VIONGOZI WA SERIKALI WAKUNJUA
MAKUCHA KWA WATAKAOKEKETA WATOTO WA KIKE.
Na Anthony Mayunga-Serengeti
Novemba 7,2012.
VIONGOZI wa serikali mkoani Mara wamevun ja kimya na kutoa onyo kwa wananchi watakaojihusisha na shughuli
za kukeketa watoto wa kike kuwa watashughulikiwa kwa kuwa ni uvunjaji wa
sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 na makosa ya kujaamiina ya mwaka 1998.
Hatua hiyo inakuja huku
tayari maandalizi ya ukeketaji watoto wa kike katika wilaya mbalimbali mkoani
Mara yakipamba moto kutoka kwa wazazi na walezi.
Mkuu wa mkoa wa Mara John
Tupa akiongea na Mwananchi kwa njia ya simu amesema viongozi wa ngazi zote
wameishaelezwa mikakati ya kukabiliana na wale watakaokaidi.
“Ukeketaji ni ukiukwaji wa
sheria kama serikali tunatambua mwaka huu watafanya hivyo,kwa kushirikiana na
wadau mbalimbali ikiwemo viongozi wa dini zote,watendaji wa ngazi zote na wazee
wa mila lengo ni kuhakikisha wanakomesha ukatili huo”alisema.
Alikwenda mbali zaidi na
kudai hata ngariba wameishaambiwa kuachana na kazi hiyo inayokiuka sheria za
nchi”hatutasita kuwakamata wataokiuka kwa kuwa ni makosa ,naomba kila mmoja
atimize wajibu wake”alisema mkuu wa mkoa.
Kuhusu viongozi wa kisiasa
hasa wa kuchaguliwa kuogopa kuwakemea wananchi kwa hofu ya kupoteza kura
alisema mkakati wa sasa ni kuhakikisha wanahusika kwa kuwa kila kiongozi
anatakiwa kuwa mlinzi wa sheria za nchi.
Aliwataka wanaharakati
mbalimbali wanaojihusisha na utoaji wa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa
kijinsia hususan ukeketaji wa watoto wa kike washirikiane na serikali.
Rpc kanda maalum.
Kamanda wa mkoa wa kipolisi
Tarime na Rorya Justus Kamugisha alipoulizwa mikakati waliyonayo kukabiliana na
watakaohusika alisema ,suala hilo wanalichukulia
kama ilivyo kwa makosa mengine ya jinai.
“Ukeketaji ni kosa la jinai
tutawakabili wahusika kama ilivyo kwa makosa ya jinai,maana kama ni elimu
wameambiwa sana kuhusu madhara ya ukeketaji wanatakiwa kuepuka kujihusisha na
matukio hayo ili kuepuka mikono ya serikali”alisema.
Hata hivyo alisema sekta ya
maendeleo ya jamii inatakiwa kujipanua zaidi ili kuweza kuwafikia wananchi
waachane na uvunjaji wa sheria .
Mratibu wa mradi wa Childrens
Dignity Forum (Cdf) Joram Wimmo alisema katika utafiti wao walibaini kwa mwaka
huu watoto zaidi ya 4,000 wako hatarini kukeketwa kwa wilaya moja tu ya Tarime.
Hatua ambayo anaona kuwa
inahitaji ushirikiano mkubwa na wadau mbalimbali kwa kuwa wilaya zingine za
Serengeti,Rorya,Bunda,Butiama na Musoma kuna jamii hizo zinazohusika na
ukeketaji,hivyo idadi huenda ikawa kubwa zaidi.
Kutokana na tafiti hizo kwa
sasa wamejikita kutoa elimu kwa jamii hasa ya koo 5 za Kikurya kwa
kuwashirikisha wazee wa mila ili watambue madhara na waweze kuachana na kazi
hiyo.
Hata hivyo imebainika kuwa
baadhi ya wazazi waishio mpakani mwa Tanzania
na Kenya
kupeleka watoto huko kwa ajili ya kukeketwa na watarudi baada ya kupona.
Mwaka 2010 licha ya serikali
kupiga marufuku lakini ukeketaji wa watoto wa kike uliendelea kwa kuambatana na
sherehe za kifahali huku watoto waliokeketwa wakipitishwa mbele za ofisi za
serikali ikiwemo polisi bila kuchukuliwa hatua.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment