakini unyama unatendeka wako kimya wanamaliza kazi ndipo wanajitokeza tumeshangaa sana mbona wakisikia Intruda magari hujazana na mabomu kwa nini hili hawakujitokeza haraka”alisema.

Alisema mgogoro huo unatakiwa kupatiwa ufumbuzi kwa kuwa madhara yake yatakuwa makubwa zaidi kwa jamii hizo ambazo kimsingi ni ndugu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Wegita kata ya Kibasuka inakokaa koo ya Wanyabasi  Kermani Nyakiha alisema matukio hayo yamefanywa na vijana wala wazee hawahusiki na hawajui,lakini wamekaa kikao ili kukomesha hali hiyo,

Kaimu Kamanda wa polisi .
Kaimu Kamanda wa  mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya Sebastian Zakaria alikiri kuwa hali ilikuwa mbaya na sasa kumetulia baada ya kupeleka nguvu kubwa za kuzuia vurugu hizo.

“Ni kweli nyumba zimechomwa ni kama 28 hivi ni vibanda walikuwa wametegesha hawakai watu na zingine za kudumu kama 9 zimebomolewa lakini hazikuwa na watu ndani “alisema.

Alikiri baada ya mtu mmoja kuuawa ambaye hakumtaja jina lakini anatoka koo ya wanyabasi ndio kichocheo cha vurugu,pia ugomvi wa vifusi ambavyo anakiri viko kijiji cha Kewanja vinapelekea uhasama.

“Tumekaa na koo ya Wanyabasi leo lengo ni kuweka mambo sawa tumeshirikisha wazee wa mila lakini koo ya Wanyamongo  vijana wanawadharau wazee wa mila  hawataki kuwasikiliza ,lengo ni kuwapatanisha”alisemakamanda.

Aidha vurugu hizo zilipelekea huduma za usafiri kusitishwa kwa kuwa kuna baadhi ya magari yaliharibiwa ,lakini hali imetulia na magari yanayofanya safari zake Tarime na Mugumu yanapita kwa ulinzi wa polisi.

Kuhusu ulinzi anadai umeimarishwa na wameongeza nguvu kuhakikisha wanadhibiti vurugu hizo.

Mwisho.

0 comments:

Post a Comment